Nimejifunza mengi sana ila kubwa nililojifunza ni kuwa ujumla wa mambo yote tunayoyafanya hapa duniani ni kwaajili ya kutafuta na kupata furaha, hakuna hata mmoja wetu anaefanya chochote kwa ajili ya kupata isiyo kuwa furaha , kamwe hakuna .
Nikajifunza pia furaha ni ndogo sana kuliko wanayo ihitaji, ni kwamba furaha inagombaniwa hali yenyewe ipo kwa kiasi kidogo, kwa hiyo wengi hawaipati na wanayo ipata hawadumu nayo maana inahitajika na wengi sana.
Nikajifunza pia ili uweze kupata furaha inabidi uwe na furaha pia, yaani toa furaha upate furaha, hi furaha uliyo nayo wewe haiwi furaha mpaka uitoe na wewe upewe ndio furaha huwa furaha, ila tu wewe inakupasa utoe kikubwa na chenye thamani ili upate walao furaha kidogo. Hii ni kwa sababu furaha inathamani kubwa hivyo inabidi utoe vya thamani ili uweze kupata furaha.
Nikahitinisha kwamba bila mtu mwenzangu siwezi kupata furaha, ili niweze kupata furaha inabidi ihusu mtu mwingine, sasa kwa vile kati ya viumbe vyote hakuna kiumbe chenye ubinafsi kama mwanadamu.
Hivyo USIJE KAMWE KUTARAJIA KUPATA FURAHA KUTOKA NJE YA WEWE.