Wana JF, nakwazika na saa zingine nasikia kupata wehu na mambo kadhaa ya Jamuhuri yetu ya Muungano. Naomba mnisaidie majibu au kutoa hoja na mwelekeo katika haya yafuatayo:
1. Tangayika na Zanzibar (nchi mbili) ziliungana na kutengeneza nchi mbili, Tanzania na Zanzaibarhii inawezekanaje??? marais wawili?? Katiba Mbili? tena kwa mujibu wa katiba ya Zanzibar iliyofanyiwa marekebisho mwaka jana, Zanzibar ni nchi huru yenye mipaka yake?
Tangu 1964 hapajawahi kuwa na nchi moja kwenye huu Muungano. Wazanzibari tukijuwa kuwa kuna zanzibar na Tanganyika na kiongozi wetu mkuu Karume alishakataa Azimio la Arusha na kusema mwisho chumbe! Wimbo wetu wa Taifa tukiutambua kuwa ndio wimbo wa Taifa, na viongozi wa nje tukiwapokea kwa heshima zote za kitaifa. Tulikuwa tukitumia bendera yenye jembe kila sehemu ya serikali. Hapo nafikiri utaelewa kuwa nchi ni mbili na hivyo ndivyo tulivyokubaliana!
2.Tanganyika iko wapi katika Muungano au Watanganyika (kama sehemu mojawapo ya muungano) tunatambulika au kuji-identify wapi katika Muungano?
Tanganyika mliamuwa kujiita Tanzania na majina yote mliyabadilisha na kuwa Tanzania. Zaidi ya mabadiliko ya jina hakuna kilichobadilika. Rais, Waziri Mkuu, Bunge, mahakama,jeshi na kila kitu hakijawahi kubadilika. Hata Mzanzibari (kwa jina) alipopewa urais alipewa urais wa Tanganyika. Hapo mwanzo Makamo wa Rais alikuwa akishughulikia mambo ya Zanzibar lakini Tanganyika mkaona hata yeye awe Makamo wa Rais wa Tanganyika. Kimipaka nafikiri bado ni ile ile na ndio sehemu inayoshughulikiwa na Rais na Taasisi zake na Bunge!
3. Je kipi ni sahihi kutamka au kutambulika kati Tanganyika na Tanzania bara??
Sahihi kutamka ni Tanzania na wala sio Tanganyika au Tanzania Bara kwani Tanganyika ilishabadili jina na kuitwa Tanzania bara ingekuwa sahihi kama kungekuwa na Tanzania mbili. Kuna Zanzibar na Tanzania tu.
4. Najua kwenye hesabu inawezekana 1 + 1 = 2 lakini huwezi kuunganisha nchi mbili ukapata nchi mbili, hapa si hakuna muungano??? Au sisi ni shirikisho?
Kwa hesabu za Kitanzania na muungano wao ni sahihi kwa 1+1= 2 kwani tumezoelea utopian (nadharia).
5. Katika kuandika katiba, katiba ya WAZANZIBAR iliandikwa na wao wenyewe tena na referendum yao wenyewe bila kuhusishwa Tanzania bara. Sasa sisi wa bara tunapotaka kuandika katiba kwanini iwe ndio katiba ya Muungano pia???
Sababu ni kuwa bado hamjakuwa tayari kujivua Gamba na kusema wazi kuwa nyie ni Tanganyika ndani ya Gamba la Tanzania. Sasa unapovaa gamba inbidi ushirikiane na wale uliowavalia gamba lao. Lengo la Muungano wa Tanzania lilikuwa usawa kwa nchi zote lakini hili la kujitwallia madaraka yote ni uvaaji wa Gamba!
6. Watanganyika tuna haki gani katika muungano kuandika katiba yetu wenyewe kwanza (inayotuhusu sisi na watu wetu hao zaidi ya Million 40) kabla ya waZanzibari kuhusishwa??? NAONA TANGANYIKA TUNAINGILIWA NA KUNYIMWA HAKI YA KUTAMBULIKA (KAMA SEHEMU MOJAWAPO YA MUUNGANO) KULIKO HATA MNAVYOFIKIRIA?
Watanganyika hamuingiliwi bali mnajipendekeza kwa Muungano. Kama mliweza kuwafanya CCM wajivue magamba kwanini gamba hili nalo hamlilazimishi kuvuliwa. Naomba ujiulize kwenye makelele haya mengi ya Katiba nani (labda Mbatia) anaesema kuwa Katiba kwanza iwepo ya Tanganyika kabla ya Muungano? Kelele ni ohh wawakilishi wa Zanzibar wasiwe sawa na wa Tanganyika, hii inaonyesha mtizamo wa kuidai Tanganyika? Halafu hamkosi kitu kwa kujibadilisha jina.
7.Kwanini ya ZANZIBARI yawahusu ZANZIBARI TU na ya Hayatuhusu WABARA,wakati ya BARA yawahusu WANZANZIBARI??? au ndio mambo ya chako changu, changu changu??
Hivyo sivyo hata kidogo. Toka lini Zanzibar ikahoji mambo mnayofanya? Mbona mnahoji na mnataka kuidhamini Zanzibar katika mikopo? Halafu kule bungeni mbona mambo yote yanayozungumzwa ni ya huko tu? Na hata hotuba ya Rais hata zile za mwisho wa mwezi huwa zinahusu huko tu?/ Kiko wapi hicho cha ya bara kuwahusu Wazanzibari?
8. Inakuaje Rais wa Muungano ndio rais wa Bara (Tanganyika - ambayo haipo) tena ni Rais wa Zanzibar pia?? hapohapo eti Wazanzibar Wana Rais wao tena????
Bwana mdogo Rais wa Zanzibar ni mmoja tu na Rais wa Tanzania si Rais wa Zanzibar bali Rais wa Tanzania ni Rais wa Tanganyika. Kihesabu Tanganyika kama kawaida ndio wanaonufaika kutumia Tanzania na sio wazanzibari hata katika hili la urais.
9. Inakuaje Tanzania ndio Tanganyika pia???? yaani hata sijui nauliza nini nahisi naanza kuchanganyikiwa???
Hapo juu ulishasema hiyo ndiyo changu changu chetu changu! Kama hali hii bado inawaridhisha basi hizo ni silka.
10. Kama sisi ni muungano kwanini Wazanzibar wampigie kura Rais Wetu (wa bara) na sisi hatumpigii kura kumchagua Rais wao (zenji)????? Huu ni muungano wa aina gani huu???? muungano nusu (partial) au????
Bado unarudu kule kule mdogo mpe pipi ili alale mkubwa afanye atakavyo.
11. Hivi sasa naambiwa KATIBA YA ZANZIBAR NI KINYUME NA KATIBA MAMA YA MUUNGANO na ETI pia kutokana na marekebisho ya KATIBA YA ZANZIBAR ya Mwaka jana HUU MUSWADA wetu wa katiba ni batili HIYO PIA ni kwa mujibu wa KATIBA YA JAMUHURI YA MUUNGANO kwa kuwa haujahusisha Baraza la wawakilishi la Zanzibar na Rais na Mwanasheria wau sijui......Hapa nahisi haya mambo yanazunguka katika duara la kizungu zungu (in cycles) na yaani inakua ni kama ile ishu ya nani alianza kati ya kuku na yai na ndipo hunifanya nijione kama akili yangu imefika mwisho wa kufikiria...which is which jamani????
Kwani kilichoanza ni kipi? kuwepo kwa Zanzibar na baadae ndio kuja Muungano au kulianza Muungano na baadae kukazaliwa Zanzibar? Jawabu ni kuwa Zanzibar ilianza na hapo ndipo neno mama linapokuja. Mtoto hawezi kumzaa mwana. Nionavyo mimi kama Tanganyika kwa jina jipya mlilolichukuwa ndio utaifa wenu ulianza hapo basi hiyo Katiba ya Muungano itakuwa Katiba mama kwenu kwani utaifa wenu ulikuja kwa Katiba hiyo. Hali ni tafauti kwa Zanzibar kwani kwao Katiba ya Zanzibar ni Katiba mama kwa vile utaifa wao haukufutika. Kufanya mabadiliko ni sawasawa na mtindo wa dada zetu kutafuta wigi kuondowa nywele wanazozioneya haya!
12. Haya yote ya muungano ambayo na Zanzibar inahusika yananichanganya akili sana naweza kuchanganyikiwa mwenzenu! Je sisi (Tanzania Bara) tunaweza kutumia utaratibu gani utakao tuwezesha kuandika katiba yetu wenyewe kwanza kabla na waZanzibar kuhusika?
Watanganyika hamjawahi kufanya kitu na Wazanzibari wakakuzuieni. 55 haikuzuiwa na Wazanzibari bali aliezuia ni Baba wenu wa Taifa. Isitoshe Wazanzibari mbona wameshaanza harakati za kutaka mjivue Magamba lakini kwa hili si CCM si CHADEMA nyote mnalingangania gamba!
13. Nashindwa hata kuendelea sijui hata niulize nini, yaani sijui????
14. Wakati hapo hapo kuna ANGALIZO hili hapa chini (alilolisema Nyerere) nalinukuu...
"....On april 26, 1964, two independent African states surrendered their sovereignty to one New country - the United Republic of Tanzania......"
Pengine alikuwa sahihi kuwa nchi mbili zilitowa sovereignity kwa nchi moja mpya (Tanganyika ilijibadilisha jina. Nikifikiri naona hakukosea kwani nchi mbili hizi kilichotolewa muhanga ni sovereignity basi lakini nchi ziliendelea kuwepo. Katika kupoteza sovereignity Zanzibar ndiyo ilipata hasara kwani Tanganyika ilivaa Gamba na kujinyakulia hiyo sovereignity iliyoacha na Zanzibar na Tanganyika. Ni kizungumkuti kikubwa mmoja anapojidai kujilsha kitu kwa kutumia Gamba!
......naona kwa mujibu wa marekebisho ya katiba (ya Zanzibar - 2010) Zanzibar washajichululia 'SOVEREIGNTY' yao Sisi Bara tunasubiri nini????
Hadi sasa bado hawajaipata bali walichofanya ni kuwakumbusha waliovaa Gamba kuwa Zanzibar bado ni nchi na waliovaa Gamba hawataki kutoka kwenye Gamba kwani kufanya hivyo hiyo sovereignity wanayotumia peke yao itabidi apewe Tanzania ya kweli na iwe inagawiwa sawa kwa wote. Hilo wavaa Magamba hawataki!
15. Yaani hata sijui, hivi naruhusiwa kujadili muungano au siruhusiwi???...
Msaada wenu jamani!......