Mvutano wa kisheria, tuhuma ya msanii aliyechoma picha ya Rais


lkn kama mnajua kwamba watoto masikini “wanapotoshwa” kwa nini mnawakamata masikini na msikamate hao wanaowapotosha hao watoto wa masikini kama ni kweli ni watenda haki ?
 
Sasa ndugu Yesu hapo Chadema imehusikaje?
 
kitendo kile ni sawa na mtu kuokota makaratasi ili awashie mkaa kwenye jiko lake.

Hahahaa ,kama lingekuwa kosa wangefungwa watu wengi sana ,magazeti kibao yana picha ya rais na watu wanayachoma.

Msingi ni kwamba RC alisema akamatwe kwa kosa la kuchoma picha ya rais na kama siyo kosa basi aachiwe kisha akamatwe tena wamfungulie kesi nyingine labda ya kutukana ambayo ina dhamana.
 
Wizara ya Afya taarifa yake inasema kati ya watu 4 hapo ulipo Kwa idadi hiyo mmoja wenu atakuwa na tatizo la Afya ya akili
 
penal code ni kubwa sana ndugu yangu. kwa tuliokaa mahakamani mda mrefu, kosa lipo.
Ila wee unachekesha kweli, lete hivyo vifungu vya penal code hapa sisi tujionee na tuhakiki, lete uthibitisho hapaa.

Wee c umekaa mda mrefu mahakamanii? Haya lete hapa watu tujisomee hiyo sheria.

Hatutaki porojo na vijisababu vya kutunga au kuokoteza ili mfurahishe nafsi zenuu, Lol
 
Huyu chizi naye anajiita wakili
 
Lakini Kosa la Dogo ni la kimaadili zaidi kuliko kijinai.

Ni utovu wa nidhamu kuchukua picha ya mtu na kuichoma hadharani tena mtu huyo akiwa ni Rais wa Nchi.

Mtu kama humpendi na chumbani kwako kuna picha zake unachukua unazitia kiberiti kimya kimya.
 
Kwenye penal code kuna kosa linaitwa ARSON i.e kuchoma Mali moto, swali ni vitu vinavyoitwa Mali ni vipi?
Mbona mimi jana tuu nimetoka kuchoma picha kibao zikiwepo za Magufuli, Samia, Mbowe, Msigwa, Lissu, etc. Waje wanikamate
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…