Mwaka mmoja bila Magufuli: Jimbo Kuu Katoliki Mwanza kuongoza Misa ya maombezi yake

Mwaka mmoja bila Magufuli: Jimbo Kuu Katoliki Mwanza kuongoza Misa ya maombezi yake

Je wewe unajua kabla ya kifo chake aliongea/ aliomba nini kwa Mungu wake?!
Maandiko yanasema.. “Your ways are not my ways”. Isaiah 55: 8-9
Hajui lolote, amejawa na chuki na uchawi.
 
Mhashamu Baba Askofu Mkuu Renatus Nkwande wa Jimbo Kuu Katoliki la Mwanza anawaalika waamini na watu wote wenye mapenzi mema katika adhimisho la Misa Takatifu ya kumuombea pumziko la milele mbinguni Hayati John Pombe Joseph Magufuli.

Misa hii takatifu itafanyika Jumapili ya Machi 20 katika viwanja vya madhabahu ya Bikira Maria Malkia wa Kawekamo kuanzia saa nne kamili asubuhi. Aidha, Mhashamu Baba Askofu Mkuu Renatus Nkwande anatukumbusha kumuenzi Hayati Magufuli kwa kuwa Wazalendo wa kweli, kudumisha amani, undugu na maendeleo ya taifa kwa ujumla.

Hayati Magufuli apumzike kwa amani mbinguni.

View attachment 2147385
Alikuwa MUONGO ,makampuni ya serikali TTCL/ATCL yalifannya sanaa za maonesho KUTOA GAWIO kwa serikali ,wakati yalikuwa yanajiendesha kea hasara.

Lengo ni kuwahadaa WATANZANIA wajinga ambao hawana CRITICAL mind.

Mwishoni ikabainika katika report ya CAG kuwa mashirika hayo ni Yalioparate kwa hasara.

Kifupi MAGUFULI ALIKUWA SAWASAWA NA (Mfalme JUHA)
 
Mnamuombea nani?Mnamuombea maji ya kunywa au nini?Mmekosa kazi za kufanya.Nasikitika kwamba naye alikuwa mkatoliki.Nkt!
Tunamuombea Rais bora kabisa kuwahi kutokea nchini mwetu ili aendelee kula raha mbinguni. Unateseka ukiwa wapi? 😁
 
Aliomba msamaha Lissu ?.
Aliomba msamaha aliowapora fedha ?.
Aliomba msamaha waTZ kwa kupora uchaguzi ?.
Aliomba msamahaa wazazi wa Ben ?.
Aliomba msamahaa waTZ kwa kuharibu uchumi ?.
Aliomba msamahaa waTZ kwa kuharibu mahusiano ya kimataifa hasa nchi jirani ?.

Hicho kiherehere cha Roman Catholic kinatoka wapi zaidi ya kudumaza waKristo kiimani na hata namna bora ya kutumia akili zao.

Kifupi hiyo misa ni chukizo mbele ya Mungu.
Huwa mnaonesha chuki ilivyo mbaya na inavyoua taratibu.

Amuombe msamaha Lissu, sijui wazazi wa Ben kwa lipi? Hebu tuwekee uthibitisho hapa.

Aharibu uchumi halafu hao mabeberu wenu wafanya declaration kuwa tupo uchumi wa kati!!!

Uhusiano gani wa kimataifa, huu wa kuwauza Wamasai, au huu wa kuwauzia Wachina bandari na kuwapa mamlaka ya kuongoza uchumi wa nchi yetu?

Punguzeni chuki, itawaua.
 
mie naangaliaga hizi post nawazaga sana kuhusu binadamu aliyezaliwa na binadamu mwenzie! nyie mnaoombea kwa kudanganya watu ili mpate hela mjenge mahekalu na starehe kibao wakati waumini wenu wanashinda njaa kwa kuamini mnawaombea utajiri mlaaniwe
Wao Injili yao ni utajiri na kuondoa mapepo tu. Hawajui hata maana ya msalaba.
 
Swali kabla hujaswaliwa
Nina hakika Mungu anatuangalia anatafakari kuna mahali alikosea kutuumba wa TZ, tuna unafiki mkubwa sana kuanzia makasisi na waumini.

Lakini ashukuriwe Mungu hajawahi kutenda kwa kufuata unafiki wetu
Wala hajawahi kumuacha mtu muovu astawi kwa kitambo sana
Swali kabla hujaswaliwa... Maana yake utaswaliwa, au haujui hata ulichokiandika!? 😁
 
Nitakukumbuka rais wangu..
Nilikupigia kula mimi
Nilipenda biti zako
Nilipenda utani wako mf. Mpanuliwe wapi?😂😂
Muda wa kucheka tulicheka muda wa kazi ilikuwa kazi kweli.
Napenda na mimi siku 1 nije kuwa kama wewe tena zaidi ya wewe.

Ulikuwa na HURUMA ! Huruma! Tena Huruma ya kweli. Nakujua tangu ukiwa mbunge.

Chema hakidumu hakika chema hakidumu
Familia yako mola aendelee kuifanyia wepesi.
Daaaah....
Magufuli alikuwa peace sana kwa Watanzania wazalendo, na aliwapenda kwa dhati kabisa. Alikuwa mtetezi wa kweli wa wanyonge.
 
Baada ya hapo akazuia wanaCCM wote kwenda kumuona Lissu, akamuamrisha na Ndugai asimpe mafao yake, jamaa lilikuwa nafiki na katili sana
Huyu hakuwa Mwanaccm

images.jpeg
 
1.MKATILI
Kama ulikuwa katili kwa Watanzania, kama ulikuwa unawaonea Watanzania wanyonge, kama ulikuwa fisadi, kama ulikuwa kibaraka wa mabeberu ni lazima ulikutana na moto wa Magufuli.

Hatukushangai. Magufuli aliwapenda na kuwatetea Watanzania walioonewa. Nasi Watanzania wengi tunampenda na tunazidi kumuombea apumzike kwa amani mbinguni.

2.WATU WAMEUWAWA NA KUPOTEA KATIKA UTAWALA WAKE
Watu walikuwa wanapotea kabla yake na wanapotea baada yake, hiyo hata siyo hoja. Hata hivyo kipindi cha Magufuli wanaopotea walipungua sana.

4.AMELETA OMBWE LA AJIRA KWA KUTOAJILI MUDA MREFU.
Hakuna Rais ametengeneza ajira nyingi kama Magufuli. Wakati wake Watanzania wengi sana walijiajiri.

5.ALIKUWA NI MTU MWENYE VISASI KWA WALIOMKOSOA
Hakuna Rais aliyekosolewa kama Magufuli. Akina Lissu walikuwa hadi wanamtukana (Refer kabla, wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu 2020) lakini wapo wanadunda.

Ninafikiri upunguze chuki, itakusaidia kuwa na maisha marefu.
 
Kwa hiyo alikuwa anamkubali kwa vitendo vyake? Amesahau alivyomdhalilisha Askofu mwenzake kwa kumuweka katika kundi la wahamiaji haramu? Amesahau yaliyompata Tundu Lisu?
Kwani kama kuna mashaka kwenye uraia wa mtu na serikali ikaamua ku-clear hayo mashaka kuna shida gani?

Tundu Lissu alipatwa na nini?
 
Back
Top Bottom