Tumwombee kama tunavyowaombea wakosefu wengine, lakini siyo kwa sababu alikuwa kiongozi mzuri.
Kiuongpzi, marehemu alikuwa kiongozi mbaya kuliko yeyote ambaye tuliwahi kuwa naye. Alikuwa kiongozi katili kwa kiwango ambacho hakijawahi kushuhudiwa, mdhulumaji, aliyejaa chuki na upendeleo, n.k.
Tunapomwombea huruma ya Mungu, tusisahau kuliombea Taifa letu ili isitokee wakati Mungu wetu akaruhusu Taifa lipate kiongozi mbaya wa kiwango cha marehemu, kiongozi muuaji, mtesaji, mdhulumaji, asiyejali haki wala uhuru wa binadamu wenzake.
Mungu azidi kuwajalia moyo subira, unyenyekevu wale wote waliopotelewa na ndugu zao (Ben Sanane, Azory Gwanda, Kinguye, n.k.). Mungu azidi kuwajalia moyo wa msamaha wale waliopatwa na madhira makubwa yaliyosababishwa na marehemu (Lisu, Rugemarila, Deo, na wengine wengi waliorundikwa ndani kwa kesi za kutengeneza ili kuwakomoa).