Mvuto wa Ajabu: Watu, Watoto na Wanyama. Mabaya yapo pia

Mvuto wa Ajabu: Watu, Watoto na Wanyama. Mabaya yapo pia

Karibu yote hayo yananitokea kasoro hapo kwenye wanyama. Sipendi wanyama huyo paka akinisogelea tu naweza hata nikamfukuza.

Kuna ile nyingine, bidhaa haivumi kabisa mfano tshirt au begi la mgongoni halafu baada ya kununua na kuanza kutumia ghafla inakua chaguo la wengi. Hii imetokea sana wakati nipo chuo. Unakuta viatu vya design fulani ambavyo havivumi kabisa chuoni. Nikinunua na watu kuniona navyo ghafla vinakua maarufu. Hii niliishtukia nikatengeneza logo yangu nikawa naprint tshirt naziuza kwa wanafunzi wenzangu chuoni. Nilipiga sana hela chuo.

Kuna nyingine moja hiyo watu kufikiria nina hela, yaani nikiingia sehemu wananichukulia kama kijana fulani hivi ambae ameshajipata, mambo safi kumbe mimi mwenyewe apeche alolo tu.

Kuna nyingine hiyo tupo sehemu watu wanaendelea na mabishano yao. Mimi nipo kimya nipo bize tu mambo yangu labda naperuzi mtandaoni au naangalia mpira. Halafu ghafla mmoja wapo ananipoint kutaka niongee chochote kuhusu topic wanayobishana.

NB: una kipawa cha ushawishi mdogo angu. Ingia kwenye siasa au fungua kanisa upige vichwa
OK,
Hata mimi huwa najikuta naongea kitu sijawahi kusikia ila nimekiwaza tu then watu wanaenda kuchek mtandaoni wanasema nilikuwa right
 
Unapokua na aura/nyota safi maana yake ukifanya mapenzi mnabadilishana nguvu, kama wewe ulikua ni mchafu, uchafu wako unaenda kwa yule mwingine unabaki msafi, au unapungua ila pia na yeye ile nguvu yake yeye unakua umeibeba wewe, ukija kwenda kwa mwingine unaenda kubeba vya mwingine na kuacha vya kwako.

Hivyo unaweza kukuta ni kama mzunguko tu, Hapa hua wapo wanaokua wanajua wanachokifanya, Energy vampires, wanavuna nguvu yako kiroho kupitia tendo la ndoa, hii hua ni kazi rahisi sababu kwenye tendo unakua umeenda kwa kukubali mwenyewe. ukiona kuna mtu unafanya nae ndio mambo yako yanyooke wewe ndo huyo Energy vampire, sasa kua kitaalamu,

Kuna familia kabla ya kuoa au kuolewa lazima wakague mpaka nyota yako, watu hawataki utani kabisa au kubahatisha. Familia za kitajiri nyingi hauoi hovyo, wahindi mpaka harusi zinapangwa kulingana na energy, destiny n.k ili waendeleze PROSPERITY.

ukitembea na wanawake tofauti tofauti maana yake kila siku mnabadilishana bahati nzuri, mikosi, mabalaa, laana n.k vyote mnakua mnabebeshana.
Hapa siku pingi mkuu
 
Is this true? Kwamba ukiconnect na mtu, iwe kibiashara, kikazi au kimahusiano kuna energy mnabadilishana? Kama jina negative energy na mwenzangu ana positive energy tunabadilishana? How does this work?

Kuna vitu kwangu vinabaki kuwa nadharia naona havina uhalisia!!
Kuna subtle energy exchange ambazo kwa akili ya kawaida unaweza usivione ila vipo
 
what is samadhi and what is Satori?

Ila naweza kukupa experience zangu kama zina reasonate unachokisema.
Satori is the no mind-body expireince. Where you become luminous of your true nature.. Beyond time and space
 
Ndio maana naonaga vijana Wana mapete mengi mengii mikononi
Hao wanaweza wakawa wanavaa kama urembo tu, ila chunguza pete kama za msanii Ali kiba, ndio mfano wa pete kama zile ni madini yale yana nguzu zake mbalimbali kutokana na kito husika.
 
Japo Mimi ni mkristo ila mtu kama shekhe WALID

huyu jamaa ana nyota ana mvuto hata ongea yake huchoki kumsikiliza mwingine ni gwajima hata prophet IPM anaweza kuongea vizuri sana.

Nb. Jaribu kuiga anacho kieleza au kuongea uone kama utaweza kuwa kama wao

Izi ni vipawa/ karama za kipekee za watu ambao ni gifted
Na huwa ni mpaka mtubutulie kabisa maana mara nyingi watu hawajui kuzichannel hizo energy
 
Kuna movie moja hivi ya comedy ya wazungu sikumbuki jina lake. Kuna mshkaji alikua dokta wa meno. Yeye akisex tu na mwanamke, huyo mwanamke soon anaolewa. Basi mademu walivyoshtukia mchango ikawa balaa. Jamaa asubuhi anafika kazini anakuta foleni ya wanawake nje ya mlango wa ofisi yake.

Tumia fursa hiyo mkuu.
Hahahaha, ajidanganye aige vitu ambavyo habimake sense.. 😂
 
Energy hii ninayo sana, mifano mingi sana
No. 1
Katika harakati kusaka kibarua nilipita ofisi moja, reception kulikuwa na watu wengi wamekaa kwenye benchi ile naingia niliangalia mara moja ila safari yangu kufika dirisha reception nikaamua kuangalia ASEE macho yote kwangu, nlipotezea kiaina, nmefika nikaanza kuulizia ishu ilonipeleka kabla sjamaliza nkashangaa napapaswa kugeuka kitoto kimemuacha mama ake ambaye alikuwa naye anaelekea sehemu nyingine kikanifuata nilikisemesha na kukiambia mama ana kuita, hakikuondoka hadi alipokifuata kuendelea na na safari yao 😃. Niliwaza sana hiyo moment, nilivyofika hapo nikahamia ofisi nyingine - maneno ya jamaa(MTUMISHI) yalinipa nguvu sana "UNA ENERGY NZURI SANA nikamuuliza kivipi sijaele-CONFIDENCE &PRESENTABLE, NINGEKUWA MKURUGENZI NINGEKUAMBIA KESHO NJOO UANZE KAZI tuliongea mengi kana watu tunajuana kitambo kumbe tulikutana siku hiyo moja ya swali niliuliza zaidi ni nini alichoona kwangu akasema FIRST IMPRESSION MATTER & NINA ENERGY NZURI alinipatia mawasiliano yake.
Yapo mengi uvivu kuandika🙌🤐
Keep sharing mkuu..

Kuna siku nimependa zangu restruant, sasa nipo zangu tu idle kwenye Meza yangu, then nashangaa katoto ka kike kamekuja nilipo nikaanza kkkukasemesha kameniangallia machoni huku kametabasamu

The whole time me mwenyewe naona aiibu familia yake na kila mtu wanatuangaliia..
 
Kwaio mtu anapewa dawa au unarogwa kwa nyota au inakuaje kama una weza KUELEZEA kwa faida ya wengi
MImi nakusudia kwamba unakuta kwamba unafanya kazi labda dukani kwa mtu na huyo boss unakuta ameshagundua nguvu uliyonayo, sasa wewe hujui kama una hicho kitu hivyo boss anafaidika sana kwenye biashara yake kupitia uwepo wako hapo ilihali wewe anakulipa ujira wa kawaida wakati kama ungejijua ungeweza kufanya shughuli zake mwenyewe ukafaidika na hiyo nguvu. Sasa unaweza kukuta boss anakuonyesha upendo sana kumbe anajua wewe ndio unamtajirisha.

Kuna maboss wengine ili amuajiri mfanyakazi kwanza anamchunguza nyota yake, sasa bora ibaki kukutumia tu hivyo kuliko wakaamuwa kuitumia hiyo nyota yako kichawi kwamba wewe unaishi maisha yako huko ila wao wanaitumia nyota yako.
 
Interesting,

huyo unaohisi ni wewe ni EGO.

Body + Mind + Soul = complete human.

Hakuna kinachomvaa mwenzake,

Mtu anapozaliwa hua anakua conditioned na mind kulingana na mazingira, hvyo atapewa jina, elimu, n.k. hivyo mind inakua very rigid na kushikamana na mifumo, hapa ndio kunazaliwa kinachosemekana psychology, in reality hakuna vichaa bali kuna watu ambao wamekosa alignment kwenye MIND sababu ya kutoka kwenye mifumo pasipo kua na grounding.

unachojaribu kukisema wewe ni EGO = hicho ndio kinakudanganya kua you are a spiritual person, na hilo ndio vazi sasa, ila kiuhalisia wewe haupo, ni kama vile mimi sipo ila unatambua hii ID hapa.

Body + Mind + Soul = ONE, Monad, Mungu mmoja, or whatever you can personalize it.

Sasa ili kuunganisha vyote vitatu, changamoto wengi inakuja kwenye mind ku drop systems tulizovishwa na jamii, hapa ndio ukifanikiwa watu wanaita enlightment, gnosticism, individuation n.k

Wengi ambao wanajiita spiritual people hua ni watu walioshiba EGO na wanajiona kwamba wao wako tofauti na maumbile, ndio maana sijashangaa ww kusema unajiona kama alien n.k sababu Ego imevaa vazi la spirituality.

Bila BODY and MIND, soul inakosa expression, bila Body , soul and mind vinakosa expression, bila mind, soul and body vinakosa expression. Mwili ukifa utarudi tena kupitia mwili mwingine mpaka utakapomaliza safari, na kumaliza safari it is a successful coagulation or union of BODY MIND and SOUL, hvyo hicho unachosema kinachelewesha ni EGO, ambayo unapokaa kwenye meditation lengo ni kuiua hyo ego ikose power ili uunganike moja kwa moja na Soul (The true essence of YOU)
Had to smile! This is powerful.
 
Hapa kwenye first impression matter umenikumbusha mbali sana

Kuna dada mmoja nilikuwa nafika lodge yao kila nikienda kwenye mishe huko mkoani

Baada ya kuanza kubadilishana energy sijui ni hasi au positive,siku moja ananiambia "yani siku ya kwanza kukuona tu nilitokea kukuelewa sana" 🤣🤣
Wewe ulikuwa unasakwa tu hapo...
Angekwambia siku ile ile ya kwanza
 
MImi nakusudia kwamba unakuta kwamba unafanya kazi labda dukani kwa mtu na huyo boss unakuta ameshagundua nguvu uliyonayo, sasa wewe hujui kama una hicho kitu hivyo boss anafaidika sana kwenye biashara yake kupitia uwepo wako hapo ilihali wewe anakulipa ujira wa kawaida wakati kama ungejijua ungeweza kufanya shughuli zake mwenyewe ukafaidika na hiyo nguvu. Sasa unaweza kukuta boss anakuonyesha upendo sana kumbe anajua wewe ndio unamtajirisha.

Kuna maboss wengine ili amuajiri mfanyakazi kwanza anamchunguza nyota yake, sasa bora ibaki kukutumia tu hivyo kuliko wakaamuwa kuitumia hiyo nyota yako kichawi kwamba wewe unaishi maisha yako huko ila wao wanaitumia nyota yako.
Hii ipo sana na watu wanatembea na karama kubwa hawajijui wanakua watumwa wa kutumika kuwafaidisha wengine
 
Back
Top Bottom