Sang'udi
JF-Expert Member
- May 16, 2016
- 9,138
- 22,236
Mhashamu Baba Askofu Mkuu Renatus Nkwande wa Jimbo Kuu Katoliki la Mwanza anawaalika waamini na watu wote wenye mapenzi mema katika adhimisho la Misa Takatifu ya kumuombea pumziko la milele mbinguni Hayati John Pombe Joseph Magufuli.
Misa hii takatifu itafanyika Jumapili ya Machi 20 katika viwanja vya madhabahu ya Bikira Maria Malkia wa Kawekamo kuanzia saa nne kamili asubuhi.
Aidha, Mhashamu Baba Askofu Mkuu Renatus Nkwande anatukumbusha kumuenzi Hayati Magufuli kwa kuwa wazalendo wa kweli, kudumisha amani, undugu na maendeleo ya taifa kwa ujumla.
Hayati Magufuli apumzike kwa amani mbinguni, Amina.