Muungano wa Tanganyika na Zanzibar: Una faida gani na kwa manufaa ya nani?



Habari ndio hio Mkuu,


,"Without any question, the manner and the implications of the union between Tanganyika and Zanzibar is the most misunderstood aspect of Tanzania's political development. It may not matter very much when foreigners get confused, but unfortunately there are many times when Tanzanians themselves appear to misunderstand" - JK Nyerere.
 
Da hata mimi umenichanganya, nafika mwisho nimesahau mwanzo! Tukitengana ccm inapoteza wabunge kama 40 toka visiwani. Watakomaje?
 
Da hata mimi umenichanganya, nafika mwisho nimesahau mwanzo! Tukitengana ccm inapoteza wabunge kama 40 toka visiwani. Watakomaje?

Kumbee, nahisi na wao CCM unawachanganya akili ndio maana hadi leo hawajui wafanye nini wanaukingia kifua tu!
 
[quote="theophilius,

Mkuu.
Huyu rais ana kofia mbili ni rais wa Muungano, lakini wakati huo huo ni Rais wa Tanganyika.
Usijichanganye wala usikubali kuchakachuliwa. Kabla ya kutoa jibu la suali lako gumu, nikuchukue kabla ya Muungano.
Nani alikuwa rais wa Tanganyika? Nyerere
nani kwa upande wa Tanganyika aliingia mkataba na rais wa Zanzibar?...Nyerere.

Nani alitayarisha hati za muungano?...... Mwanasheria mkuu wa Tanganyika kwa idhini au amri ya Nyerere.

Je Tanganyika na Zanzibar waliunganisha kila kitu au kila jambo? Jawabu ni hapana. sasa kama ni hivyo yale mambo ya Tanganyika yaendeshwe na Nani? Rais wa Tanganyika au vipi? Hapa ndio unaipata dhana ya kuvaa kofia mbili.

Je Muungano una haki au mamlaka ya kuifuta serikali ya Tanganyika au Rais wake? muungano hauna mamlaka hiyo.
Muungano ni kiumbe wa Tanganyika na Zanzibar, bila ya hawa hakuna Muungano. sasa vipi tena baada ya Muungano mmoja apotee?....ukiwa na jibu la kitandawili hiki basi umeondoa utata wa muungano huu.

sasa wacha nichangie juu ya suali uliloliuliza.

Mkuu. Urais wa muungano ni taasisi ya muungano.
Lakini kwa bahati mbaya hakuna mipaka ya kueleweka baina ya mambo ya Tanganyika na mambo ya Muungano. Yote yamechanganywa katika kapu moja. na kwa hiyo, wanatenda mambo kwa kuboronga tu, ubabe na kubahatisha bahatisha. Vile mtu anavyotafsiri mwenyewe na kama hatapata kuulizwa au kuwekewa kipingamizi hujihisi ametenda sawa.

Lakini ugumu unaongezeka yanapokuja masuali ambayo moja kwa moja yanagusa ubia, mamlaka ya Zanzibar moja kwa moja. Kama katiba ya Muungano.

katiba ya Muungano ni zao la hati(mkataba) ya Muungano kwa hiyo inahitaji majadiliano ya Tanganyika na Zanzibar kwa pamoja. Muungano hauwezi kujiundia mamlaka ambayo haukupewa na Tanganyika na Zanzibar.

Nani anatoa mamlaka kwa Muungano? Serikali ya Tanganyika na Serikali ya Zanzibar. Hawa kupitia majadiliano wanaweza kuongeza au kupunguza mamlaka ya Muungano wa Tanzania....sasa kazi ipo hapa..serikali ya Tanganyika inapokuwa imeji-dissolve kienyeji nani watakaa kujadiliana? ndio tunaishia kuwa huu si muungano...ni "Changa la Macho", "mazingombwe" ausanii at its best!
 
mkuu maswali yako ni mazuri sana-cha ajabu viongozi wetu hawataki kuiachia zanzibar-yaan mi ni moja ya vitu ambavyo sivipendi na vina nishangaza sana-sijui kwa nini wa-zenji tunawahusisha kwenye mambo yetu-
kuna baazi ya viongozi wanadai eti kwa sababu za kiusalama ndo maana zenji wanaikumbatia-hivi jamani kwani Kenya na Uganda zipo mbali na Tanzania? Kweli hii nchi haina viongozi
 
Hakuna kosa kubwa nyerere alilofanya kama kuleta huu mungano, kuliko hata siasa za ujamaa, kwa sababu moja kubwa ni kuwa Tanganyika imetoka kwenye ukoloni halafu ikawa mkoloni.
Sasa kitu kingine ni kuwa tunafanya makosa makubwa kuona kuwa wazanzibari wanafaidika na huu muungano, ukweli ni wachache ambao ni wafanya biashara na wanasiasa, sasa hao ndio wanaofanya muungano uendelee.
Tunaitaji kiongozi mwendawazimu kuuvunja, sio wanafiki
 

Mkuu.
Unaongea kama vile Zanzibar haikuwepo kabla ya Muungano.
Kama Zanzibar haikuwepo au haikuwa ikijiendesha yenyewe kabla ya muungano utakuwa uko sahihi katika usemayo.

Kama Zanzibar ilikuwepo na ilikuwa inafanya biashara na nchi nyengine basi sioni kama itakuwa ni tatizo ikitokea Muungano kuvunjika.

Unakumbuka soviet Union....nchi nyingi zimeibuka baada ya umoja huu kuvunjika. zenyewe zinajiendesha na zina mahusiano na Russia mpya. Wengine wananunua gesi kutoka Russia kukidhi mahitaji ya nishati katika nchi zao.

Wapo watanzania wana majumba UK, US, Dubai, wengine wazee wa vijisenti wana fedha katika benki za nje. Kwa hiyo hii pia si issue ya kuogopesha watu.

Kama unafuatilia Dubai investments wao wanajenga properties na kuziuza kwa wageni,katika nchi nyingi wanakaribisha wageni kununua makaazi katika nchi zao...ni biashara. na hao wenye majumba au biashara nyengine watakuwa na uamuzi wa kuendelea na bishara au kufunga biashara zao kulingana na mazingira. wakiamua watauza majengo yao na kuelekea kule wanakoona kunafaa, au naturalisation ya uraia pia ni jambo ambalo linaweza kufanyika.

Hapa ndio inakuwa ni muhimu na jambo bora muungano kama utavunjika, uvunjike kwa salama na sio kwa vita. Kura ya maoni ndio njia ya salama zaidi. Mambo huwa yanajadiliwa kabla kulingana na kura ya yes au no. na kunakuwa na mipango ya utekelezaji kulingana na matokeo ya kura hiyo ya maoni.

Tatizo lipo kwa hao viongozi ambao hawaoni mbali.
 
huyu aliyeleta hii ramani Unimaps.com - Tanganyika & Zanzibar, 1886 sikubaliani nayo. kama muungano ukivunjika & i pray for that nchi zitarudi kama ilivyukuwa kabla ya muungano.

binafsi mimi ni mzaliwa wa tanga tena kwetu ni vile vijiji vilivyo katika pwani ya bahari ya hindi kuelekea mombasa barabara ya horohoro ukisimama pwani ya kijiji chetu pemba unaiona ileee!... na sidhani kama tukiletewa kura ya maoni ati tangayika au znz! kamwe hatuwezi tukachaguwa znz. wazee wangu wengi wa pale kijijini wanayemfahamu ni nyerere hawana historia wala ufahamu wowote kuhusu znz.. iweje leo hii mje muwaambie kwamba wao ni wa znz! this must be JOKE!
 
hio ramani ni ya zamani sana-then naamini tanganyika hawawezi kukubali kuwaachia zenji pande hizo zote-naamini hata kwa vita tutapigania ardhi yetu
 

Binafsi naona kuna sababu nyingine labda za msingi ambazo may be viongozu wa CCM wanazilinda ndio maana wanakumbatia huu muungano, hata kudiriki kutaka suala lake lisijadiliwe kwenye katiba mpya!

Watu hatuuongei tu huu muungano is a pain in the ass!
 

Mkuu naunga mkono, na sisemi kwamba naona wanzanzibar ndio wanaofaidika hapana, ila naona kwamba Zanzibar wanapewa VETO kwenye mambo ya bara (sio Tanzania) wakati bara hatupewi, hapo natatizika.
 
Chanzo tafadhali.
 
Binafsi naona kuna sababu nyingine labda za msingi ambazo may be viongozu wa CCM wanazilinda ndio maana wanakumbatia huu muungano, hata kudiriki kutaka suala lake lisijadiliwe kwenye katiba mpya!

Watu hatuuongei tu huu muungano is a pain in the ass!
naomba hii nchi ipate kiongozi ambaye atakuwa tofauti na wengine ili hili swala la muungano aje alifanyie kazi-ili huu muungano ufe
 
naomba hii nchi ipate kiongozi ambaye atakuwa tofauti na wengine ili hili swala la muungano aje alifanyie kazi-ili huu muungano ufe

Halafu Swali ni kwamba; Sasa kama tuna wawakilishi/ wabunge kutoka Zanzibar kwenye bunge letu la Muungano, kuna haja gani tena kutaka Bunge la Zanzibar lihusishwe tena katika maamuzi....wakati bunge letu halihusishwi katika bunge (baraza la wawakilishi) la Zanzibar!
 
Majibu ya maswali yote yatapatikana iwapo Tanganyika Italivua Koti la Muungano.

Matatizo ya muungano huu nimefuatilia kwa kina na mijadala yake,kitu ambacho nimekiona mkanganyiko wa mambo ulianzia pale Tanganyika ilipo jufuta kimnya kimnya na kujigeuza kua Tanzania.

Hebu ndugu muuliza masuali Jaribu kujaalia kua Tanganyika ipo leo na zanzibar ipo halafu tukawa na kitu cha muungano yani Tanzania,halafu Tanganyika ikafanya mambo yake binafsi kama ilivyo Zanzibar leo,na Tanzania ikashuhulika na Mambo ya muungano tu,Je ungali jiuliza maswali hayo leo?

Na huo mfumo niliokueleza ndio mkataba wa muungano ulivyoelekeza,haukusema kabisa kua baada ya muungano Tanganyika au na pia Watu wanapaswa kufahamu kua Muungano haukua wa mambo yote bali ni baadhi tu ya mambo.

Hapa ndio Maana wazanzibari hadi hii leo wanachojua nikua Tanzania ni Tunda la Muungano,Ndio maana wanataka kilichomo ndani ta tunda wakigawe sawa sawa.
Ama kosa lililofanywa na watanganyika wenyewe lakijiingiza ndani ya KOTI (MUUNGANO) na kujigeuza jina na kijifanya wao(Tanganyika) ndio Muungano na muungano ndio wao(Tanganyika),hili wazanzibari hatutaki kulijua tunachojua ni makubaliano yetu tu yaliomo ndani ya mkataba wa muungano.

Nikisema makubaliano ninamaana ya liokubaliwa na nchi mbili yani Tanganyika na Zanzibar sio yaliobadilishwa na Bunge la Tanganyika lililojibadilisha jina na kujiita Bunge la Muungano.

Wito wangu kwa Watanganyika waanze harakati za kuidai nchi yao kwanza halafu ndio tufikire tena kama iko haja ya kuungana au tukakutane Muungno wa Af.Mashariki.
 

Wew wakikluruhusu au wasikuruhusu ujadili tu ama kwa Wazanzibari kwao ni ruhusa kuujadili.
 

Kama unakusudia kwenye Katibahii inayojadiliwa mtalazimika iwe hivyo hadi pale mtakapojivua Gamba la Tanzania na kusema tunaunda katiba ya Tanganyika na hilo ndugu yangu hamko tayari hata siku moja.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…