Mvua kubwa Pwani na Dar; Tujuzane hali ilivyo maeneo yetu ili tuwe na taarifa za TAHADHARI

Mvua kubwa Pwani na Dar; Tujuzane hali ilivyo maeneo yetu ili tuwe na taarifa za TAHADHARI

Niliambiwa na wenyeji zile radi ni Jambo la kawaida. Na sijaona bado.
Nikasema hapa acha niondoke tuu.
Niliondoka Kesho yake.

Wewe chuma imeshukia kwenye nguzo ya umeme. Nguzo imechanwa kama vile kijiti
Acha kuogopa Kifo Mzee hutaki kwenda kuonana na Mungu live
 
Ukitaka kujua radi si kitu cha kuleta utani nacho, Nenda Rukwa, Ruvuma, Kigoma na Kanda ya Ziwa.

Radi za hii mikoa, zinaweza kuondoa uhai wako within a second!

Radi si kitu cha mchezo.

Kuna radi moja ilipiga wanafunzi wa Businda Secondary, Kule Bukombe Geita. Ikaua wanafunzi Saba na kujeruhi wengine. ilipiga darasa wakiwa kwenye vipindi.View attachment 3557743

Mimi binafsi nilisoma Bukoba kanda ya ziwa, Hizi radi nilizi experience kabisa. Yani radi ikipiga unaona kabisa ule mstari⚡️unajichora na kushuka ardhini kabisa.

Kuna siku tupo darasani, uliwaka mwanga mkali, sasa kwa vile radi ni kama umeme, husafiri kwenye vitu vya chuma, kiti nilichokuwa nimekalia kilikuwa na chuma, nilisikia kabisa shoti, mwilini.

Radi ikipiga sehemu, kitu chochote chenye asili ya chuma, kinapokea ule umeme wa radi.

Kuna mwanafunzi mmoja wa shule ya msingi, hiyo shule ipo jirani na sekondari yetu, sasa huyo mwanafunzi ni binti mdogo tu, alikuwa anaenda kumpelekea mwalimu mwamvuli. Mvua ilikuwa inapiga kwelikweli na radi zinawaka.

Sasa ile ametoka darasani na mwamvuli wake anampelekea mwalimu ambaye alikuwa nje ya darasa hilo, kwenye gari lake, ili waweze kurudi wote darasani na mwamvuli huo.

Aisee! ile anatembea kumuendea mwalimu alipo, iliwaka radi, ikapiga kile kichuma cha juu ya mwamvuli ☂️. Ikammaliza yule mwanafunzi palepale. Yule mwanafunzi alikuwa mweusi tii! Akafa palepale.
Kilicho mwokoa yule mwalimu, yeye alikuwa ndani ya gari.

Radi sio poa, ni zaidi ya umeme.

Binafsi ni muoga sana wa radi.
Popote mlipo mauti yatakufikeni tu! Hata mkiwa kwenye ngome madhubut kiasi gani!

Hayo ni maneno ya M/Mungu.....

Mkuu ushasema Radi ilipiga hadi darasani ikaua wanafunzi,nakumbuka Iko kisa mkuu! (R.i.p wanetu).

Sasa kama ni ivyo Radi inaweza ikakuchapa hata ukiwa geto kwako unakula ugali dagaa mchele! Maana haijalishi upo nje au la! Huko kanda ya ziwa kwa Radi ni balaa,Kwa sisi wa hii mikoa mingine haitishi sana.
 
Dar Kila kitu wanalalamika.

Wiki iliyoisha nilikuwa Kahama. Dadeki! Kuna mvua zinapiga bhana! Kwanza radi inapiga hadi Baba mwenye nyumba unasema Leo kazi IPO.

Mstari mwekundu unajichora unatembea alafu unakuja kutua karibu na nyumba yenu mpaka cheche. Sikilizia mlio wake. *****. Kama unapresha unaweza kufa.

Ogopa radi inapiga mpaka umeme unajizima. Nilikimbia
Kule Bukoba, ilikuwa ikipiga radi hadi Transfoma za umeme, zinazima.

Radi za kanda ya ziwa ni balaa.
 
Mvua ikija lawama
Joto likiwepo lawama

Ova
 
Hivi wale kondoo waliokuwa wanapigana na radi siku hizi hawapo?
 
Watu wa Dar, mvua kidogo tu wasiwasi kibao...

Sisi wa mkoa kuna wakati hatulioni jua wiki nzima, bogi linapiga mdogo mdogo...
 
Back
Top Bottom