Mwaka huu 2023 umekupa funzo gani kubwa katika maisha yako?

Mwaka huu 2023 umekupa funzo gani kubwa katika maisha yako?

Mapenzi yanaweza kuwa mlango wa mafanikio katika maisha yako.
Ukipendwa pendeka acha nyodo wazuri ni wengi
 
Funzo la 2023…

Kutegemea wanasiasa ni kujinyima uwezo wa kufikiria
 
Kila mtu ana uhalisia pande mbili, ule upande anaouficha itatokezea tu, ni suala la muda.
Kuna mtu namfahamu kwa miaka 20 sasa, mwaka huu ndiyo nimeujua uhalisia wake kamili.
Na hapo Bado hujaujua uhalisia wake
 
Umenifunza kumsikiliza mke wangu.Hawa mafala wengine ni wakunywa nao beer tu na kuishi nao kwao akili.
 
Nimejifunzaa mtu mweusi Hana rafiki wa kweli wengi ni wanafiki,,jiamin wew mwenyew na maisha yakoo
 
  • Nzuri
Reactions: EEX
Wakuu,

Mwaka 2023 unakaribia kuisha, tumekutana na mambo mengi, ya kufunza, kukatisha tamaa, kutusogeza mbele ama kuturudisha nyuma, kutupa nguvu na kutufurahisha pia.

Katika mambo yote uliyokutana nayo, ni kipi kimekugusa sana kwa namna moja ama nyingine na kukufunza jambo?
1. Serikali haipo kwa Wanchi bali kwa ajili ya Viongozi= Baada ya SAlma Kikwete bila huruma kulazimisha wapewe mafao wakati wapo kazini na huku wapo kwenye ndoa na hata waliofiwa wanamiradhi ya waume zao, mabilioni ya fedha.

2. Viongozi wa Dini wapo kwaajili yao na si waumini waende Mbinguni,=Baada ya kukuta wale tunao waamini kila siku wanabaka watoto wetu tunowapeleka huko wakapate elimu, mbaya zaidi wanawageuza kinyume cha maumbile, dini za waarabu zimetuhribu na hatudhubutu kuzikataa.

3. Hatuna uchaguzi wala hakujawahi kuwa na uchaguzi= Maboksi ya kura yalikamatwa Kawe, yet Tume ikabariki na wasimamizi wa kimataifa wakabariki, ; COVID-19 ni laana kwa taifa lakini wameendelea kulindwa ili kamati za bunge zitimie.
 
Huu mwaka nimejifunza mengi,kikubwa do not trust anybody hata akiwa mtu wa karibu yako.Nalia ndani kwa ndani.Hakika nimetendwa haswa na mtu wa karibu haswa
Yaani acha kabisa Mimi ni binamu yangu niliempenda sana namshukuru Mungu kwa kunionesha mapema

Yule jamaa ni zaidi ya mnafiki shetani kabisa yule
 
Usiache ndoto zako kwa sababu ya changamoto. Jifunze kupambana nazo ili ndoto zako zitimie.

Ndugu wa damu anaweza kukupoteza kwa sekunde, hivyo uwe makini sana unapopanga mambo yako

Usitegemee mali ya familia kuwa itakuinua hasa mkiwa mmezaliwa wengi. Unaweza kupotezwa

Usidharau kazi maana zile kazi ambazo zinaonekana hazifai, hakika zina matunda mazuri sana

Jiwekeze kwenye vimradi vingi tofauti tofauti, hakika hufungua mwanga wa maisha
 
Huu mwaka nimejifunza kutoa zaidi kwa wenye uhitaji kushiriki zaidi kwenye jamii.

Kuna jamaa alinikutaga ferry miaka mitatu nyuma alinikuta nakunywa kahawa na washkaji bondeni tunastorika akanichomoa mimi pekeyangu akasogeza pembeni na akanieleza kiume kakwama hana nauli katoka jela wiki moja iliopita na akapewa dili kimbiji kuna kazi kaenda kakosa kazi akarudi mpaka ferry kwa miguu na ukitizama mazingira yake kweli kachoka.
sikutoa neno mdomoni niliingia mfukoni na akilini nikasema hela yeyote kubwa inayopanda basi nitampa bila kupepesa macho.
Nilipanda na 5k na 10k nikampa 10k bila kusita alishukuru sana nikamwambia kwa utani watu kama nyie mnatusuaga maisha ukizipata usinisahau ukija ferry ulizia 92 utanipata basi jamaa akaniaga nikampa na 200 ya kuvukia akaondoka na mm nikabaki sikumuambia mtu lile swala, Mungu mkubwa jamaa mwaka huu juzi tu kaja na lx namba E aloo alivyovimba nilishamsahau, mwamba akaniita 92 nikamfuata akaniambia zama ndani kaka nikulipe fadhila. Sikuamini kama ni yeye nikaweka pikipiki yangu vizuri nikazama ndani akaniuliza wapi naweza kunywa beer nikaenjoy nikamuelekeza tukaenda tukakaa alifunguka mengi sana magumu aliopitia stori zake ziliniumiza roho sana ila zilinipa nguvu ya kuendelea kupambana jamaa alipiga vyombo mpka pakafungwa akaomba nimrudishe kwake hapo ndipo nilipochoka mwamba anaishi mashavuni balaa akanipa maokoto tukapeana shukrani nikajigeuza kurudi ferry, njiani nilikua nawaza ila nikabaki kusema Mungu mkubwa leo sio sawa na jana.

Kwenye swala la kushiriki kwenye jamii mtaani kwangu kulikua na msiba basi mambo hayakua safi sana nilipofika kutoa pole mama wa ile nyumba aliniomba kama mwanae nimkopeshe 100k sikuwa na hicho kiwango nikamuomba wife lakini wakati napeleka hiyo hela nikajifunza msibani pale mambo ni mbovu hakuna hata chai kumepoa nilijiskia vibaya sana nikatoa ile hela nikampa nikaondoka kwenda kutafta angalau vitu kadhaa nivipeleke watumie nina rafiki yangu kwao wanatoa sana wa wenye uhitaji nikamnyookea mzee wake nikamueleza mazingira na nn nimefanya mpaka muda huo akanielewa akachukua ndinga yake tukaingia duka la jumla ambalo ni lake akachukua mchele sukari majani unga wa ngano amira na mazaga ya kupikia tukaenda msibani akawapa pole tukarudi kwake yule mzee akanikalisha chini akanipa somo ambalo bila kishiriki kwenye jamii kamwe nisingelipata alimwaga madini kwangu mimi niliona ni maneno ya dhahabu, msiba ulipoisha yule mama alikuja kusema asante nilikua na wife mama yule alilia sana akijua mimi ndiye nimetoa yote yale alinishukuru na kuniachia maneno yenye baraka nilipata amani sana kujua nimesaidia penye uhitaji. 2023 nimejifunza jambo na halitofutika maishani mwangu
Somo gani alikupa mzee?kama hutojali kushare...
 
Wakuu,

Mwaka 2023 unakaribia kuisha, tumekutana na mambo mengi, ya kufunza, kukatisha tamaa, kutusogeza mbele ama kuturudisha nyuma, kutupa nguvu na kutufurahisha pia.

Katika mambo yote uliyokutana nayo, ni kipi kimekugusa sana kwa namna moja ama nyingine na kukufunza jambo?
Hakuna taasisi au binadamu atakuja kukuokoa aua kukutetea. Maisha ni zawadi uliyopewa wewe pambania malengo yako.
 
Kukaa miezi sita bila nyeto au kugegeda kunawezekana ila uwe umefulia
Naomba ipingane na hii kidogo ukiwa na hela kiasi sawa. Pesa ikiwa nyingi unakuwa busy hata hamu na muda wa kufanya mapenzi huna. Unapata hamu ukiwa umepumzika nyumbani kuna kipindi unaweza ukahisi una matatizo.
 
nimejifunza yafwatayo:

1. Uhai wa binadamu ni kitu ambacho kinaweza kuisha wakati wowote, mahali popote, na katika mazingira yoyote yale. Tujitahidi kuishi vizuri na watu na kumtukuza Mungu.

2. Utu ni jambo adimu sikuizi, watu wanathamini mali na hela zaidi ya utu. Wengi waliotuzunguka kwenye maisha, wako karibu yetu kwasababu ya vitu tulivyonavyo na sio utu. Vitu hivyo vikiisha, wengi watatukimbia, hata simu zetu hawatapokea. Hayo yakitokea, tunapaswa kusali sana na kusonga mbele na maisha.

3. Kila mtu amekuja duniani kivyake na ataondoka duniani kivyake. Ishi maisha yako, usiangalie ya watu, ya watu hayakuhusu wala ya kwako hayawahusu.

4. Tujitahidi kufurahia maisha wakati wote, hatuishi mara mbili.
you nailed it
 
Back
Top Bottom