Mvua kubwa Dar usiku huu kuamkia 20 Jan 2024. Je maeneo yenu kuna maafa?

Msanii

Platinum Member
Joined
Jul 4, 2007
Posts
25,252
Reaction score
36,513
Wananzengo,
usiku saa 9 nimejikuta navamiwa na wanangu chumbani, wanaogopa radi kabambe zinazopiga sambaba na mvua hii kubwa yenye upepo wa kuhamisha milima.

Soon kunakucha.

Tujuzane endapo kuna maafa maeneo yenu. Lengo ni kupashana taarifa. Tupia picha .

Nawalinda wanangu hapa wasipigwe na ngurumo ya radi.πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€..... yaani kha! Wanaogopa sana lile libombastic sound baada ya radi kumulika.

Tanesco aibu sana kwa haya mnayotufanyia.

============



 
Mvua ni kubwa sana wanaokaa sehem za mabondeni sijui wakoje mwenyezmungu awanusuru nimepita toangoma nyuma ya kituo cha mafuta oilcom sasa hv mitaa ya kule kama bwawa maji yamejaa sana sijui. Wakaz wake wakoje
 

Jumamosi hii wanaoenda kazini wanalaani hatari, ila ambao hawaendi kazini ni kulala hadi njaa iume kisawasawa ndo waamke kupika.

Hongereni kwa hali ya hewa nzuri, pole kwa wanaoishi maeneo ya chini ya usawa wa bahari maana mafuriko hayatawaacha salama.

Huwa sielewi kwanini Tanesco hawapatani na mvua, ikinyesha tuu umeme usipokatika basi hilo eneo limebahatika.

Poleni kwa yote, ndo maisha.
 
Msanii kwenye ubora wake!
mvua tushaizoea mkuu kawaida sana, hao watoto wako wanaoogopa hizi radi Mtoto za Dar? wapeleke Tabora, Kigoma, Rukwa huko wapambane na Baba zao Radi inachapa mpaka unadham ni Bomu la Nyuklia.


Umetaja Tabora...

Nimepakumbuka kwetu....

Wacha nifanye mchakato niende kusabahi nyumbani.

TRL weeaa aaayuuu..!
 
Msanii kwenye ubora wake!
mvua tushaizoea mkuu kawaida sana, hao watoto wako wanaoogopa hizi radi Mtoto za Dar? wapeleke Tabora, Kigoma, Rukwa huko wapambane na Baba zao Radi inachapa mpaka unadham ni Bomu la Nyuklia.
Mikoani Radi zinapiga za nguvu sana kupita huko mjini.
Naiogopa sana Radi maana kukuondoa ni dk.0 tu
Huko zinawasaidia EarthWire nadhani.
Huku vijijini ni chache sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…