Mwaka huu 2023 umekupa funzo gani kubwa katika maisha yako?

Mwaka huu 2023 umekupa funzo gani kubwa katika maisha yako?

Mimi nimejifunza uvumilivu, kukabiliana na failures, dhihaka na kunyanyuka tena na kuanza upya.

Nimeamin katika kufanya kitu kidogo katika ubora mkubwa pale napokosa mafasi ya kufanya vitu vikubwa.

Nimeimarika katika kupenda kwa Akili na kujali familia kuliko kingine chochote.

“Siasa na Dini ni Biashara za watu, Tutafute hela tu"
Hakika!!
 
Ni mwaka wa mafunzo baada ya kupita katika bonde la mauti na ilibaki kidogo tuu nifike mwisho kama siyo simu ya yule dogo niliempokea kazini akitokea mtwala. Sasa nina mtazamo tofauti kabsa na dunia hii hakuna kitu kisichokua na mwisho kikubwa ni kuwa postive muda wote na ikimpendeza Mungu mwezi wa 12 nitaungana tena na familia japo kwa wiki mbili
 
Huu mwaka umenifanya niamini kila kitu kinawezekana... nimefanya mambo makubwa ambayo kwa umri wangu sikudhani kama naweza kufanya....Mafanikio ya kila mtu yapo mikononi mwake kwakweli, ni suala la kumwomba Mungu na kuamua kufanya
Tugawane hayo mafanikio.

Kwangu naona kama sijafanya makubwa , Malengo hayajatimia kwa 60%. Najipa moyo mda bado upo? NAAMINI MUNGU ANAWEZA KUTOA HATA KAMA YAMEBAKI MASAA KUMALIZA MWAKA.
 
Mtu akikuomba chakula mpatie kama unacho, njaa ni kitu kibaya sana, heshimu fedha hata kama ni ndogo kiasi gani,. Mtu akikuomba msaada kama unaweza kumsaidia msaidie, USIMJUDGE, kama anadanganya hiyo ni juu yake.

Mfanye Mungu wako kuwa wa kwanza kwenye kila utendalo, INALIPA.

Watu wengi wako karibu na wewe kwa sababu kuna namna wanafaidishwa na vitu fulani kutoka kwako, vikiondoka HUTOWAONA, jipange kisaikolojia na wala ISIKUUMIZE.


Familia ni kila kitu kwenye maisha, Asante 2023.
Hakika
 
Wakuu

Najua tuna mambo mengi yanayotusibu kwenye harakati za kila siku kutafuta mkate.

Leo ikiwa ni tarehe 13 December kuna kitu/vitu ulitamani kufanikisha lakini unaona vimeshindikana au hujafikia matarajio tupeane uzoefu.

Naamini tuna mengi ya kujifunza as long as bado tunaendelea kupambana
 
Back
Top Bottom