Mwaka mmoja bila Magufuli: Jimbo Kuu Katoliki Mwanza kuongoza Misa ya maombezi yake

Huu ni unafiki wa wasukuma, mbona hawawaombei waliouawa na Magufuli au kwa maelekezo yake?
 
Mlizimia mwenge Chattle siku ya kumbuziki ya kifo cha Mwl .Nyerere kwanini misa kitaifa msifanyie chattle huko?

Mmemsaliti dikteta aliyepeleka hadi route ya ATCL chattle.
Hiyo siyo ya Kitaifa, ni ya Kanisa Kuu Mahalia la Mwanza.
 
Waliouwawa mtwara na Tanga alikuwa JPM? Acha chuki na JPM mzandiki wewe
Hata akina Daudi Mwangosi, Dr. Ulimboka, wale raia watatu wa maandamano ya CHADEMA Arusha na wengineo wengi ilikuwa wakati wa Magufuli.
 
Umekosa kazi ya kufanya. Unaombea wafu? Ni sawa na kuombea jiwe. Wafu hawasikii chochote na hesabu zao zimefungwa kwa matendo waliyotenda wakiwa hai (km vile risasi kwa Lissu, kifo cha Ben Saane, pesa za maduka ya kubadilisha fedha za kigeni, nk.). Tengeneza maisha yako ya baadae ya kiroho ukiwa hai leo. Ukishakufa hesabu yako inafungwa.
Ufisadi siyo mzuri mkuu.

Karibu Kawekamo tumuombee kipenzi cha Watanzania wengi.
 
Ilikuwa ni mchaka mchaka aliselema...
Uchumi wa nchi ulikua kwa kasi sana.

Sasa hivi tunakopa, tunaomba misaada na wameongeza kodi na tozo za kutosha...

Lakini hakuna mradi mkubwa unaoendelea vizuri, hakuna ajira, hakuna nidhamu maofisini, n.k.

Mpaka unajiuliza kama tuna uongozi.
 
Unaifunga wewe?

Tuwekee credible source ya mafundisho yako haya
 
Yesu aliteswa na kufa kwa ajili yakukomboa ulimwengu baada ya siku tatu akafufuka zile siku alienda kuwakomboa walioko toharani waliokufa na wanaopata mateso.lazima tumwombee mpendwa wetu aende kuume kwa Baba aminaaaa
 
Tunaombea roho yake sio mwili. Mwili upo chato umetuzwa ila roho bado inaishi ndio tunaiombea ikapumzishwe mahala pema peponi aminaaa.mwili unaombewa siku yakupumzishwa kwenye nyuma ya milele sasa tunadeal na roho ambayo bado inaishi
(
 
Utaomba sana. Hesabu yake ilikwishafungwa 17 March 2021. Alikuwa na miaka 61 ya kuweka mambo yake sawa na Mungu/Yesu. Usimlaumu Mungu/Yesu bure. Miaka 61 inatosha kutubu, kumkiri Yesu na kuishi vizuri na binadamu wenzio. Wafu hawawezi kutubu. Hawasikii ama kuelewa chochote. Ecclesiastics 9:5. Tubu dhambi leo na umfuate Yesu Kristo. Ukifa basi. Hakuna cha kuombewa ama kutokuombewa.
Yesu aliteswa na kufa kwa ajili yakukomboa ulimwengu baada ya siku tatu akafufuka zile siku alienda kuwakomboa walioko toharani waliokufa na wanaopata mateso.lazima tumwombee mpendwa wetu aende kuume kwa Baba aminaaaa
 
Ingekuwa na maana gani kuishi maisha ya toba sasa? Yaani uue watu, uwafunge maiti kwenye viroba, utese watu... usitubu wakati uko hai, halafu ukifa ndugu zako wanakuombea unakuwa mtakatifu huko kifoni, unaepuka hukumu ya Mungu!!?? Nani angekwenda huko jehanamu sasa? Na maana ya kutubu na kuishi maisha ya Kristo wakati uko hai ingetoka wapi sasa!! Tumia ubongo wako vizuri (Ecclesiastes 9:5).
Tunaombea roho yake sio mwili. Mwili upo chato umetuzwa ila roho bado inaishi ndio tunaiombea ikapumzishwe mahala pema peponi aminaaa.mwili unaombewa siku yakupumzishwa kwenye nyuma ya milele sasa tunadeal na roho ambayo bado inaishi
(
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…