Mwaka huu 2023 umekupa funzo gani kubwa katika maisha yako?

Mwaka huu 2023 umekupa funzo gani kubwa katika maisha yako?

Usikate Tamaa, usichoke kutafuta, Bwana hakawii kuitimiza ahadi yake kwako na wala hachelewi....

Msuhukuru Mungu kwa kibali na zawadi ya Uhai na Afya alokujalia, Mara zote mtumainie yeye tu.

Nakuombea Roho Mtakatifu ahuishe na kufungua maskio ya kiroho moyoni mwako ili uwe tayari kuskia sauti ya wito wa Mungu katika maisha yako.

Bwana na akutendee muujiza wako kabla ya mwaka ujao kwisha.
Amen
Mkuu nashukuru
 
Experience

Ukimuomba M/Mungu mwaka huu anaweza akakujibu/akakupa baada ya miaka 10 na hata 15 anapoona yeye kuwa upo tayari kwa ulichokiomba kuwa upo vyema na utaweza kukitunza na kukilinda

Asante M/Mungu Kwa kila jambo nitaendelea kukutukuza daima kama nilivyofunzwa na walezi na wazazi wangu sitolalamika kama vilee sijawahi kukulalamikia kuwa hiki au kilee sina nitaendelea kukuomba msamaha hata kama sijakukosea

Unanipa vingi na kunilinda na vingi nazidi kupokea baraka kutoka kwako unavyonibariki ni vingi sanaa na vikubwa mno kwangu japo kwako ni vidogo zaidi ya mchanga , ukipenda utacha nimiliki hivi hivi tu nashukuru kwa vyote ukipenda tena niongeze M/Mungu mpendwa nitavipokea na kukushukuru daima na kuomba baraka zako uzidi kunitunzia, ameeni [emoji1431]
 
Nilijiwekea sheria na kanuni kuwa sitamkopesha mtu pesa zaidi ya elfu 20 hadi 30 mwisho. Na nimefanya hivo toka 2021 baada ya kupoteza pesa kwa kuamini watu.

Sasa mwezi wa 9 nikavunja mwiko huo kwa kumkopesha mtu laki 1, ambayo alipaswa kunilipa trh 25 Nov, 2023.

Leo ni wiki ya 3 sijaona hata mia zaidi ya uongo na sms ndefu, nimekwazika sana sana najilaumu kwa kuvunja sheria niliyojiwekea.

NB. KUNA WATU AMBAO NINA HISTORIA NAO NA ZAIDI YA MIAKA 6 HATUJAWAHI KUZURUMIANA HAWA TUNAKOPESHANA ZAIDI YA HIZO ILA MTU FROM NO WHERE SITARUDIA TENA NIMEKOMA.
 
nimejifunza yafwatayo:

1. Uhai wa binadamu ni kitu ambacho kinaweza kuisha wakati wowote, mahali popote, na katika mazingira yoyote yale. Tujitahidi kuishi vizuri na watu na kumtukuza Mungu.

2. Utu ni jambo adimu sikuizi, watu wanathamini mali na hela zaidi ya utu. Wengi waliotuzunguka kwenye maisha, wako karibu yetu kwasababu ya vitu tulivyonavyo na sio utu. Vitu hivyo vikiisha, wengi watatukimbia, hata simu zetu hawatapokea. Hayo yakitokea, tunapaswa kusali sana na kusonga mbele na maisha.

3. Kila mtu amekuja duniani kivyake na ataondoka duniani kivyake. Ishi maisha yako, usiangalie ya watu, ya watu hayakuhusu wala ya kwako hayawahusu.

4. Tujitahidi kufurahia maisha wakati wote, hatuishi mara mbili.
 
Jambo la maana nililolifanya nikuacha Tungi na baada ya kuacha Tungi nikagundua nilikuwa napoteza Hela nyingi Kwenye mbususu maana Tungi na mbususu n mate na ulimiii [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Wakuu,

Mwaka 2023 unakaribia kuisha, tumekutana na mambo mengi, ya kufunza, kukatisha tamaa, kutusogeza mbele ama kuturudisha nyuma, kutupa nguvu na kutufurahisha pia.

Katika mambo yote uliyokutana nayo, ni kipi kimekugusa sana kwa namna moja ama nyingine na kukufunza jambo?
1702463246258.png
 
Jambo la maana nililolifanya nikuacha Tungi na baada ya kuacha Tungi nikagundua nilikuwa napoteza Hela nyingi Kwenye mbususu maana Tungi na mbususu n mate na ulimiii [emoji23][emoji23][emoji23]
We jamaa acha tabia mbaya. Hutatoboa[emoji1787]
 
Kila mtu ana uhalisia pande mbili, ule upande anaouficha itatokezea tu, ni suala la muda.
Kuna mtu namfahamu kwa miaka 20 sasa, mwaka huu ndiyo nimeujua uhalisia wake kamili.
 
Back
Top Bottom