Mwaka 1999 kurudi nyuma ilikuwa ngumu sana kuchaguliwa shule ya Sekondari ya Serikali. Waliobahatika walijulikana kata nzima. Je, wewe ni mmoja wao?

Mwaka 1999 kurudi nyuma ilikuwa ngumu sana kuchaguliwa shule ya Sekondari ya Serikali. Waliobahatika walijulikana kata nzima. Je, wewe ni mmoja wao?

Mimi mwaka niliomaliza STD 7 hapo dar shule zilikuwa Ni hizi tu

Azania
Benjamin William mkapa
Dar es salaam sec
Kambangwa
Kisutu
Kibasila
Zanaki
Jangwani
Kiluvya
Chang'ombe
Forodhani
Tambaza ( a level tu)

Ukikosa hizi we umeshafeli [emoji1787][emoji1787]

Otherwise uende kipaji maalumu
 
Bila ile vita bila shaka tungekuwa mbali sana zaidi ya hapa
Dah umenikumbusha ile vita mwana,IDD amini alitishia atalipua bugando hosp, enzi hizo tunaishi mwanza ujue mwanza bugando ndo ilikuwa gorofa pekee.

Kila kaya iliamriwa kuchimba handaki nyuma ya nyumba,dah wiki mbili nzima familia yote tulikuwa tunalala shimoni.
 
ulikuwa mzembe sana chief, au ndo ulikuwa mtoto wa mama sana
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Uzembe nilianza kuupata baada ya kupona kufukuzwa shule kisa niliongoza mgomo nikipinga kupewa nyama moja moja nikiwa kidato cha pili.
R.i.p. mzee Mwamlima mpishi wa shule akafukuzwa baada ya kukutwa na nyama, unga na mafuta ya kupikia.
 
emoji1.png
emoji1.png
emoji1.png
emoji1.png
emoji1.png
emoji1.png
 
Tusisahau uwezo mkubwa sana wa walimu wa shule za msingi wa kipindi hicho. As far as I can remember there used to be exceptional teachers with an extraordinary ability, they didn't have huge education but they were the best at the subjects they were teaching.
 
Mzee mwaka gani hapa? Wakati wangu haikuwa Boyz, ilikuwa mchanganyiko. Maeneo ya mizizini tulikunjana sana huko karibia na printing Centre. Sina hakika kama Subiaco, cafeteria maarufu bado ipo, madeko kule chinga walizaa sana na wanafunzi kikazaliwa kizazi cha watoto tulichokuwa tunakiita top layers!! [emoji2957]
Nasubiri picha ya shule yangu Ndanda boys ingawa mimi sikumaliza 1999 kurudi nyuma!!
 
[emoji2] [emoji2] Au ukiachia gogo unaruka juu kabla hakijafika chini, vinginevyo choo cha chini unaoga wewe haha
[emoji23][emoji23], hivi kumbe hizi mambo zipo shule nyingi, nakumbuka kipindi nasoma kuna choo kimoja ulikuwa ukiingia unatundika nguo juu ya mti, vinginevyo ni hatari. Baada ya kupata huduma zinapitiliza kwenye povu[emoji23].
 
Walimu wala hawana kosa..shida mtaala wa serikali
Ndio mimi ni mmoja wao. Kati ya wanafunzi 90 tuliomaliza shule ya msingi Magereza Moshi tulichaguliwa wawili (2) tuu kwenda Form I Mawenzi Secondary School.

Najivunia sana elimu ya wakati ule kwani sijabebana na lundo la vitabu wala kuchoshwa na Tuition; walimu walijuma na kutupa NOTES na majaribio yaliyotuwezesha kuwa mahiri.

Elimu ya sasa hivi mtoto wa CLASS II anaandikia vitabu zaidi ya nane, daftari la Class work na Homework anakuwa na mzigo uliozidi umri wake; sijui hawa walimu huwa wanaokotwa wapi maana badala ya kuwapa watoto notes na homework, watoto wanatumia vitabu kama ndio notes.
 
Nakumbuka Sumbawanga mjini, mwaka 2001 kurudi nyuma, ikifika Desemba kabla ya Christmas majina ya waliopangiwa kwenda kidato cha kwanza, manispaa nzima yanabandikwa kwenye ubao wa matangazo wa soko kuu. Shule yangu tulikuwa 100 darsani, tuliotoboa tulikuwa 13 tu kwenda form one boarding nje ya Sumbawanga na wengine day ndani ya Sumbawanga mjini.
Mkuu, ndani ya Sumbawanga mjini kulikuwa na shule za secondary kama zipi?
 
Back
Top Bottom