Mwaka 1999 kurudi nyuma ilikuwa ngumu sana kuchaguliwa shule ya Sekondari ya Serikali. Waliobahatika walijulikana kata nzima. Je, wewe ni mmoja wao?

Asanye Serikali ya CCM kuongeza secondary kwa wingi!
 
Sasa hivi C mbili na D moja unaingia advance
Tena unaweza kuta C za civics na nutrition, D ya Bible/Islamic knowledge

Chuo E mbili

Akitoka hapo hataki kazi za bodaboda, eti anataka kazi za hadhi yake, hivi wana hadhi gani hawa mbwa!!!!
Kwa chuo kwa sasa lazima uwe na D mbili na kuendelea
 
Andika tena mkuu mimi bado sijakuelewa
Watu wa zamani,fresh from school au college. Walipokuwa wakiajiriwa,uwezo wao siku za mwanzo kazini ukilinganisha Na waliowatangulia kazini . Tofauti ya kiuwezo ilikuwaje?
 
Jangwani na Zanaki,kisutu na Forodhani,Kibasila hazikua Secondary?,naanza kupata wasiwasi na wewe
 
ulikuwa mzembe sana chief, au ndo ulikuwa mtoto wa mama sana
 
Mwaka 2001 mwezi wa 5 nilimaliza Advance kwa bahati nzuri tulifaulu wanafunzi karibu wote. Wale wachache waliobakia walienda kusoma TUMAINI UNIBERSITY. Wale watu tulikuwa tunawadharau sana kwakuwa wanasomeshwa na wazazi wao. Chuo hapakuwa na loan board.
Dah walikuja kusoma watoto wa masikini kwelikweli. Wengine tuliwasaidia kuwavusha barabara.
 
Hiyo haikuishia mwaka wa 1999, ilikwenda mpaka 2001/2 hivi, nakumbuka nilifaulu Mkolani Sekondari, ila kulikuwa mbali kipindi hiko na usafiri ulikuwa ni wa Taabu haswaa! Baba akanambia nihamie Thaqaafa nikakataa nikamjibu mimi nimefaulu siwezi kwenda shule ya waliofeli. Akanitizamaaa akaniacha kule kule. Kiukweli nilikuwa najisikia Furaha sana.
 
Umeandika kana kwamba ni jambo la kujivunia?

Unataka kusemaje? Kwamba ninyi ndio mlikuwa vipanga pekee hapa Tanganyika?

Excuse me, spare me the nonsense!

Ninachofahamu ni kuwa, shule zilikuwa chache sana. Wengi walikosa nafasi pamoja na kwamba walifaulu vizuri.

Halafu unakuja unajitapa hapa, ati ooohh tulienda sekondari wachache mno!

Kwamba ni swala la ujiko sana au wewe ulikuwa mtu spesheli sana kuliko wengine?
 
Kuna kauli moja Mh. Masaburi aliwahi kuitoa dhidi ya wabunge juu ya namna yao ya kufikiri ninaomba nisiiseme kwako.
 
Umenikumbusha Masurufu na Gorvement warrant wakati kwenda likizo
 
siyo elimu tu wanaufahamu kuliko hao viongozi wenu serikalini
Punguza kuropoka maneno ya kashifa na dharau.
Hao viongozi wengi unaowasema ni member humu JF.

Pia humu JF kuna watu wana uelewa mdogo sana hadi unajiuliza huyu ana matatizo ya akili au ya elimu?
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Ni kweli ....kwa zamani shule za private secondary zilikua za wale ambao hawakufaulu sana kwenda shule za serikali
Duh unanikumbusha mbali. Shuleni kwetu tulifaulu watatu tu tena wavulana. Ukienda private unaonekana hauna kitu[emoji23][emoji23]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…