Mvutano wa kisheria, tuhuma ya msanii aliyechoma picha ya Rais

Arson ni kosa la kuchoma moto mali ya mtu mwingine kwa dhamira ya kuharibu.

Hiyo picha ni ya nani?

Picha ya kuchora isiyo na ithibati ikionesha sura ya kufanana na kitu fulani itakuwaje ushahidi ambao unataka ushahidi usio na shaka?
Precedent nyingi nilizosoma zilikuwa za mazao
 
Endeleeni kuwapotosha vijana kutoka familia maskini huku wa kwenu mkiwahimiza kuwa makini na kujiepusha na siasa za kipumbavu. Huwezi kukuta mtoto wa kiongozi wa ngazi za juu CHADEMA anafanya harakati za kipumbavu au kuropoka hovyo. Watoto wa maskini kama kina Mdude ndo hutolewa kafara ili kupata political mileage. Wewe mleta uzi nina uhakika huwezi ruhusu mwanao achukue picha ya Rais na kuichoma huku akirekodi video.
Kuchoma picha ni kosa au siyo kosa!?
 
Kwamba hata yule kijana aliyekamatwa Rungwe kwa kosa la kuipiga kiberiti picha ya Rais Samia, hana kosa lolote na hata wakamataji hawajui wampachike kesi gani, maana kwa katiba ya Tanzania kitendo kile ni sawa na mtu kuokota makaratasi ili awashie mkaa kwenye jiko lake.

Inadaiwa kukamatwa kwake kumesababishwa na mihemko tu na fikra duni za viongozi wa Mbeya

=========

Ni siku tatu tangu Jeshi la Polisi mkoani Mbeya limkamate Shadrack Chaula (24), kijana anayetuhumiwa kuchoma moto picha ya Rais Samia Suluhu Hassan, suala hilo limeibua mvutano wa kisheria, ikielezwa hakuna sheria iliyovunjwa.

Akizungumza na Mwananchi jana Julai 3, 2024 kuhusu kosa la kijana huyo na lini atafikishwa mahakamani, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Benjamin Kuzaga amesema jukumu lao liliishia kumkamata suala la kupelekwa mahakamani linabaki kwa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka.

“Siwezi kusema ni lini atapelekwa mahakamani, kazi yetu ilikuwa ni kumkamata, Ofisi ya Mashtaka ndiyo itaandaa mashtaka kwa kuangalia ushahidi na kuonyesha ni vifungu gani vya sheria mtuhumiwa amekiuka,” amesema.

Suala hilo pia limeibua mjadala kwenye mitando ya kijamii na miongoni mwa waliolijadili ni Wakili Peter Kibatala aliyeandika ujumbe kupitia ukurasa wake, na baadaye alipotafutwa na Mwananachi kuufafanua, amesema amewaelekeza mawakili wiwili kwenda kutoa msaada wa kisheria kwa kijana huyo.

“Hatutaingilia maamuzi ya mkuu wa mkoa aliyetaka kijana huyo ahojiwe, lakini atakapopelekwa mahakamani ana haki ya kupata msaada wa kisheria, ndiyo maana niliwagiza mawakili wenzangu wawili kwenda kumsaidia kijana huyo,” amesema.

Wakili wa kujitegemea, Philip Mwakilima akizungumza na Mwananchi amesema hakuna sheria wala kifungu kinachoonyesha kuchoma au kutochoma picha ya kiongozi huyo ni kosa na hakuna athari yoyote kwa jamii.

(Imeandikwa na Waandishi Wetu)

Mwananchi
Hao polisi wasiojuwa wampe kesi ipi ni wajinga tu.

Kuchoma picha ya Rais hadharani ni treason.
 
Viongozi wetu ni vizuri zaidi kutumia hekima na busara kuliko mihemko.
Ofisi ya RC ina Mwanasheria ni vizuri kupata ushauri wa kitaalam kabla ya maamuzi, kama sivyo mtawaumiza wananchi bila hatia.
 
Endeleeni kuwapotosha vijana kutoka familia maskini huku wa kwenu mkiwahimiza kuwa makini na kujiepusha na siasa za kipumbavu. Huwezi kukuta mtoto wa kiongozi wa ngazi za juu CHADEMA anafanya harakati za kipumbavu au kuropoka hovyo. Watoto wa maskini kama kina Mdude ndo hutolewa kafara ili kupata political mileage. Wewe mleta uzi nina uhakika huwezi ruhusu mwanao achukue picha ya Rais na kuichoma huku akirekodi video.
Acha dharau, siasa za kipumbavu za nyoko.
 
Kenya wangekuwa kama sisi ungekuta magereza yamejaa makosa ya aina hiyo.
 
Sawa , mbumbumbu mwenzio aliyechoma picha ya mh rais keshahukumiwa miaka miwili jela au faini milioni tano. Nakushauri andamaneni au mumlipie faini asalimike na kifungo , la sivyo jela inamhusu.
Unaonyesha jinsi ulivyo mweupe kichwani! Jela kapelekwa siyo kwa sababu kavunja sheria bali kwa sababu chawa wametumia madaraka kinyume cha katiba na sheria za nchi.
 
Jikite kwenye hoja, Je kuchoma picha ni kosa kisheria?

Halafu huo ujinga wa kuona kila anayepinga serikali katumwa ni dharau sana, yaani unataka kusema Watanzania ni mbumbumbu na kwamba hawawezi kuamua mambo wenyewe na kutafakari hadi watumwe?

Hakika utalipwa kwa dharau zako hizo, Wallah tena!
Tena ungemalizia na neno fala kabisa
 
Kwamba hata yule kijana aliyekamatwa Rungwe kwa kosa la kuipiga kiberiti picha ya Rais Samia, hana kosa lolote na hata wakamataji hawajui wampachike kesi gani, maana kwa katiba ya Tanzania kitendo kile ni sawa na mtu kuokota makaratasi ili awashie mkaa kwenye jiko lake.

Inadaiwa kukamatwa kwake kumesababishwa na mihemko tu na fikra duni za viongozi wa Mbeya

=========

Ni siku tatu tangu Jeshi la Polisi mkoani Mbeya limkamate Shadrack Chaula (24), kijana anayetuhumiwa kuchoma moto picha ya Rais Samia Suluhu Hassan, suala hilo limeibua mvutano wa kisheria, ikielezwa hakuna sheria iliyovunjwa.

Akizungumza na Mwananchi jana Julai 3, 2024 kuhusu kosa la kijana huyo na lini atafikishwa mahakamani, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Benjamin Kuzaga amesema jukumu lao liliishia kumkamata suala la kupelekwa mahakamani linabaki kwa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka.

“Siwezi kusema ni lini atapelekwa mahakamani, kazi yetu ilikuwa ni kumkamata, Ofisi ya Mashtaka ndiyo itaandaa mashtaka kwa kuangalia ushahidi na kuonyesha ni vifungu gani vya sheria mtuhumiwa amekiuka,” amesema.

Suala hilo pia limeibua mjadala kwenye mitando ya kijamii na miongoni mwa waliolijadili ni Wakili Peter Kibatala aliyeandika ujumbe kupitia ukurasa wake, na baadaye alipotafutwa na Mwananachi kuufafanua, amesema amewaelekeza mawakili wiwili kwenda kutoa msaada wa kisheria kwa kijana huyo.

“Hatutaingilia maamuzi ya mkuu wa mkoa aliyetaka kijana huyo ahojiwe, lakini atakapopelekwa mahakamani ana haki ya kupata msaada wa kisheria, ndiyo maana niliwagiza mawakili wenzangu wawili kwenda kumsaidia kijana huyo,” amesema.

Wakili wa kujitegemea, Philip Mwakilima akizungumza na Mwananchi amesema hakuna sheria wala kifungu kinachoonyesha kuchoma au kutochoma picha ya kiongozi huyo ni kosa na hakuna athari yoyote kwa jamii.

(Imeandikwa na Waandishi Wetu)

Mwananchi
Kuna maneno ya kumkashifu rais. Hilo ni kosa kisheria l. Mbona kesi iko wazi sana.

Nadhani kuna haja ya kuchuja watu hapa JF
 
Hatoenda jela maana imeandikwa Shetani hajawahi kumshinda Mungu, na huyo hakimu wenu aliyepewa maelekezo amfunge asubiri laana kuu wiki hii
Hahahahahahahah laana ya CHADEMA huwa ni baraka. Ukilaaniwa na CHADEMA ina maana kazi yako ulifanya kiusahihi. Genge la wala michango haliwezi kumlaani mtu.
 
Hao polisi wasiojuwa wampe kesi ipi ni wajinga tu.

Kuchoma picha ya Rais hadharani ni treason.
Imeandikwa wapi hiyo? Lete kifungu cha sheria? Mbona ameshtakiwa kwa kusema uwongo na siyo treason yako?
 
Kila unachomiliki wewe haimaanishi hakina nidhamu zake.

Picha ya Rais wa Tanzania ni nembo ya taifa.
Imeandikwa wapi? Kijana anakatiwa rufaa na akitoka itafanyika tafrija ya kuchoma picha za wanafumbia macho utekwaji na utesani wa watanzania...unaalikwa kushuhudia tukio hilo
 
Play stupid games win stupid prizes. Acha akanyee debe
 
Read the law Arson haipo namna hyo
Acha ujinga...umesoma hukumu ya huyu kijana aliyechoma picha ya rais? Kashtakiwa kwa kosa la kusema taarifa za uongo kama yule alieachiliwa majuzi....kuchoma picha yako unayomiliki mwenyewe siyo kosa kisheria
 
Back
Top Bottom