Angepelekwa mahakamani ashitakiwe kama kafanya jinai.
Fanyeni hayo kama kweli nyie mnatawala kwa katiba na Sheria kama mnavyojitapa.
Aliyekuwa Meja wa Jeshi la Marekani, Nidal Hasan, anatarajiwa kutekelezewa adhabu ya kifo kwa kikosi cha risasi Desemba 3, 2026, katika Kambi ya Fort Hood, Texas.
Hasan alihukumiwa kifo baada ya kumpiga risasi na kuwaua wanajeshi 13 wa Marekani na kuwajeruhi wengine 32 katika shambulio lililotokea Fort Hood, Texas, Novemba 5, 2009.
Msemaji wa Pentagon, Sean Parnell, amesema Waziri wa Ulinzi wa Marekani, Pete Hegseth, alitoa pendekezo la utekelezaji huo, ambalo liliidhinishwa na Rais Donald Trump.
Utekelezaji huo ukifanyika kama ulivyopangwa, utakuwa wa kwanza katika Jeshi la Marekani kwa kutumia kikosi cha risasi kwa zaidi ya miaka 60, tangu kipindi cha baada ya Vita vya Pili vya Dunia.
Hasan, ambaye alikuwa daktari wa magonjwa ya akili katika Jeshi la Marekani, alikiri wakati wa kesi yake ya kijeshi mwaka 2013 kuwa ndiye aliyefanya shambulio hilo.
Katika kesi hiyo, alisema aliamini kuwa alikuwa akiwalinda Waislamu pamoja na Taliban nchini Afghanistan.
Shambulio hilo la mwaka 2009 lilikuwa miongoni mwa mashambulio mabaya zaidi yasiyohusisha mapigano kuwahi kutokea katika kituo cha kijeshi cha Marekani.