MAMMAMIA,
Mkuu.
Umekuwa mkali sana. Calm down.
Kwa sababu mambo ya Muungano hayakuwa yanazungumzwa kwa uwazi basi mambo yamechanganyika sana kiasi tunashindwa kuchambua nini ni nini!
Kitu kimoja ni kuwa Zanzibar leo kutokana na Muungano unavyoendeshwa haina mamlaka ya kiinchi,kila kitu kinapitia Muungano. Ukivunjika muungano ni kuwa wanarudisha ile sovereignty yao yote. Hiyo itakuwa hatua kubwa kwao. Sasa hili la kufa itategemea umakini wa viongozi wao watakaowachagua.
Viongozi wao wakirudisha siasa za ubaguzi basi kweli watapata tabu lakini kama wataendeleza spirit ya GNU basi hawa watu wanaweza kukwamuka kwa haraka. Mkuu zipo nchi za Sychelles, Cape Verde na Mauritious hapa Afrika ambazo ni nchi za visiwa na zipo wapi kimaendeleo ukilinganisha udogo wao na idadi ya wakaazi wake na maendeleo ya Tanzania?
Tatizo hata la Tanzania ,Tanganyika ni viongozi tu , siasa za kubabaisha na kutokuwa na priorities.
Maliasili iliyopo na nguvu kazi isiyotumika ipasavyo,Tanzania sio wa kuwa kwenye orodha ya mkiani kabisa kwa umaskini.
Ni maoni yangu kuwa Zanzibar wamebanwa sana na Muungano kiasi hawawezi kufanya maamuzi ya maana ya kuiendeleza Zanzibar hasa wanapokosa nguvu za kisheria kushirikiana na mataifa mengine duniani kama Zanzibar.
Kwa manung'uniko wanayotoa wazanzibari ni kuwa kuna mambo mengi ambayo si ya Muungano lakini hakuna mechanism ya wao kutafuta development partners bila ya kupitia Muungano. Hilo linakwamisha juhudi zao za kujiletea maendeleo.