Mkono Mmoja
JF-Expert Member
- Jan 26, 2019
- 3,359
- 6,568
Ahlan wa sahalan.
Kwa hali aliyofikia beki wa kushoto wa Simba , tshabalala ni wazi kuwa haendani tena na falsafa ya mpira wa kasi wa Simba.
Ikiwa simba inahitaji kufika mbali kimataifa basi wanatakiwa watafute mabeki wapya kushoto na kulia ili kuifanya falsafa ya mwalimu Fadlu kuwa na nguvu na imara.
Leo Djibril Sillah kamchosha sana Shabalala kiasi kwamba alishakata moto mapema kuanzia dakika ya 60. Kocha wa Azam kwa kulitambua hili akaamua azidi kumpeleke watu wenye kasi upande wake. Mara nyingi Shabalala alikuwa nje ya position yake na waliokuwa wakimfichia makosa ni Che Malone aliyeumia na baadae Karaboue Chamouh.
Lauti kama Azam wangetumia sana madhaifu ya upande wa shabalala basi wangeiadhibu sana Simba kwenye mechi ya leo.
Wito wangu kww uongozi wa Simba ni kuhakikisha kuwa wanafanya mapinduzi ya usajili katika nafasi ya beki wa kulia na Kushoto. Viongozi waache siasa za kuangalia majina badala yake walete kweli watu wa soka.
Shabalala madhaifu yajr makubwa yapo katika kukaba na kushambulia. Winga anaposhambulia yeye huwa nyuma na timu inaposhambuliwa haonekani katika nafasi yake. Kifupi anakabia kwa macho pia hana uwezo wa kupiga Crosses za maana.
Soma Pia: FT | Simba SC 2-2 Azam FC | NBC Premier League | Benjamin Mkapa | 24 Februari, 2025
Viongozi iliangalie hili kwa jicho yakinifu. Shabalala na mzee mwenzie Kapombe kinachoendelea kuwabakisha Simba ni uwezo wao wa nje ya uwanja kwenye kuwapiga misumari wachezaji wanaosajiliwa kuja kushindana nao katika nafasi zao. Ikiwa Simba inahitaji mapinduzi ya kweli basi ni vyema kuachana na wachezaji hawa na kutafuta wachezaji wenye uwezo mkubwa.