Muwekezaji kutoka Tanzania bara apigwa stop kuanzia January

Muwekezaji kutoka Tanzania bara apigwa stop kuanzia January

Nyinyi watanganyika hemu acheni tabia zenu za kibishi bishi mnavokuja kuweleza huku visiwani. Zanzibar tuna ustaarabu wetu kwaio mkija huku muwe mnakuja na adabu zenu

Mbona nyie hamna adabu mnavyokuja huku,naona sasa vigenge vya shisha vimeanza kushika kasi baada ya mwamba kuondoka ndio ustaarab huo
 
Nyinyi watanganyika hemu acheni tabia zenu za kibishi bishi mnavokuja kuweleza huku visiwani. Zanzibar tuna ustaarabu wetu kwaio mkija huku muwe mnakuja na adabu zenu
Tatizo siyo uzanzibar, tatizo ni udini.Hiyo shule inaonyesha ina misingi ya kikristo lkn inaonyesha wazazi wanaopeleka watoto wao ndy hawataki kufuata misingi na katiba ya hiyo shule

Tatizo kubwa la waislamu ni kutaja kulazimisha mambo ya dini hata sehemu ambayo wahusika wanasema hatutaki maswala ya kuleta au kupandikiza Imani Fulani hapa.

Mimi nimeshuhudia ktk shule niliyosoma wanafunzi wa kiislamu kulazimishwa kujengeaa msikiti mkubwa wakati vyumba vya kawaida vipo miaka na miaka .Na walianza kupandikiza chuki shuleni Kwa wasio waislamu.Ilifika wakati tusio waislamu tukawa tunaitwa makafiri waziwazi na wakati wa Kula hawataki kushea vyombo na wasio waislamu.Tatizo likisuluhishwa na mkuu wa mkoa na shehe wa mkoa.Ilipochunguzwa Kwa nn huo mwaka kuna matatizo ya udini shuleni wakati hayo mambo hayakuwepo wakagundua ule mwaka waliselect wanafunzi wengi wa form 5 kutokea pande za kigoma na hao form 5 ndy walioleta matatizo yote hayo

Mleta mada hii habari haijabalance,mkuu wa shule angeongea ndy tungejua ukweli kwmb pengine wazazi na watoto wao ndy wanaleta mambo ya udini kwenye shule isiyo ya kiislamu
 
Nchi inaongozwa na sheria sio mihenko ya kuogopa kuchafuliwa
Mihemuko ipi kulaziy shule ya Kikristo ichukue waislamu na ifundishe Dini ya kiislamu na kiarabu kwa lazima na irihusu waswali swala Tano? Si waende shule za kiislamu mbona ziko kibao Zanzibar huo ni upnezi wa minority wakristo walioko Zanzibar Wa waziwazi kabisa

Hizo ni chokochoko za kidini waaambieni wazazi wanaotaka watoto wao wasome kiislamu na kiarabu na wapige swala Tano waende shule zao za kiislamu.Hawalazimishwi kupeleka hapo
 
Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, imeifutia usajili Skuli ya Eden inayomilikiwa na Shirika la Afrika Agape Association kuanzia Januri 3 mwakani.

Hatua hiyo imefikiwa baada ya Wizara kubaini mmiliki wa Skuli hiyo kuendesha Skuli kinyume na sheria, miongozo na kanuni za Wizara.

Akizungumza na wamiliki wa Skuli hiyo huko Shakani Kaimu Mrajis wa Elimu na Katibu wa Baraza la Elimu Zuwena Mataka Hafidh, amesema kumekuwepo malalamiko mbalimbali yaliyowasilishwa na wazazi hali iliyopelekea Wizara kuchukua maamuzi hayo.

Ameyataja baadhi ya malalamiko hayo ni pamoja na Wanafunzi wa kislam kutosomeshwa somo la dini ya kislaam na kiarabu, kulazimishwa kujifunza dini ya kikiristo, kutotakiwa kufunga katika mwezi mtukufu wa Ramadhan na Wanafunzi kutoruhusiwa kuvaa hijabu.

Malalamiko mengine amesema kupandishwa ada bila ya utaratibu, kutokuwa na mashirikiano mazuri baina ya wazazi, walimu na mmiliki wa skuli na mmiliki huyo kuendesha skuli kwa hisia zake binafsi.

Aidha amebainisha kuwa malengo ya Wizara sio kuifutia leseni Skuli hiyo bali ni kuhakikisha inafuata sheria na miongozo ya Serikali katika kuendesha Skuli yao.

Kaimu Zuwena, amebainisha kuwa mmiliki wa Skuli hiyo amekuwa mgumu kufuata sheria na miongozo ya Wizara na kuendesha Skuli yake anavyotaka yeye jambo ambalo halivumiliki.

“Haiwezekani Skuli kuendeshwa bila ya kufuata miongozo ya Wizara kwani tuna skuli 590 hatutakuwa tayari kuona mmiliki yoyote wa skuli binafsi anakwenda kinyume na utaratibu na hatutasita kuchukua hatua,” amesisitiza.

Hata hivyo, amesema Skuli hiyo imekuwa ikifatiliwa mara kwa mara na kupewa maagizo ya kurekebisha kasoro hizo lakini haizingatii maagizo anayopewa na badala yake kuendelea kuendesha skuli kinyume na sheria.

Amesisitiza kuwa skuli yoyote ya binafsi inatakiwa kufuata sheria, miongozo na mambo mbalimbali yanayotolewa na wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar .

Nae Afisa Elimu Taaluma Mkoa wa Mjini Magharibi, Amosi John Henock, amesema toka skuli hiyo kusajiliwa mwaka 2010 imekuwa ikijitokeza migogoro baina ya mmiliki na jamii pamoja na kushindwa kujirekebisha baadhi ya kasoro ambazo alitakiwa kuzifanyia kazi.

Aidha amesema Skuli hiyo imeshawahi kufungiwa na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Ayoub Mohammed Mahmoud na kutakiwa kurekebisha kasoro zilizoonekana lakini aliendelea kukaidi.

Amesisitiza kuwa Skuli hiyo haitaendelea kufundisha mpaka pale itakapokubali kwenda sambamba na maagizo ya Serikali katika kuwapatia watoto elimu.

Amesema hata katiba ya Zanzibar imeeleza wazi kwamba mtu yoyote hapaswi kufanya jambo lolote kwa lengo la ubaguzi wa moja kwa moja ama kwa taathira yake.

Kwa upande wake Sheha wa Shehia ya Shakani bi Mwanaisha Khamis Rashid amebainisha kuwa mara nyingi amekuwa akikaa na uongozi wa Skuli hiyo katika uendeshaji elimu kwa kufuata miongozo na mitaala ya Wizara lakini hakuifuata.

Nae mmiliki wa skuli hiyo bwana Youung Am Kim ameahidi kuheshimu maamuzi ya Wizara ya Elimu ya kutofungua Skuli na hiyo na kuwajuillisha wazazi juu ya suala hilo.

Aidha amesema atahakikisha anafuata sheria ya elimu ya Zanzibar na kuondoa changamoto ambazo zinalalamikiwa kupitia Skuli yake.

Akizungumza kwa niaba ya walimu wenzake Mwalimu Ummy Aga amesema wameweka jitihada binafsi kwa wanafunzi wao kuona wanafanya vizuri katika mitihani yao na kujipima katika ufundishaji lakini kufutwa kwa Skuli hiyo imeondosha ndoto yao kwa Wanafunzi wao.
Takbiiir
 
Kinachosumbua hapo ni udini

Sekta ya elimu inatakiwa kuwa huru mfano Tanzania bara ni hiari ya shule kufundisha masomo ya Dini au kuyaacha kabisa

Za private ziko Muslim schools na Christian schools

Mtu alienda Muslim schools anakutana na ya kiislamu kibao kuanzia kuvaa hizo hijabu nk akienda Christian schools atasali kikristo nk Na wazazi huridhika

Zanzibar kinafanyika kwenye hivyo ni kutaka kulazimisha mwenye ageuze shule kwa lazima iwe Muslim school

Zanzibar mbona Muslim schools ziko kibao wazazi wapeleke watoto wao huko huo ni ukorofi usio na sababu mtu kafungua Christian school yake kwa Nini umkomalie kuwa laziy iwe Muslim school

Hii ichukuliwe kama kero ya muungano.Ichukuliwe wazi kabisa kuwa huyo mwenye shule ananyanyaswa kidini

Raisi Mwinyi aingilie kati Hilo swala haraka
Tatizo tunashindwa kuelewa Zanzibar ni nchi na INA sheria zake japokuwa ipo katika muungano na Tanganyika, hivyo sheria zake muda mwingine zinawezakuwa tofauti na za Tanganyika kikubwa kutambua na kuheshim kwa maana nchi bila sheria ni jalala.
 
Hakuna mahali popote baraza la mitihani la taifa husema lazima mwanafunzi asome masomo ya kiislamu ,kiarabu au kifaransa au kihindi hayo huwa ya hiari ya shule

Sasa Kwa Nini Zanzibar walazimishe tena kwenye shule ya Private

Huyo mkorea kaanzisha shule Kwa ajili ya minority wakristo waislamu wanazo zao Kila Kona Kwa Nini waikomalie hiyo ? Ni unyanyasaji wa kidini .Shule inanyanyaswa sababu ya Kikristo
 
Mihemuko ipi kulaziy shule ya Kikristo ichukue waislamu na ifundishe Dini ya kiislamu na kiarabu kwa lazima na irihusu waswali swala Tano? Si waende shule za kiislamu mbona ziko kibao Zanzibar huo ni upnezi wa minority wakristo walioko Zanzibar Wa waziwazi kabisa

Hizo ni chokochoko za kidini waaambieni wazazi wanaotaka watoto wao wasome kiislamu na kiarabu na wapige swala Tano waende shule zao za kiislamu.Hawalazimishwi kupeleka hapo
Serikali ya Jamuhuri ya muungano wa Tanzania imejitambulisha haina dini, ila msingi wa serikali ya mapinduzi Zanzibar unaviashiria kuwa una dini nayo ni uislamu hivyo ni kukubaliana na hali ukiwa ktk ardhi yao. When you are in Rome do what Romans do!
 
Hakuna mahalo popote baraza la mitihani la taifa husema lazima mwanafunzi asome masomo ya kiislamu ,kiarabu au kifaransa au kihindi hayo huwa ya hiari ya shule

Sasa Kwa Nini Zanzibar walazimishe tena kwenye shule ya Private

Huyo mkorea kaanzisha shule Kwa ajili ya minority wakristo waislamu wanazo zao Kila Kona Kwa Nini waikomalie hiyo ? Ni unyanyasaji wa kidini .Shule inanyanyaswa sababu ya Kikristo
Zanzibar ni nchi mkuu na kumbuka ina sheria zake tofauti na Tanganyika. Ndiyo maana hata msingi hadi mwaka huu walikuwa wanasoma miaka 6 badala ya 7.
 
Hakuna mahali popote baraza la mitihani la taifa husema lazima mwanafunzi asome masomo ya kiislamu ,kiarabu au kifaransa au kihindi hayo huwa ya hiari ya shule

Sasa Kwa Nini Zanzibar walazimishe tena kwenye shule ya Private

Huyo mkorea kaanzisha shule Kwa ajili ya minority wakristo waislamu wanazo zao Kila Kona Kwa Nini waikomalie hiyo ? Ni unyanyasaji wa kidini .Shule inanyanyaswa sababu ya Kikristo
Nchi ya Zanzibar haiendeshwi na baraza LA mitihani Tanzania, bali inasheria na taratibu zake kulingana na katiba ya Zanzibar mkuu.
 
Zanzibar ni nchi mkuu na kumbuka ina sheria zake tofauti na Tanganyika. Ndiyo maana hata msingi hadi mwaka huu walikuwa wanasoma miaka 6 badala ya 7.
Miaka sio issue hata Tanzania bara wako watoto kibao wakifika la sita mzazi anampeleka private form one bila shida

Kinachogomba hapo ni Serikali kulazimisha Christian school ibadilishwe kuwa Muslim school .Hapo ndipo tatizo lilipo kwenye huo mgogoro
 
Back
Top Bottom