Mvua kubwa Pwani na Dar; Tujuzane hali ilivyo maeneo yetu ili tuwe na taarifa za TAHADHARI

Mvua kubwa Pwani na Dar; Tujuzane hali ilivyo maeneo yetu ili tuwe na taarifa za TAHADHARI

Radi sio mchezo , nakumbuka tulikua shambani moro , ilipiga ikakausha watu watatu mbele ya macho yangu 😪
Shambani na kwenye misitu kufikiwa na radi ni fumba na kufumbua, ila hao wana nchi wa Dar makazi yao na maeneo mengi ya mifumo ya kukabiliana na radi, ila waoga wengine ikipiga radi wanajificha nyuma ya kabati 😅
 
Nina mwaka wa 4 nipo Mpwapwa, Dodoma.

Sijawahi kuona mvua kama hizi!
Mvua hizi ndizo zimefanya ibaki kidogo tuta la reli ya SGR kwenda na maji na kufanya treni kusimama siku tatu.
Mwaka huu mazao yamekubali.
Mwaka huu kulikuwa hakuna lile Jua la mwezi wa pili.
Miaka yote mvua hunyesha mwezi January tu then mwezi wa pili husimama kisha mwezi March rasha rasha na hapo ndo mwisho wake!

Jana ilianza saa 1 usiku hadi 5.
ndio mara yangu ya kwanza kuona Radi na Ngurumo ndani ya miaka hii minne.
Wape Hi...Watu Wa Ilolo,,,Hazina,,,Mji Mpya,,Ving'awe,,Kikombo,,,Igovu,,,Vianze,,,Mjitu,,Masasteba Dispensary,,,Paris Pub,,Manase Pub,,,Bambuu Pub,,,Gymkhana Pub n.k,,n.k.....
 
Sa we nae dume zima linaogopa Radi! We wakati umelala unaogopa radi na mvua, wengine ndio inawenyeshea katika kupambania maisha na mengineyo!
Mambo mengine yasifanyike kisa mvua na radi? Kuna daktari saizi ndio anaingia zamu,au askari,au wafanyakazi wa sekta nyingine! Sasa hao wote wasitoke kisa Radi na mvua?
Ukitaka kujua radi si kitu cha kuleta utani nacho, Nenda Rukwa, Ruvuma, Kigoma na Kanda ya Ziwa.

Radi za hii mikoa, zinaweza kuondoa uhai wako within a second!

Radi si kitu cha mchezo.

Kuna radi moja ilipiga wanafunzi wa Businda Secondary, Kule Bukombe Geita. Ikaua wanafunzi Saba na kujeruhi wengine. ilipiga darasa wakiwa kwenye vipindi.
FB_IMG_1773467498896.jpg


Mimi binafsi nilisoma Bukoba kanda ya ziwa, Hizi radi nilizi experience kabisa. Yani radi ikipiga unaona kabisa ule mstari⚡️unajichora na kushuka ardhini kabisa.

Kuna siku tupo darasani, uliwaka mwanga mkali, sasa kwa vile radi ni kama umeme, husafiri kwenye vitu vya chuma, kiti nilichokuwa nimekalia kilikuwa na chuma, nilisikia kabisa shoti, mwilini.

Radi ikipiga sehemu, kitu chochote chenye asili ya chuma, kinapokea ule umeme wa radi.

Kuna mwanafunzi mmoja wa shule ya msingi, hiyo shule ipo jirani na sekondari yetu, sasa huyo mwanafunzi ni binti mdogo tu, alikuwa anaenda kumpelekea mwalimu mwamvuli. Mvua ilikuwa inapiga kwelikweli na radi zinawaka.

Sasa ile ametoka darasani na mwamvuli wake anampelekea mwalimu ambaye alikuwa nje ya darasa hilo, kwenye gari lake, ili waweze kurudi wote darasani na mwamvuli huo.

Aisee! ile anatembea kumuendea mwalimu alipo, iliwaka radi, ikapiga kile kichuma cha juu ya mwamvuli ☂️. Ikammaliza yule mwanafunzi palepale. Yule mwanafunzi alikuwa mweusi tii! Akafa palepale.
Kilicho mwokoa yule mwalimu, yeye alikuwa ndani ya gari.

Radi sio poa, ni zaidi ya umeme.

Binafsi ni muoga sana wa radi.
 
RC wenu anasema mniuzie gari namba A msisababishe foleni.
 
Ndugu zangu mliopo Pwani naamini mpo salama.

Chukueni tahadhari na Mungu awalinde

Hapo ulipo mvua ipo kias gani?

Hapa nilipo inanyesha sana na radi kali mpaka usingizi umekata
Yani ninavyopenda mvua na radi, nawashangaa mnavyopeana pole 😁😁
Labda kama huko mlipo mvua zinaleta mafuriko na radi zinaua watu ila binafsi mvua ikinyesha kwangu ni shangwe
 
Ukitaka kujua radi si kitu cha kuleta utani nacho, Nenda Rukwa, Ruvuma, Kigoma na Kanda ya Ziwa.

Radi za hii mikoa, zinaweza kuondoa uhai wako within a second!

Radi si kitu cha mchezo.

Kuna radi moja ilipiga wanafunzi wa Businda Secondary, Kule Bukombe Geita. Ikaua wanafunzi Saba na kujeruhi wengine. ilipiga darasa wakiwa kwenye vipindi.View attachment 3557743

Mimi binafsi nilisoma Bukoba kanda ya ziwa, Hizi radi nilizi experience kabisa. Yani radi ikipiga unaona kabisa ule mstari⚡️unajichora na kushuka ardhini kabisa.

Kuna siku tupo darasani, uliwaka mwanga mkali, sasa kwa vile radi ni kama umeme, husafiri kwenye vitu vya chuma, kiti nilichokuwa nimekalia kilikuwa na chuma, nilisikia kabisa shoti, mwilini.

Radi ikipiga sehemu, kitu chochote chenye asili ya chuma, kinapokea ule umeme wa radi.

Kuna mwanafunzi mmoja wa shule ya msingi, hiyo shule ipo jirani na sekondari yetu, sasa huyo mwanafunzi ni binti mdogo tu, alikuwa anaenda kumpelekea mwalimu mwamvuli. Mvua ilikuwa inapiga kwelikweli na radi zinawaka.

Sasa ile ametoka darasani na mwamvuli wake anampelekea mwalimu ambaye alikuwa nje ya darasa hilo, kwenye gari lake, ili waweze kurudi wote darasani na mwamvuli huo.

Aisee! ile anatembea kumuendea mwalimu alipo, iliwaka radi, ikapiga kile kichuma cha juu ya mwamvuli ☂️. Ikammaliza yule mwanafunzi palepale. Yule mwanafunzi alikuwa mweusi tii! Akafa palepale.
Kilicho mwokoa yule mwalimu, yeye alikuwa ndani ya gari.

Radi sio poa, ni zaidi ya umeme.

Binafsi ni muoga sana wa radi.
Hayo maeneo yanakumbwaga sana na radi zinazoua
Najaribu kufikiri tatizo huwa ni nini?
Je ni hamna majengo marefu yanayoweza kuipokea hiyo radi au miti?

Hata wanyama kanda hizo wanauawa sana na radi
 
Nimegundua kama mvua imenyesha asubuh nilivyoamka baada ya kuchungulia dirishani
 
Back
Top Bottom