Muziki kutoka nchini Zaire (sasa ni D.R.C) uliwezaje kutamalaki na kupendwa sana hapa Tanzania ilhali tumepakana na jirani wengine takribani 6?

Muziki kutoka nchini Zaire (sasa ni D.R.C) uliwezaje kutamalaki na kupendwa sana hapa Tanzania ilhali tumepakana na jirani wengine takribani 6?

Nafikiri ukiachilia umahiri wa kuimba kwa sauti nzuri zilizopangiliwa, upigaji na utumiaji wa vyombo vya muziki na hata kucheza, kilichofanya nyimbo zao kuenea duniani ni jinsi walivyoendelea katika kuzirekodi, kuzidurufu, na usambazaji wake. Pengine waligundua mapema studio za kurekodi na hatimaye kuzalisha kwa wingi iwe ni kaseti au sahani za muziki wao na kuzisambaza mpaka huku kwetu. Na zaidi wakaanza kufanya ziara kwa wapenzi wa muziki wao.
Kwenye hili la kufanya ziara unanikumbusha kuna duka la kuuza kaseti za nyimbo za Kongo lilikuwa linaitwa Bukavu Music Center pale Kurasini huku Dar wanamuziki wengi wa Kongo waliokuwa wanakuja kufanya show walikuwa hawawezi kuondoka pasipo kwenda kujuliana hali na yule jamaa mmiliki.
 
Congo wenyewe kwanza walipenda utamaduni wao, nadhani pia ilichangiwa na mobutu alipopiga marufuku mambo yote ya kigeni, mpaka ukizaa mtoto shuleni ni lazima umwandikishe kwa jina la asili, hii ilichangia wacongo kupenda mziki wao na kuuboresha zaidi kupata soko nje ya nchi, sisi huku nchi nyingine hatukuthamini muziki wetu!
 
Congo wenyewe kwanza walipenda utamaduni wao, nadhani pia ilichangiwa na mobutu alipopiga marufuku mambo yote ya kigeni, mpaka ukizaa mtoto shuleni ni lazima umwandikishe kwa jina la asili,
Hii ya majina ya asili hata mimi ninaipenda sana kwa maana utakuta shuleni ukiita "Fatuma Bakari" wanakuja hao watoto hata kumi lakini laiti kama tungekuwa na huu utaratibu wa majina ya asili ninadhani hii shida isingekuwepo kabisa mkuu...
 
Nyimbo zake kadhaa ninazipenda sana aisee. Aliwahi kukosana na dikteta Mobutu
Mário,pesa position,mamuu,bina na ngai,kimpa kimsangameni,Fabrice ,muya, bureau de coers, attention na sida,candidate de mobutu,Helene,colonel bangala,fc 105 du Gabon,matata ya mwasi, cooperation odongo,1200 letters,lisolo ya Nzambe na Adamo,liberte, republique du Zaire,azda,muongo na mulozi,
 
Habari za wakati huu kaka na dada zangu wote wa humu jamiiforums.

Ndugu zangu watanzania;

Muziki kutoka nchini Zaire (sasa ni D.R.C) uliwezaje kutamalaki na kupendwa sana hapa Tanzania ilhali tumepakana na jirani wengine takribani 6?

View attachment 1644761

Mbali na D.R.C nchi yetu ya Tanzania pia imepakana na jirani zake kama vile Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Zambia, Malawi na Msumbiji.

Ninakumbuka enzi zile nipo mtoto baba yabgu alikuwa anawapenda sana wanamuziki kama akina M'bilia Bel, Madilu Système, Sam Mangwana, Pepe Kalle and Empire Bakuba, Diblo Dibala, Bozi Boziana pamoja na Awilo Longomba.

Kwanini ni muziki wa Zaire tu na sio hizo nchi zingine zilizopakana na Tanzania?

View attachment 1646545

USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
Miaka ya 50 na 60 muziki uliopendwa sana ulikuwa wa Kongo na Kenya, Tanzania tulikuwa watu wa kukopi tu kila wimbo mpya unapotoka.
 
Wakongo ni watu wa starehe sana kwa hulka yao. Kutokana na hali hiyo wakawa wabunifu sana katika utunzi wa nyimbo za muziki na uimbaji. Lakini Siasa kali za Mobutu (udikteta) uliwafanya wakongo watafute njia za kujiliwaza kwa kukimbilia kwenye muziki na hivyo mziki wao ukapanda sana chati. Lakini lingine ni ukubwa wa nchi ile. Ukubwa huo wenye makabila zaidi ya elfu moja na watu wenye vipaji mbalimbali vitakuwa vilichangia sana ukuaji wa muziki katika taifa hilo.
 
Back
Top Bottom