YE67NBE
JF-Expert Member
- Nov 30, 2015
- 15,155
- 36,337
Huu mwaka umenifunza kuwa.Wakuu,
Mwaka 2023 unakaribia kuisha, tumekutana na mambo mengi, ya kufunza, kukatisha tamaa, kutusogeza mbele ama kuturudisha nyuma, kutupa nguvu na kutufurahisha pia.
Katika mambo yote uliyokutana nayo, ni kipi kimekugusa sana kwa namna moja ama nyingine na kukufunza jambo?
1. Sio kila mwenye mvi / mtu mzima ana busara hivyo sio kila mtu mzima ni wa kuheshimiwa
2. Usimwamini mtu / ishi kwa machale
3. Pesa ni kama maji tu unaihitaji kwenye kila jambo.
4. Chaputa sio mbaya sana ila ngono halisi ni bora zaidi.
5. Usikubali kuonewa / kudharauliwa na mtu yeyote iwe kakuzidi hela au nguvu in short usiwe mnyonge.
6. Kuliko kufanya kitu nusu nusu ni bora usikifanye kabisa.
7. Never re friend a past enemy who was your friend.
8. Kuna umri ukifika usipoweza kujitegemea utaonekana kama mchawi tu hii nimeiona kabisa.
9. Kama huna value usitegemee kupata chochote chenye maana inshort. Hamna cha bure. Respect is EARNED.
10. nimejifunza kuwa marafiki wana impact sana kwenye tabia na maisha yetu iwe chanya au hasi ndio maana kuna msemo usemao "ndege wafananao huruka pamoja".
A. Ukitaka kuwa masikini kuwa na marafiki masikini
B. Ukitaka kuwa tajiri kuwa na marafiki matajiri.
Kimbembe nikuwa rafiki wa tajiri. 😃😃😃.
11. Muda mwingine drama ni tamu 😁😅😅.
Yangu ni hayo tu