Najijua
JF-Expert Member
- Nov 5, 2010
- 1,040
- 182
Daima huwa napata shaka sana juu ya kiburi cha zanzibar juu ya muungano na inavyo onekana sisi ndio tunalazimisha, wameanzisha wimbo wa taifa tumekaa kimya, wameanzisha bendera ya taifa lao tumekaa kimya, wamefanya marekebisho ya kayiba yao na kuitambua zanzibar kama taifa tumekaa kimya na sasa wameenda mbali kwa kuanzisha bodi yao ya mikopo na bado tumekaa kimya ina maana wao ndio werevu pekee?
BARAZA la Wawakilishi limepitisha Muswada wa Sheria ya kuanzisha Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu Zanzibar na baadhi ya wawakilishi wamependekeza Bodi hiyo ipewe fedha na Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu ya Tanzania (HELSB).
Uamuzi huo wa Zanzibar, utakuwa umeondoa suala la elimu ya juu kutoka kuwa la Muungano na kuwa suala la Zanzibar na linaweza kuzua changamoto ya Muungano kuhusu fomula ya kugawana fedha za HELSB, kwa kuwa mpaka sasa fomula ya kugawana fedha za misaada inaonekana kuwa changamoto inayoendelea.
Angalizo: Sidhani kama muungano unafaa kuendelea kuwepo tena kama waloungana hawauheshimu!!