Mwaka 1988 Chakachaka alipiga show Makondeko Kibamba kiingilio kilikuwa 100,000

Mwaka 1988 Chakachaka alipiga show Makondeko Kibamba kiingilio kilikuwa 100,000

[mention]Malila [/mention] na [mention]tbjlj [/mention] Michael Jackson hakupata kutumbuiza lakini mwaka 1992 alitembelea nchi nne za Africa kwa ziara binafsi ambapo alitembelea ivorycoast, Kenya na Tanzania na nchi nyingine nimesahau, kuja Tanzania ilikua Rais mwinyi anataka MJ aende akapige picha serengeti na mlima kilimanjaro ili wazitumie kwenda kutangaza utalii duniani huko, lakini dili haikufika mwisho na nakumbuka aliondoka Tanzania kurudi kenya ambako hakukaa akaenda london na ilikuja kufahamika baadae kua meneja wake alimpatia dili nyingine kubwa huko hivo ikaishia tu Rais mwinyi kupiga picha na MJ
View attachment 2582394
View attachment 2582395
Na alipokuja Tanzania alifikia Kilimanjaro Hotel
 
Siku watembelee pale Hyatt Regency level 8 wajionee watu wanaotumia pesa hapa mjini

Kwanza ukumbuke watu wengi hatujafanya starehe kabisa leo hii kidimbwi bila walau 1m hutoboi na ndio pakawaida tu, na watu wanajichanga table hata 4m inakatika kwa package zao, watu wa bata za kawaida alikua anajua kabisa nikigonga bills ( billcanaz) weekend hii weekend inayofuata nagonga kisigino tripple A , arusha then narudi town, weekend nyingine mtu yuko villa mwanza tena hii miaka ya karibuni tu ukisikia sijui the magic 101 kahama ni kiwanja kipya lazima kitengewe weekend, ukisikia sijui the cask lazima kitakua na weekend yake hujakaa sawa mara miaka ya 2010 hapo ukipata safari za Iringa unajua nitachoma nyama sterio na maji kidogo lakini nitagonga kisigino twisters au VIP huko then naenda zangu kulala hapo sasa ni miaka ya juzi achana na mbowe club za wahenga,
 
Hela ilikuwepo sana enzi za mwinyi,nzee wangu alijenga nyumba nyingi sana kipindi hicho
Umenikumbusha mkuu

Enzi hizo viwanja vinapimwa Sinza na Kinondoni ilikuwa kama leo unavyoina Madale inavyojengeka nyumba ziko mbalimbali kila kona ni harakati za ujenzi

Watu wlikuwa wanatoka Ilala, Magomeni, Kariakoo, Temeke wanaenda kununua viwanja Sinza na Kinondoni

Leo pamejaa ni mwendo wa kununua na kumhamisha mtu. Jiji linakuwa kwa kasi sana

Watu wawekeze kwenye ardhi haitawatupa.
 
Watu waliozoea bata hata akisikia vanga na mnanda ataufuata kuona hatma yake na mtakutana kesho asubuhi akiwa anarudi tena kwa mguu, kikubwa ashatoka kuserebuka na roho imetulia
Tuliwahi kutoka home Upanga na jamaa zangu kwenda kwenye mnanda pale Temeke ukumbi wa Super Stereo, kipindi hicho ngoma iliyokuwa inatamba Bwana Kipaka ya Atomic.
 
Umenikumbusha mkuu

Enzi hizo viwanja vinapimwa Sinza na Kinondoni ilikuwa kama leo unavyoina Madale inavyojengeka nyumba ziko mbalimbali kila kona ni harakati za ujenzi

Watu wlikuwa wanatoka Ilala, Magomeni, Kariakoo, Temeke wanaenda kununua viwanja Sinza na Kinondoni

Leo pamejaa ni mwendo wa kununua na kumhamisha mtu. Jiji linakuwa kwa kasi sana

Watu wawekeze kwenye ardhi haitawatupa.

Watu wanahamishwa na wengine walikimbilia mapinga, kibwegere, madale, chanika, vikindu, kisemvule, mlandizi, yaani kote maisha unapisha wenye pesa wajenge, hasa anakuja mtu kama denfrance whiteinn sinza unaachaje kumpisha? Na kafika bei
 
Pesa ilikuwepo kipindi hicho. Mzee wangu alisafiri mwaka 1994 dar hadi malawi kwenda tamasha la mnyama lucky dube.
kuna mabwege fulani kwenye uzi huu, wakisoma hiki ulichoandika, watasema babaako alikuwa mfujaji sana, utadhani walikuwa wanamsaidia kuzitafuta.

kuna watu umaskini umeharibu sana akili zao.
 
Watu wanahamishwa na wengine walikimbilia mapinga, kibwegere, madale, chanika, vikindu, kisemvule, mlandizi, yaani kote maisha unapisha wenye pesa wajenge, hasa anakuja mtu kama denfrance whiteinn sinza unaachaje kumpisha? Na kafika bei
Lazima uumpishe dau analokupa hata haufikirii mara mbili unasema asije akahairisha bure ukose mahela

Kuna mzee mmoja alikuwa ni daktari alikuwa na eneo kubwa hapo Victoria aliuza bilioni 1 kipindi cha Kikwete

Mzee hata hakujifikiria mara mbili katafuta mwanasheria zikapigwa saini za mauziano mzigo ukaingia kwenye akaunti yake
 
Imepita miaka 35,
Nimekumbuka kitu kimoja
mwaka 1988 enzi hizo Ivon Chakachaka akiwa kwenye peak,kulikuwa na mmakonde mmoja akiitwa Dk Khalid Alex mbunge wa Mtama by then,sina uhakika na jimbo ila ni huko kusini
,alikuwa na ukumbi kule kibamba Luguruni maarufu kama Makondeko,

Ule ukumbi ukienda leo hakuna hata mabaki ya tofali hata moja ulikuwa ukumbi wa kisasa kwa miaka ile,kumbuka ulikuwa utawalawa Mzee Ruksa,

Chakachaka akiwika na nyimbo zake kama Sangoma,Umkhomboti,Thank you Mr Dj,am in love with DJ,alikuwa wa moto kwelikweli ila huyu tycoon wa enzi hizo bwana Alex akafanikiwa kumleta nchini,kiingilio kilikuwa shilingi laki moja,lakini ukumbi ulifurika aswaa japo uko nje ya mji,ni miaka 35 imepita ila laki moja !!!
Huyu dada alikuwa 'mtamu' sana enzi hizo...
 
Naelewa kuwa dala ilikuwa ni shilingi tano,
Nilikuwa najaribu kuelezea kwa nini ile sarafu ya sh 5 iliitwa dala!!
One dollar ilikaa muda mrefu sana ilikwa na thamani ya sh 5 , ile sarafu ilipotoka ikaitwa one dollar , waswahili tukaibatiza dala
Sasa nini kilitokea hadi dollar ikafika 2390?
 
Umenikumbusha mkuu

Enzi hizo viwanja vinapimwa Sinza na Kinondoni ilikuwa kama leo unavyoina Madale inavyojengeka nyumba ziko mbalimbali kila kona ni harakati za ujenzi

Watu wlikuwa wanatoka Ilala, Magomeni, Kariakoo, Temeke wanaenda kununua viwanja Sinza na Kinondoni

Leo pamejaa ni mwendo wa kununua na kumhamisha mtu. Jiji linakuwa kwa kasi sana

Watu wawekeze kwenye ardhi haitawatupa.
Nashangaa Dodoma bado haikui kwa miaka 6 ambayo Serikali imehamia, ila Dsm ukifika kkoo panavunjwa hatari
 
Sasa nini kilitokea hadi dollar ikafika 2390?

Thamani ya pesa kwa nchi za afrika mashariki yaani Tanzania na kenya ilikua ni sawa, kidogo uganda ilikua chini sasa mambo yalibadilika kwa mzee mwinyi ambapo tulianza kuimport zaidi kuliko kuexport, na kwa Nyerere viwanda Tanzania vilikua vingi tu vinazalisha bidhaa nakuuza nje urafiki, mwatex, bora, general tyre na tobacco hivo tuliuza nje zaidi, mzee ruksa aliona ujamaa unatuchelewesha ikawa sasa ni Ruksa kufanya biashara kachukue chochote leta uuze au peleka chochote kutoka nje ufanye biashara ni ruksa, hapo thamani ya shilingi ikaanza kuporomoka hadi leo, hadi kwa mkapa mwanzoni dollar moja ilikua kama sawa na shilingi 500 hivi kama sijasahau, ikaja dola moja ikawa sawa na 1000 na ukumbuke kenya wao viwanda vilizidi kua vingi na kufanya kazi na wamefanya export zaidi na zaidi hivo japo nao shilingi yao inayumba lakini kwa east africa wako bado imara, na kwa sasa east afrika ni mpambano mkali kati ya Tanzania na kenya japo na wengine hawajalala wanatufukuza kimyakimya hivo tungepata uongozi wakusimamia shilingi vizuri naamini ingepanda tena zaid lakini tukipata kiongozi anawaza ile Tanbond aiuzie nchi nyingine halafu ipewe jina la blueband na ije tuuziwe tena balaa huanzia hapo
 
Umenikumbusha mkuu

Enzi hizo viwanja vinapimwa Sinza na Kinondoni ilikuwa kama leo unavyoina Madale inavyojengeka nyumba ziko mbalimbali kila kona ni harakati za ujenzi

Watu wlikuwa wanatoka Ilala, Magomeni, Kariakoo, Temeke wanaenda kununua viwanja Sinza na Kinondoni

Leo pamejaa ni mwendo wa kununua na kumhamisha mtu. Jiji linakuwa kwa kasi sana

Watu wawekeze kwenye ardhi haitawatupa.
Kijitonyama na sinza ni swamp area ,watu wamelima sana mipunga maeneo hayo miaka hiyo
 
Thamani ya pesa kwa nchi za afrika mashariki yaani Tanzania na kenya ilikua ni sawa, kidogo uganda ilikua chini sasa mambo yalibadilika kwa mzee mwinyi ambapo tulianza kuimport zaidi kuliko kuexport, na kwa Nyerere viwanda Tanzania vilikua vingi tu vinazalisha bidhaa nakuuza nje urafiki, mwatex, bora, general tyre na tobacco hivo tuliuza nje zaidi, mzee ruksa aliona ujamaa unatuchelewesha ikawa sasa ni Ruksa kufanya biashara kachukue chochote leta uuze au peleka chochote kutoka nje ufanye biashara ni ruksa, hapo thamani ya shilingi ikaanza kuporomoka hadi leo, hadi kwa mkapa mwanzoni dollar moja ilikua kama sawa na shilingi 500 hivi kama sijasahau, ikaja dola moja ikawa sawa na 1000 na ukumbuke kenya wao viwanda vilizidi kua vingi na kufanya kazi na wamefanya export zaidi na zaidi hivo japo nao shilingi yao inayumba lakini kwa east africa wako bado imara, na kwa sasa east afrika ni mpambano mkali kati ya Tanzania na kenya japo na wengine hawajalala wanatufukuza kimyakimya hivo tungepata uongozi wakusimamia shilingi vizuri naamini ingepanda tena zaid lakini tukipata kiongozi anawaza ile Tanbond aiuzie nchi nyingine halafu ipewe jina la blueband na ije tuuziwe tena balaa huanzia hapo
Mkuu tukipata viongozi imara Kenya atapata taabu sana
 
Nashangaa Dodoma bado haikui kwa miaka 6 ambayo Serikali imehamia, ila Dsm ukifika kkoo panavunjwa hatari

Dodoma haina asili ya wapambanaji kiuchumi wagogo bado wavivu sana , uwepo wa vyuo, bunge vikao vya viongozi kila leo, achilia mbali kwa sasa serikali imehamia jumla ingekua ni wapambanaji dom ingesahaulika miaka 10 tu, halafu Dar kamwe tusiifananishe na mkoa wowote Tanzania, dar ni lango kuu la kutokea na kuingia Tanzania bado Dar itabaki kua Dar, sehemu ambayo bado itakua muhimu kwa uchumi wa nchi yetu, acha ligi za Arusha na mwanza, njombe na kahama, ziendelee lakini bado Dar ni dude kubwa sana
 
Back
Top Bottom