Muungano wa Tanganyika na Zanzibar: Una faida gani na kwa manufaa ya nani?

Muungano wa Tanganyika na Zanzibar: Una faida gani na kwa manufaa ya nani?

Tunahitaji kutafakari sana kwa hili, Mzee wetu aliwahi kusema kuwa muungano umesaidia usalama kwa bara.
Kwa sasa jama hawa mamwinyi wana kila kitu chao kuanzia bendera, wimbo, rais, na mambo mengine mengi. In Short if we were to vote today then i would vote for a big NO. na sitabadili huu msimamo. Tuachane nao tu manake maandamano kibao hasa ule ugonvi wa deposits za mafuta yalogunduliwa. Katika bajeti ya taifa nadhani wanapata mgao mara mbili kutoka muunganoni na mapinduzini!
Ni wakati wa kuwa na Tanganyika yetu ndo tuungane nao. Huu unafiki wa serikali mbili ni dhambi kubwa ya taifa!
 
Wakuu wote wa serikali 2 na 3 njooni hapa mtupe elimu sisi watanganyika.Binafsi siioni faida ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar.Kila napouliza naambiwa ''Nyerere na Karume''.Je kuna sababu za maana sana mkatushawishi.Bora wazenji wao wanajiachia kwao na bara.Mtanganyika anapata faida gani sasa. Halafu kwa nini kina CCM wanaonekana wajuaji na kuziona peke yao hizo faida?
 
Huu muungano umekaa kisiasa zaidi,hauna manufaa kwa wananchi,unawanufaisha matajiri viongozi.
 
Mkuu binafsi nakuunga mkono wa kutoona faida za huo Muungano ila kwa haraka haraka na jibu la kukurupuka ni kwamba faida yake kwangu ni kuwa baada ya kufunga ndoa nilienda honey moon Zenji, wife aliinjoi mbaya kula vyakula vya baharini pale Forodhani............kwangu ni hayo tu, ngoja wanaojua faida zaidi waje kutueleza.
 
Huu muungano umekaa kisiasa zaidi,hauna manufaa kwa wananchi,unawanufaisha matajiri viongozi.



ndio maana sitaki kujadili upuuzi huu tena marakwa mara tungejajili maji,elimu,ajira,afya,resouces zetu na faida ya wananchi sio huu utumbo wa muungano
 
Muungano wa Marekani ni Nchi 52 hauna kero za muungano wala wizara ya muungano Pia zile Nchi ndogo hazina Utitiri wa Viongozi na wabunge Kama ilivyokuwa kwa Zanzibar wana Lundo la Viongozi lukuki huku Mishahara Yao ikilipwa na Tanganyika wao pato Lao ni Dogo sana hawawezi hata kulisha kijiji . Wapo Wajanja wanafaidika na zile Pesa zinazotengwa kwa ajili ya kutatua kero za muungano wao wanazitafuna kijanja Hata Lile Fungu yaani Mgao wa Fedha za Zenji toka Hazina napo kuna wajanja wananifaika ! Hao sasa Ndio wanapenda serikari 2 ili kero ziendelee na wao wazidi kuneemeke kwani Tanganyika bila Zanzibar Hakuna muungano

Lengo la Karume na Nyerere ilikuwa ni Muungano wenye Faida kwa Pande zote mbili , yaani Zanzibar wana Faida ya kupata Umeme,chakula na mengineyo toka Tanganyika huku upande wa Bara wakifaidika na Usalama wa mipaka Baharini nk . Kipindi kile Faida zilikuwa zinaendana kidogo ,lakini siku hizi Zanzibar amekuwa na Faida kubwa zaidi ya Tanganyika Ndio Maana akipiga Chafya tz bara anaugua haraka kisha kuhaha kuitafuta dawa ya kuwatibia wote .Faida ya muungano ipo Zanzibar pekee lakini Tanganyika hainufaiki na Muungano sasa.
 
hivi kama mtu akiamua kuwatwanga , zanzibar itaokoa kitu gani ? Kama mnajali usalama mngewapa wale wahuni wajenge ghorofa karibu na ikulu ?
hao ni wauza sembe kama wafanyavyo ikulu..kifupi ni Business Partners wa Ikulu ya JK na Riz1..
 
Mwenye Faida na Muungano ni Zanzibar tu, ebu fikiria Wazanzibar wanaishi Tanganyika wanamiliki Ardhi ,biashara wengi ni waajiliwa ktk Sekta mbali mbali wanaishi kwa Amani pasipo Ubaguzi wowote wala Vikwazo . Hii ni faida kubwa sana, Wabunge wao wanapata Posho Dodoma,wengine ni Mawaziri huku Tanganyika kihalisia Zanzibar ndiye ananufaika na muungano huku Tanganyika yeye akihaha kulinda Muungano kwa pesa nyingi , wakati Watanganyika wanabaguliwa Zanzibar hawaruhusiwi kumiliki Ardhi ,Ubaguzi wa kidini ni Vioja vingi tu Hivyo Tanganyika haina Faida na Muungano kabsa.
 
Mkuu binafsi nakuunga mkono wa kutoona faida za huo Muungano ila kwa haraka haraka na jibu la kukurupuka ni kwamba faida yake kwangu ni kuwa baada ya kufunga ndoa nilienda honey moon Zenji, wife aliinjoi mbaya kula vyakula vya baharini pale Forodhani............kwangu ni hayo tu, ngoja wanaojua faida zaidi waje kutueleza.

kweli ni faida ya kukurupuka!yani pesa inayopotea kushugulikia makero ya muungano si zingejenga visima tukaacha kushea maji na vyura
 
shukrani kwa members wote waliochangia opinions zao mwaka 2010-2011.ama hakika nimejifunza elimu nzuri juu ya muungano.
 
Huko n kuchukua risk kwan vta wakat wowote inaweza tokea hata km uchumi n mkubwa au mdogo na uelewe haimaanish kwamba yukijitenga bas ndo mambo yatakua shwar bali lazma kutakua na mtafaruko wa hapa na pale,tuweishika znz kiulinz hata kwa miaka mia kumi bt we cant drop it ,ni kwa kujihami kwan u cant determine war , fungua macho and keep yo heard up na uone mbali



Vita kati ya Nani na nani,wakati majeshi yataendelea kua yapo chini ya muungano.?Vita inatokea endapo nchi moja inataka kujitenga kwa hiyari na nyingine inailazimisha kijeshi.Muundo wa serikali yatu utajenga amani zaidi .Mana utakua na fursa nzuri ya kuunda serikali ya umoja wa kitaifa kwa pande zote kutoa viongozi kwenye serikali ya Muungano.
Na ni vyema tukajiuliza ni kwa nini wazanzibari wengi hawaupendi Muungano wa serikali mbili japo watu wanasema kwamba wao ndo wananufaika zaidi.
Jambo jengine ni Muungano kuvunjika ,huo ndio upotoshaji hakuna mahali tume zote zilizoundwa wamependekeza kuvunja Muungano.Watu wanachosema ni utekelezaji na uendeshaji wa nchi mbili na serikali mbili zenye mamlaka sawa utakuwa na mkanganyiko mkubwa bila ya kuwa na serikali ya Tanganyika.
 
Acha tuendelee kuwahadaa kwa kuwapa vyeo huku bara ili tuendelee kuwakalia wasiwe na utambulisho nje hasa nchi za mashariki ya kati.

una uhakika waznz hawatambuliki nje ya mipaka ya JMT?
 
Back
Top Bottom