Mwaka huu kutakuwa na njaa, heri ukose hela ila uwe na chakula ndani

Ndege joni enzi za jiwe alikuwa mmojwapo wa vijana wake wa mstari wa mbele humu jukwaani, siku hizi amepoa sana.
Sijapoa na mama tunamkubali kidizaini cha msingi tuna enjoy maisha
 
HAKUTA KUWA NA NJAA BALI MIGOGORO MINGI KAMA MAGONJWA,VITA,MAUAJI MENGI,VIFO VINGI ,MDORORO WA UCHUMI ,WATU WENGI KUFIRISIKA NA MAGEUZI YA DAMU. MPAKA 2028 NDIO MWISHO
 
mavuno mwaka huu yako juu sana hii imechagizwa na ruzuku aliyoiweka mama kwenye pembejeo

watanzania tafuteni mboga tuh unga mama kashawarahisishia wala hakuna shaka juu ya hili
 
Nalo neno.
 
Njaa ya wapi mbona huku tumevuna na kusaza?

Mavyakula hadi tunamwaga.

Labda huko kwenu ndo mna njaa!
 
Sembe sasa kilo ni alfu moja, natamani twende hivi hivi
Unatamani sembe kilo ibakie buku sio. Ndio maana nilionaga kilimo ni upuuzi. Yaan mtu unalima Kwa shida unaishia kulisha chakula watu mjini huku miaka nenda rudi mtu upo palepale. Kilimo nlikilima Kwa sababu nilikuwa chini ya wazazi sikuwa na jinsi. Ila sasahv sidanganyiki
 
Hakuna njaa mwaka huu labda ujao mahindi debe elf 7 ,mchele kilo 1000
 
Tafuta Hela mkuu, unga si AKIBA pesa ndio akiba ya Kila kitu. Mfano mtoto akiumwa hapo uwezi mpelekea docta unga na Mchele ampe mtoto huduma bali atataka pesa.. Narudiaa tafutaa pesaaaa sanaaaaa..
Mkuu sisi kikwetukwetu kutibiwa in exchange of food products ni Jambo la kawaida sana!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…