Muungano wetu: Mgao wa Fedha za IMF na Zanzibar kupewa asilimia 18, ni sahihi?

Weka hapa huo mkataba wa Muungano.Pili unaelewa maana ya kero za Muungano? Na je mkataba ni biblia au msahafu?

Mwisho Zanzibar sio Mkoa ni Nchi na pia ni sehemu ya JMT kwa hiyo ina haki zote na tena haki zaidi ya Mkoa.
Haki zipi sasa? Mtaalamu amesema 21% na 30% sio halali yenu, nyie ni 4.5%, je ni kweli?
(230/1300)×100 = ???
 
Wazanzibari waliokuwa Tanganyika wameanza kurudi makwao,mizunguko yahela ipo safi, watumishi wa umma huko Zanzibar wanaishi maisha ya peponi huku tanganyika maisha ni magumu mno,mfumuko wa bei chakula,vifaa vya ujenz n.k ni juu.Zanzibar hawalimi lakin maisha kwa sasa ni murua.Acha tupigwe wajinga wengi mno.
 
Zanzibar sio Mkoa ni Nchi na pia ni sehemu ya JMT kwa hiyo ina haki zote na tena haki zaidi ya Mkoa.
Hakuna aliyesema Znz haina haki, ila kuhusu mikopo na misaada kutoka nje haki ya Znz ni 4,5%.
Huwezi kuwapa 30% watu 1m na 70% watu 60m. Huo ni wizi na unyang'anyi jamani.
 
Iwe pasi kwa pasu, si mna upenda muunga o??
 
Mambo mengine yaacheni kama yalivyo...
 
Hakuna aliyesema Znz haina haki, ila kuhusu mikopo na misaada kutoka nje haki ya Znz ni 4,5%.
Huwezi kuwapa 30% watu 1m na 70% watu 60m. Huo ni wizi na unyang'anyi jamani.
Hakika, kinachofanyika sasa ni kutafuta hasira za Watanganyika, na huenda inafanywa makusudi.
 
Kwani Tanganyika iko wapi? Mbona siioni kwenye Atlas, siioni kwenye ramani ya dunia, siioni Google Maps. Iko wapi hiyo Tanganyika inayozungumziwa kila siku humu ndani?
 
Kwani Tanganyika iko wapi? Mbona siioni kwenye Atlas, siioni kwenye ramani ya dunia, siioni Google Maps. Iko wapi hiyo Tanganyika inayozungumziwa kila siku humu ndani?
Tanganyika ndiyo Tanzania. Na hilo limekuwa sababu mojawapo ya malalamiko ya Wazanzibari kuwa Tanganyika imevaa koti la Muungano.

Kiuhalisia, Tanganyika ndiyo Tanzania lakini ndani ya hiyo inayoitwa Tanzania, imetoa sehemu ya mamlaka yake kwa Zanzibar, na yenyewe kuendelea kusimamia yale ya Tanganyika.

Kwa ujumla, hata kwa logic ndogo kabisa, huu Mwungano ni utata mtupu. Hata tukichelewesha vipi, kuna siku ama utavunjika au utaboreshwa ili kuleta mantiki.
 
Kumbukeni hili limepata baraka za mkuu wa awamu ya 6 kwa ushirikiano na yule wa zenji
Ndugai kuna kitu alitaka kufikishia umma kuhusu mgawanyo uliopita wa fedha za covd lkn 'akapotea njia'
Wakipata nafasi ya kuongea akina ndugai, polepole na wengine hali itakuwa mbaya sana
 
usilolijua ni bora uulize masoko yote hayo ni PPP ambapo wawekezaji binafsi wanafanya. Miradi ya bandari Mamngapwani na Malindi pia inajengwa kwa PPP na Mamlaka ya Uwekezaji ya Oman. Mradi wa Darajani ni uwekezaji wa Kampuni ya AFRICAB ya wazawa. Ni kweli kwa sasa Zanzibar kuna miradi mingi ipo katika Planning Stage lakini asilimia kubwa ni ya uwekezaji binafsi wa ndani na nje ya nchi. Miradi hiyo mchango wa Serikali ni mdogo sana
 
Hili swala ndio lililomtoa Ndugai kwenye Uspika...CCM mlifurahi sana kubaki na bunge la ndio Mzee ona sasa maumivu tunayaonja wote.
 
Ramani gani hiyo inaonyesha Tanganyika ndiyo Tanzania? Au ni wapi Tanganyika inatambulika kama Tanzania? Tanganyika siioni kwenye ramani popote pale.
 
Ni bora tutengane tu,kwenye masuala ya ulinzi kama itakuwa lazima basi ndio tuwe na makubaliano!
50/50 wakati mdanganyika hawezi kumiliki ardhi Zanzibar na mzanzibar anaweza kumiliki ardhi Bara!
Kichekesho nyinyi watu wa maajabu sana. kitu usichokijuwa ni bora kufanya uchunguzi ili kuwa na uhakika na unachokisema. Mmeimbishwa uongo na nyinyi mmekuwa mkiurudia mpaka mnauamini kuwa ni ukweli. Zanzibar ardhi yote ni ya Serikali. Mzanzibari anapatiwa hati ya matumizi ya ardhi ya kulima, kujenga na shughuli za uzalishaji wa kawaida. Uwekezaji mkubwa inabidi aombe kukodishwa ardhi ambayo atalipa kodi kila mwaka Serikalini. Hivyo hivyo kwa mgeni anaekuja kuwekeza nakodishwa ardhi kwa malipo kwa muda aliokubaliwa kwa kujibu wa sheria zilizopo. Halafu mnajiwa kuwa Mtanzania yoyete anaweza kuwa Mzanzibar akiamua kufanya hivyo? anachotakiwa aishi Zanzibar miaka 5 na kuomba ndio maana Mhe. Ali Hassan Mwinyi amekuwa Mzanizbari na Rais wa Zanzibar. Kwa hiyo kama hoja ni ardhi nenda kaishi Zanzibar ili upate hiyo ardhi inayokutoa roho.
 
Hivi vitu ndio vilishababisha Ndugai kulazimishwa kujiuzulu Kwa lazima. Ndugai alipojaribu kuhoji ishu za mikopo alionekana ni msaliti. Alionekana msaliti namba moja kwenye chama
 
Weka hapa huo mkataba wa Muungano.Pili unaelewa maana ya kero za Muungano? Na je mkataba ni biblia au msahafu?

Mwisho Zanzibar sio Mkoa ni Nchi na pia ni sehemu ya JMT kwa hiyo ina haki zote na tena haki zaidi ya Mkoa.
Pamoja na haki zote hata ingekuepo ni nchi huru haingeweza kupewa hela nyingi kiasi hicho kwasababu pesa hutolewa kulingana na GDP ya mkoa husika. Kwahiyo Znz isingeweza kupewa kiasi chote hicho cha pesa kwasababu haina uwezo wa kuzilipa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…