Infantry Soldier
JF-Expert Member
- Feb 18, 2012
- 15,892
- 16,476
- Thread starter
- #181
Sawa bro.Nishakuelewa mkuu, ila nilikuwa nasisitiza tu kuwa zile zama sio za kujivunia, ni maoni yangu tu kwa ujumla
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Sawa bro.Nishakuelewa mkuu, ila nilikuwa nasisitiza tu kuwa zile zama sio za kujivunia, ni maoni yangu tu kwa ujumla
Katika 69 nilichaguliwa peke yanguUnaweza kukuta darasa la saba walikuwa hata 70 alafu wawili tu ndio walichaguliwa
Asanye Serikali ya CCM kuongeza secondary kwa wingi!Habari za wakati huu kaka na dada zangu wote wa hapa JamiiForums.
Ndugu zangu watanzania;
Mwaka 1999 kurudi nyuma ilikuwa ngumu sana kuchaguliwa shule ya secondary ya serikali. Wachache waliobahatika walijulikana kata/tarafa nzima. Je, wewe ni mmoja wao?
TABORA BOYS SECONDARY SCHOOL
View attachment 1661676
Juzi kuna mtoto wa jirani yangu alinifuata akaniambia brother ninaomba uniangalizie matokeo yangu ya darasa la saba. Mimi bila hiyana na smartphone yangu hii nikaingia katika website ya necta nikamuangalizia fresh tu. Dogo bwana alipata C flat masomo yoooote.
Nikajua ndio basi tena. Baada ya selection ya shule kutoka nikasikia huyu dogo amepangiwa shule moja ya kata mwendo kama wa dakika 20 kutoka hapa tunapokaa, ndio nikajisemea kimoyomoyo hakika dunia imebadilika kwa kasi sana.
Yaaani mtu anapata C flat bado anaenda secondary? Ninakumbuka dada yangu aliyeniachia ziwa, sasa hivi ni engineer, yeye ni moja kati ya wanafunzi 4 waliofaulu kwenda secondary shule ya serikali. Kumbuka enzi hizo kuchaguliwa tulikuwa tunaita kufaulu.
Yaaani wewe ukichaguliwa unaonekana umefaulu na wale ambao hawakuchaguliwa wanaonekana wamefeli ingawa kiuhalisia hawakuwa wamefeli ila shule zilikuwa ni chache mnoooo kiasi kwamba ni ngumu ku-accomodate wanafunzi wooote waliofaulu.
View attachment 1661678
Dada yangu alifaulu wakati huo baba anafanya kazi Wilaya ya ******* Mkoa wa Mbeya. Watu walifurahi familia nzima, lilipikwa pilau kana kwamba kuna sherehe ya kipaimara. Ndugu waliokuwa wanaishi karibu walikuja kumpa pongezi dada utadhani labda amejifungua mtoto.
Dada alikuwa maarufu sana kwa maana akiwa anaenda shuleni basi ni yeye tu ndiye aliyekua anaonekana asubuhi amevaa sare wakati huo wenzake aliomaliza nao darasa la saba bado wamelala au wameenda shambani.
Mgeni aliyekuwa hapafahamu nyumbani akiwa anaulizia kwa mama fulani wenyeji wanaanza kudadisi kwa kuambiana "au yule mama mjaluo ambaye mwanae anasoma secondary". Kwenda secodary ya serikali ilikuwa ni umaarufu kama dereva kwa maana enzi zile hakuna gari ya automatic transmission.
Gari zote ni manual na anayeweza kuendesha ni mzee mmoja au wawili tu mtaa mzima. Wanafunzi wa secondary walikuwa maarufu kama madereva kutokana na uchache wao.
View attachment 1661682
Matokeo yalikuwa yanasubiriwa kwa hamu na shauku kubwa sana kwa maana matokeo na selection zilikuwa zinakuja kwa pamoja tofauti na sasa hivi ambapo matokeo yanaanza kutoka na mwanafunzi au mzazi wake anaingia katika internet kisha baada ya mwezi mmoja mbele ndio selection inatangazwa.
Je, wewe ni mmoja ya wanafunzi wachache waliobahatika miaka ya 1990?
USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
Hata mie nilienda Tanga Tech,wilayani kwangu nilikua pekeyangu,kwa mkoa sina kumbukumbu,nyakati zile unajiona mwamba haswa,ila sasa tulifaulu watano shuleni kwetu,watatu tulikua WARUDIAJI,wa zamani tu ndio watanielewaAisee mimi ni mmojawapo... Na tulikuwa tunatoka sita tu mkoa mzima kwenda IFUNDA TECH kila mwaka... Nilijulikana ile mbaya yaani
Kwa chuo kwa sasa lazima uwe na D mbili na kuendeleaSasa hivi C mbili na D moja unaingia advance
Tena unaweza kuta C za civics na nutrition, D ya Bible/Islamic knowledge
Chuo E mbili
Akitoka hapo hataki kazi za bodaboda, eti anataka kazi za hadhi yake, hivi wana hadhi gani hawa mbwa!!!!
Watu wa zamani,fresh from school au college. Walipokuwa wakiajiriwa,uwezo wao siku za mwanzo kazini ukilinganisha Na waliowatangulia kazini . Tofauti ya kiuwezo ilikuwaje?Andika tena mkuu mimi bado sijakuelewa
Yaani ilikuwa taabu!97 - 4 = 93 hawa wote chaaaali, doooh Tanzania yetu imetoka mbali sana mkuu
Jangwani na Zanaki,kisutu na Forodhani,Kibasila hazikua Secondary?,naanza kupata wasiwasi na weweEnzi zetu kwa Dar shule zilikuwa nne tu basi yaani Pugu,Minaki,Tambaza,Azania hakukuwapo na Benjamini Mkapa.
Mtoto wa kiume unatakiwa ukaze ili uende angalau hata Aza Boy.
Ila binafsi nilichaguliwa Ilboru kata nzima nilikuwa mwenyewe ila DsM nzima tulikuwa watatu tu.
Advance tukatupwa mzumbe pale kwa DsM tulikuwa wa tano mkoa mzima.
ulikuwa mzembe sana chief, au ndo ulikuwa mtoto wa mama sanaNilianzia kuruka kichura kwenye hiyo round about hadi bwenini, ni mwendo wa viwanja viwili vya mpira wa miguu,begi na jembe nimejitwisha kichwani.
Nilivyo fika getini akanisamehe, akanirudisha tena nilipoanzia kuruka kichura kwa lengo la kujitambulisha.
Kweli maisha ni hatua...
Huyu alihadithiwa bwana basi muacheJangwani na Zanaki,kisutu na Forodhani hazikua Secondary?,naanza kupata wasiwasi na wewe
Kuna kauli moja Mh. Masaburi aliwahi kuitoa dhidi ya wabunge juu ya namna yao ya kufikiri ninaomba nisiiseme kwako.Umeandika kana kwamba ni jambo la kujivunia?
Unataka kusemaje? Kwamba ninyi ndio mlikuwa vipanga pekee hapa Tanganyika?
Excuse me, spare me the nonsense!
Ninachofahamu ni kuwa, shule zilikuwa chache sana. Wengi walikosa nafasi pamoja na kwamba walifaulu vizuri.
Halafu unakuja unajitapa hapa, ati ooohh tulienda sekondari wachache mno!
Kwamba ni swala la ujiko sana au wewe ulikuwa mtu spesheli sana kuliko wengine?
Umenikumbusha Masurufu na Gorvement warrant wakati kwenda likizoNdugu zangu waliosoma zamani kidogo itakuwa wanakumbuka vitu kama wali na maharage siku nne au tano ,wali nyama(nyama ya kuku,ng'ombe),maziwa,mikate mikubwa na siagi,uji uliochanganywa na maziwa,chai safi,madaftari na kalamu za bure,kuogelea bwawani,kula mboga za majani.........elimu imetoka mbali sana,sasa hiv ni balaa...
Punguza kuropoka maneno ya kashifa na dharau.siyo elimu tu wanaufahamu kuliko hao viongozi wenu serikalini
Nini wee? Typing error tyuuh
Labda alimaansha upande wa wavulana.Jangwani na Zanaki,kisutu na Forodhani hazikua Secondary?,naanza kupata wasiwasi na wewe
[emoji23] [emoji23] [emoji23]Tulipasua vibaya saana....nakumbuka wilaya nzima tulikiwa 15 tu tulijulikana!! Moshi Tech, Bihawana, Msalato, Weruweru; Tabora Boyz / Girls....
Wakati huo elimu under Mwalimu ilikuwa na hadhi...ukiwa form one ukirudi likizo kwenye msiba kijijini basi unakaa na wazee wa heshima eee wazee wastaafu na walimu na watumishi wa Serikali kama katibu kata / tarafa; Mratibu wa Elimu etc
Sasa hivi laah form one shule ya kata anachojua ni mauno ya nandi na singeli....
Duh unanikumbusha mbali. Shuleni kwetu tulifaulu watatu tu tena wavulana. Ukienda private unaonekana hauna kitu[emoji23][emoji23]Ni kweli ....kwa zamani shule za private secondary zilikua za wale ambao hawakufaulu sana kwenda shule za serikali