atafanya nini kwa ukaidi wa serikali wakifanya uchaguzi bila katib mpya wala tume huru?
1. Kulikoni ndugu kuwa "an angel of doom" pasipokuwa na sababu zozote? Kwanini kutaka kututisha kwa niaba ya adui yetu?
Jibu langu kwako ni kuwa:
"tutalivuka daraja tutakapokuwa tumefika darajani."
Zingatia kichwa cha mada:
"Mwabukusi na mfupa uliowalemea wengi."
Dhahiri bin shahiri ni "pessimism" yaani "fear of the unknown" utakuwa ndiyo ule "mfupa" uliowalemea wengi.
Hamuwezi bado kuwa na furaha sasa kuwa akiliweza mwingine kwa niaba ya taifa ni jambo la kheri la kushiriki japo kwenye kusherehekea sote matunda yakipatikana?
Kulikoni nyie kufikiria mabaya tu? Hamjipi hata nafasi ya kufikiria mema, mafanikio, au ushindi?
Ninyi fikra zenu kwenye kushindwa tu? Looh! Watu wa namna gani nyie?
Na ninakwambia kwa Samia alivyo (dikiteita mkubwa kuwahi kutokea at least) hakuna katiba wala tume huru ya uchaguzi. Atafanya nini kama mwabukusi?
2. Mkuu wewe siyo nabii Tito.
"Kwamba nani au mama Abduli yuko vipi, hiyo inatuhusu nini sisi? Labda kama ungependa tujichagulie adui ndugu?"
Nani asiyejua kuwa mwisho wa matatizo yetu ni Tahrir? Wewe unajua. Chadema inajua. Samia anajua. CCM inajua. Nk, nk.
Tunataka haki? Hatutaki tozo? Tukutane Tahrir
Kulikoni kutoamua kuyamaliza matatizo yetu sasa?
au Slaa (mchumia tumbo la ubalozi, unadhani angelikuwa Sweden angelikuwa na Mwabukusi), au Mdude?
3. Hekima yenu inapatikana wapi?
August 6, 2023 kulikuwa na uzi huu:
CHADEMA wa Mtandaoni watamwelewa lini Dr. Lwaitama?
"Waswahili wanasema yaliyopita si ndwele ..."
Nyie mmeng'ang'ania chuki tu. Kulikoni kuwa kama "luba?"
Walikuja Lowassa, Sumaye, Nyalandu nk, kwa wakati wao wakaondoka. VIvyo hivyo kina Shilinde, Matambi na wenzao. "No hate no fear." Tatizo liko wapi? Watu watakuja, na wengine watakwenda. Hiyo ni kawaida. Malaika tujawapate wapi?
Hatuwezi kuwa na marafiki wala maadui wa kudumu. Na huo ndio ulio ukweli.
Kuunganisha nguvu na vyama vilivyopo kungelikuwa na msukumo /pressure zaidi kwa CCM kuliko hiki wanchokifanya hawa watatu.... na maria spaces
Mkuu, kwanini mnachofanya ninyi mnadhani ndicho kilicho sahihi? Kwanini ninyi hamchukui hatua kuunganisha nguvu na wengine? Jitihada za kuunganisha nguvu ziko wapi?
"Compromise" ni pande mbili. Hata msumeno hukata ukienda na pia ukirudi.
"Hamtaki suluhu. Kumbe mnataka nini basi ndugu zetu?"
Kwanini kukaza ubongo hivi na kudhania mlio sahihi ni ninyi tu?
Uzi huu ulikuwa na maana kamili:
Kwanini Wakili Mwabukusi na wenzake wanastahili kuungwa mkono
Kwani nani anataka kupigiwa magoti? Kwanini tusiangalie hoja kwa maslahi mapana ya nchi?
Kwanini kama vipi kutaka kuzitatiza jitihada takatifu hizi za wananchi?
"Tusioneane haya machoni ndugu zangu."
Uzi huu ulikuwa wa Aug 28, 2021:
CHADEMA: Bila kuwapa Makavu hakuna Katiba Mpya
Maudhui yake hata leo yangali yanaishi.
NOTE: WATANZANIA HAKUNA WA KUHIMILI KUPIGWA RISASI AKIWA ANAANDAMANA, SISI NI WAOGA, MIMI NA WEWE NA YULE.....................
4. Wamekufa kina Mahlangu, Biko, nk. Wamekaa jela kina Mandela, Sisulu, nk. Wamekuwapo kina Tutu ndugu. Majina yao tapo yameandikwa kwa wino wa dhahabu Afrika Kusini huko.
HAMAS, Gaza huko hakuna asiyejua nini kinaendelea.
i). "Ni heri kufa ukipigania nchi kuliko kufa kwa Malaria." -- Lwaitama.
ii). "Usitutishe, usitutishe, usitutishe, ..ninarudia usitutishe!" -- Maalim Seif. (RIP)
Angalizo:
"Kuteleza si kuanguka hakuna aliye mkamilifu, mkubwa au wa muhimu zaidi kuliko Taifa. Tulipo ni pema zaidi. Tujikite kwenye maelewano kuliko mafarakano."
Tukumbuke hata misahafu ya dini husema:
Heri wapatanishi, kwa maana hao wataitwa wana wa Mungu.
Cc:
Zawadini