Mwaka 2006 ni kama juzi tu ila ndio miaka 20 sasa, muda unakimbia kweli kweli

Mwaka 2006 ni kama juzi tu ila ndio miaka 20 sasa, muda unakimbia kweli kweli

Mwaka 2006 ni kama juzi tu wakuu. Ila ndio miaka 20 imepita,haya ni baadhi ya matukio yaliyotokea 2006 na sasa yana miaka 20.

Juma Akukweti akiwa Waziri anafariki baada ya kuanguka na ndege huko Mbeya baada ya kuwasagia kunguni wafanyabiashara ndogondogo.

Ubungo mataa kunapigwa tukio la ujambazi baada ya majambazi kujaribu kuiba pesa kwenye magari ya NMB. Lilikuwa tukio la aina yake, namkumbuka namna Kamanda Tibaigana alivyokuwa anatupa updates.

Kwenye uga wa michezo, mwanasoka bora Zinedine Zidane anampiga kichwa Marco Materazzi katika fainali ya Kombe la Dunia mwaka 2006. Tukio hilo linachukuliwa kama kumbukumbu ya michuano hiyo.
View attachment 3527169
Sio kichwa zidane alimpigwa mbichwaaa yule mchezaji mwehu..
 
Mwaka 2006:

Wema Sepetu anashinda taji la miss Tanzania, sasa hivi kashakuwa msimbe na mshangazi Jokate aliyemaliza nafasi ya juu katika mashindano hayo

Moshi William (TX William) wa kundi la Msondo Ngoma anakufa

Sadam Hussein anahukumiwa kifo

Twitter (X) yaanzishwa rasmi

Pluto inaondolewa kwenye orodha ya sayari kwa sababu ya kukosa sifa
 
Mwaka 2006 nilikua darasa la sita, jimboni kwa huyo Akukweti, wananchi walifurahia sana kifo chake,
Hii sijawahi kuisikia kama kuna waziri alidondoka na ndege. Nakumbuka ya Filikunjombe .

Natamani mtu aweke hiki kisa cha Akukweti inaonekana aliwasgia sana kunguni wafanyabiashara ndogo ndogo, wakamlilia Mungu akapita naye.
 
Back
Top Bottom