Mvutano: Ni kwanini Mungu alimruhusu mwanaume kuweza kuwa na mke zaidi ya moja kwenye biblia lakini makanisa yamekataza?

Acha mbwebwe dogo. Hapo anasema ikiwa umemuacha mkeo na ukaoa mwanamke mwingine, unatakiwa umuhudumie yule wa kwanza. Hajasema opening wake wengi. Acha kupotosha we maamuma.
Hapo kuna neno kuwa ukimuacha mkeo au unajitungia tu, yaani umuache mkeo halafu umuoe mwingine kisha huyu wa mwanzo uendelee kumtunza ikiwemo haki yake ya ndoa, we ndoo fala kabisa huelewi.
 
Mwanamke awe na waume wangapi?

Sent from my moto g 5G (2022) using JamiiForums mobile app
 
Mkuu mshamba,
Hata mimi huwa biblia naona unaji-contradict sana.

ILA kuhusu mstari kuwa na Mke mmoja upo labda ujasoma vzuri tu.
 
Agano jipya wachungaji ndio waliagizwa kuoa mke mmoja TU.
Kwa wengine maandiko hayajaweka wazi.
 

Je Biblia Inaruhusu Mwanamume Awe na Wake Wengi?​


Jibu la Biblia​

Kwa muda fulani, Mungu aliruhusu mwanamume awe na wake wengi. (Mwanzo 4:19; 16:1-4; 29:18–29) Lakini Mungu hakuanzisha mpango wa mwanamume kuwa na wake wengi. Alimpa Adamu mke mmoja tu.
Mungu alimwagiza Yesu Kristo akazie mpango aliokuwa ameanzisha awali wa mwanamume kuwa na mke mmoja. (Yohana 8:28) Yesu alipoulizwa kuhusu ndoa, alisema hivi: “Yeye aliyewaumba hao kutoka mwanzo aliwafanya mwanamume na mwanamke na kusema, ‘Kwa sababu hiyo mwanamume atamwacha baba yake na mama yake naye atashikamana na mke wake, na hao wawili watakuwa mwili mmoja.”—Mathayo 19:4, 5.
Baadaye, mmoja kati ya wanafunzi wa Yesu aliongozwa na roho ya Mungu kuandika hivi: “Kila mwanamume na awe na mke wake mwenyewe na kila mwanamke awe na mume wake mwenyewe.” (1 Wakorintho 7:2) Pia, Biblia inasema kwamba katika kutaniko la Kikristo ni lazima mwanamume aliyefunga ndoa na ambaye ana majukumu ya pekee awe “mume wa mke mmoja.”—1 Timotheo 3:2, 12.
 
Kumbukumbu la Torati 17:15-17

15 mnapaswa kumweka mfalme ambaye Yehova Mungu wenu atamchagua.+ Mnapaswa kumchagua mfalme kutoka miongoni mwa ndugu zenu. Hamruhusiwi kumweka mfalme ambaye ni mgeni, ambaye si ndugu yenu. 16 Hata hivyo, hapaswi kujipatia farasi wengi+ au kuwafanya watu warudi Misri kuchukua farasi wengi zaidi,+ kwa kuwa Yehova aliwaambia hivi: ‘Msirudi huko tena kamwe kupitia njia hii.’ 17 Wala hapaswi kuwa na wake wengi, ili moyo wake usipotoke;+
 
Ach la mke mmoja mi nashangaa na hii ya wengine kutooa au kuolewa kabisa sijui wameitoa wapi
 
Kanisa ni kampuni kama kampuni zingine mfano pepsi, tigo, Azam e.tc. hata wewe unaweza anzisha kanisa lako na tengeneza na ruhusu sheria zako.
 
Hakuna sehemu kuna kiumbe kinaitwa Mungu kimekaa kinatupa maelekezo ya namna ya kuishi ,huo ni utashi wa watu kama tamaduni na desturi za jamii husika .

Desturi ya mke mmoja haipo kwenye biblia ila wakristo walifuata utamaduni wa kizungu ,walio waletea injili, baada ya kuona wake wengi ni mfumo dume .
 

Kumbukumbu la Torati 17:15-17

15 mnapaswa kumweka mfalme ambaye Yehova Mungu wenu atamchagua.+Mnapaswa kumchagua mfalme kutoka miongoni mwa ndugu zenu. Hamruhusiwi kumweka mfalme ambaye ni mgeni, ambaye si ndugu yenu. 16 Hata hivyo, hapaswi kujipatia farasi wengi+ au kuwafanya watu warudi Misri kuchukua farasi wengi zaidi,+ kwa kuwa Yehova aliwaambia hivi: ‘Msirudi huko tena kamwe kupitia njia hii.’ 17 Wala hapaswi kuwa na wake wengi, ili moyo wake usipotoke;+

Kwenye biblia ipo.

in a way which is more logical and consistency the wholesome god, all loving he is not existed.
 
Huu ndio uzoefu wako mfalme Sulemani maana wewe ulikuwa nao 1000. Uliwezaje wewe?
Suleiman ana maajabu mengi sana, hakuta mfalme atakaye tokea kama yeye, Yan anakubakika pande zote mbili at the same time
 
Hawapaswi kuwa na wake wengi ila sio kwamba wanapaswa kuwa na mke mmoja , ukiwa na wawili au watatu bado sio wengi.
 
Unasoma bibli ipi mwenzetu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…