Muungano wa Tanganyika na Zanzibar: Una faida gani na kwa manufaa ya nani?

Muungano wa Tanganyika na Zanzibar: Una faida gani na kwa manufaa ya nani?

tumebakiza siku 12 kabla ya maadhimisho ya miaka 46 ya muungano wa mataifa ya tanganyika na zanzibar yaliyozaa tanzania hapo jumatatu aprili 26.

Imekuwa ni jadi na utamaduni kufurahia sikukuu hii na kuwaenzi waasisi wa muungano wetu mwalimu nyerere na mzee abeid karume kwa matamasha, gwaride na shangwe kebekebe.

Lakini imekuwa ni dhambi, tena yenye sumu kali kwa mtu yeyote kuhoji au kutaka kuuchambua muungano huu.

Lengo lango si kuuliza historia au kudadisi uhalali wa muungano wa tanzania bali ni faida zake na manufaa yake kutokana na mfumo wa muungano kwa mujibu wa katiba ya tanzania, mamlaka zilizoko kama vile mahakama, bunge, baraza la wawakilishi na ni vitu gani ambavyo ni kwa ajili ya muungano na vipi si kwa ajili ya muungano.

Je kwa nini tuliweka vipengele fulani viwe masuala ya muungano na vingine visiwe?

Je muungano huu una maana gani ikiwa vipengele ilivyoko vinakingana na azma kuu ya kuunda taifa lenye nguvu na umoja?

Je wananchi wa tanzania, wananufaika vipi na muungano huu na wanaathirika vipi kutokana na muungano huu na mfumo wake?

Je kuna haja ya kuupitia muungano na ama kupengua vipengele fulani au kuunganisha kila kitu na kuwa na sura moja bila kutofautisha ya hili la watanganyika au watanzania bara na lile ni la wazanzibari?
muungano huu kwa muundo wake watanganyika hawautaki na wazanzibar ndio kabisa hawautaki,sioni sababu ya umuungano kuendelea kuwepo maana znz hawautaki kwa kuwa wanataka nchi yao iwe kidini,wakati tanganyika ukiangalia ukubwa wa jimbo huko bara na znz haviendani.matatizo yako mengi znz hata kimataifa wanasema wanaonewa kwa hiyo nadhani ni bora sana uvunjike
 
Inawezekana kulikuwa na mambo mengine ambayo tuliochelewa kuzaliwa hatuyajui.
Naomba kufahamishwa kwanin tuliungana?
Kwanin Tanganyika ikafutwa?
 
Kwanini zenj ijitawale tanganyika hata kuitaja iwe dhambi?
Kwanini Rais wa muungano akienda zenj awe chini ya rais wa SMZ?
 
Nawe nakuuliza ukiweza kujibu ndilo pia jibu la sababu ya kuungana kwa tanganyika na zenji.........."kwa nini mwanaume na mwanamke wanaoana?"
 
Karibuni kwenye jukwaa hili, tujadiliana faida mbalimbali za muungano na hasara tutakayoipata muungano ukivunjika.
 
tuliungana kwa malengo ya kuidhibiti zanzibar amabyo wakati huo ilikua na ushawishi mkubwa wa kiuchumi na mipango ya maendeleo kwa watu wake.pia tuliungana ili kuidhibiti ili lengo la kuifanya serikali hiyo kuwa ya Kislam,
pia tayari kulikua na maingilianio sana kati ya dar es salaam na zanzibar sasa bila ya udhibiti tungeshindwa kufanya propaganda zetu za siasa za ujamaa ambazo zilikua zipo mbioni kutekelezwa, hivyo serikali isingeweza kuwa na jirani yenye soko huria ambapo raia wake wapo huru kuishi popote na yenye kufata sera za capitalism katika kuendeleza uchumia wao.
kwa vile sera zetu za mpendwaa wetu zilikuwa ni za kutuweka katika kambi za "kuzalisha mali" vijiji vya ujamaa...kama animal farms basi isingekuwa rahisi kupiga propaganga za yomba yomba wakati jirani anakula mkate na siagi...tukampindua na tukamuanganisha .....
 
Inawezekana kulikuwa na mambo mengine ambayo tuliochelewa kuzaliwa hatuyajui.
Naomba kufahamishwa kwanin tuliungana?
Kwanin Tanganyika ikafutwa?

Kamuulize Dorado na Kasim hanga, nafikiri hata Jumbe anaweza kukuambia, but be careful.
 
Sababu ziko mingi zilizosabisha sisi kuungana kwanza nyerere alikuwa mjanja sana..angalia hiz sababu:-kwanza baada mapinduzi walitaka waungane ili kuilinda zanzibar dhidi ya wavamizi na pia nyerere aliogopa kuwa zanz inaweza kuwa kichochoro cha kuficha wavamizi na nyingine nyerere aliona mbali sana kuwa zanz ni ambayo ina resources nyingi na si tegemezi na pia wazanzibar na wadanganyika walishachanyika sana sababu ya koloni alilowatawala
 
Panafricanism 10 %

Coldwar 90% .What a shame it should have been the other way round tatizo baadhi so called father of nation(exception of Nyerere, Nkrumah) walikuwa wa binafsi mno.
 
Tuliungana kwa sababu ya Umbumbumbu na UOGA wa wazanzibar (Kumuogopa sultani kuwa anaweza kurudi baada ya mapinduzi) na UJANJA wa Nyerere.
 
Sababu ziko mingi zilizosabisha sisi kuungana kwanza nyerere alikuwa mjanja sana..angalia hiz sababu:-kwanza baada mapinduzi walitaka waungane ili kuilinda zanzibar dhidi ya wavamizi na pia nyerere aliogopa kuwa zanz inaweza kuwa kichochoro cha kuficha wavamizi na nyingine nyerere aliona mbali sana kuwa zanz ni ambayo ina resources nyingi na si tegemezi na pia wazanzibar na wadanganyika walishachanyika sana sababu ya koloni alilowatawala

When these discussions were at an advanced stage, Nyerere is said to have called in his Attorney-General at the time, British expert Roland Brown, and asked him to draft a Union Agreement without anybody knowing. In the case of Zanzibar, the Attorney-General, Wolf Dourado, is said to have been sent on a one-week ‘leave' and instead a Ugandan lawyer, Dan Nabudere (accoridng to his own account which was corroborated by Babu), was brought in to advise Karume on the draft submitted by Tanganyika. Both Brown and Nabudere were present in the Karume-Nyerere discussions. One can speculate that one reason why Dourado was not involved was because he was ‘inherited' from the previous ZNP/ZPPP regime and the revolutionary government was hesitant to involve him in such a sensitive matter. (Othman).

Hebu nitafsie hii sijaielewa vizuri
 
Kama muungano uko matatan wazenji wote wenye hatam bara wajikane ili tuone nin cha kufanya make wao hata hawaon uchungu wa maendeleo duni. Mfanowe ni mawaziri wa .,.na....? Washikaji inaeleweka.
 
Inawezekana kulikuwa na mambo mengine ambayo tuliochelewa kuzaliwa hatuyajui.
Naomba kufahamishwa kwanin tuliungana?
Kwanin Tanganyika ikafutwa?
hakuna mambo yoyote yaliyosababisha muungano tusiyoyajua-
kifupi viongoz wetu waliungana tu bila hata wao kujua..kifupi akili zao ndo ziliishi hapo-hata wao hawana sababu za kuungana
 
Sababu ziko mingi zilizosabisha sisi kuungana kwanza nyerere alikuwa mjanja sana..angalia hiz sababu:-kwanza baada mapinduzi walitaka waungane ili kuilinda zanzibar dhidi ya wavamizi na pia nyerere aliogopa kuwa zanz inaweza kuwa kichochoro cha kuficha wavamizi na nyingine nyerere aliona mbali sana kuwa zanz ni ambayo ina resources nyingi na si tegemezi na pia wazanzibar na wadanganyika walishachanyika sana sababu ya koloni alilowatawala
Hapo nilipo bold-kati ya tanganyika na zanzibar ni ipi yenye resources nyingi?mbona unashindwa hata kufikiri?

When these discussions were at an advanced stage, Nyerere is said to have called in his Attorney-General at the time, British expert Roland Brown, and asked him to draft a Union Agreement without anybody knowing. In the case of Zanzibar, the Attorney-General, Wolf Dourado, is said to have been sent on a one-week ‘leave’ and instead a Ugandan lawyer, Dan Nabudere (accoridng to his own account which was corroborated by Babu), was brought in to advise Karume on the draft submitted by Tanganyika. Both Brown and Nabudere were present in the Karume-Nyerere discussions. One can speculate that one reason why Dourado was not involved was because he was ‘inherited’ from the previous ZNP/ZPPP regime and the revolutionary government was hesitant to involve him in such a sensitive matter. (Othman).

Hebu nitafsie hii sijaielewa vizuri

Huu muungano ni as if ni wa watu 2
 
Nina shauri sana watanzania wenzangu kama tunataka Muungano huu udumu katika taifa hili basi ni sharti kila raia aache tabia ya unafiki,woga na mambo yote ya kizabizabina.Maana yangu hapa ni kwamba kwa wenye dhamana na wafuasi wa tabaka zote ni lazima wapende amani itokayo mioyoni mwa walio wengi kuliko kulinda amani kwa nguvu ya dola maana amani inayolindwa na umma ama watu[civils]ni amani ya MUNGU.Mathalani kuapa kulinda muungano unao nung'unikiwa na umma ni batili mbele ya Mungu.KWA machache haya natoa salaam zangu za dhati kwa watanzania wote hasa ambao wamekuwa katika manung'uniko juu ya mfumo wa muungano huu[JMT] ambao upo kwa nguvu ya dola na si nguvu ya Mungu[umma],muungano ambao pia husherehekewa kwa nguvu ya pesa isiyo ya amani.Kama kuna siku itatokea umma ukaunda muungano wa amani ni pale nchi zitakapo unda shirikisho ambalo litalinda wigo wa kisiasa wa asili badala ya kupoteza historia ya kila kizazi.AMANI YA MUNGU ITULINDE TUPATE RAHA MIOYONI MWETU.
 
nimeipenda hyo binafs had leo sizijui hzo faida, ila nashangazwa na wenzang wanaposema zipo nyng bila walau kutaja japo moja tu!!!!!
 
Back
Top Bottom