Watu wa Dubai kuanzia Ijumaa, Jumamosi, Jumapili ilikuwa ingia toka kwangu.
Nilifanya kheri ya kuwakaribisha na kuwachinjia kondoo siku ya Ijumaa, nikawapiga na pilau la Dar la kufunikia kwa kaa juu, sharti kwa makuchambari na mapilipili ya kusagam ya kupika, Matunda organic, fresh ya shamba, pilipili kichaa za kusaga za kufa mtu, kila anaeila lazima atokwe kmasi na chozi.
Waaranu wakapenda sana tena sana, wanasema hii pilau nzuri kuliko ya Indonesia. Ma frsh juice ya malimao nimetupia mbegu za komamanga za kinyeji ndani, pembeni nikawawekea na juisi la mabungo nimelimwagia juisi ya pilipili mbuzi kwa mbali, kupata flavour na muwasho kwa mbaaali. Nikaikoroha kwa sukari guru,nikaichuja vizuri, tupia maji yatangawizi kidogo, ukaju kwa mbali, vihiliki vya kusaga vya ushikaji.
Dah! Mwenyezi Mungu mkubwa, mbona siku ya pili wameziuliza juisi za jana, wamekuja na makondoo yameshapikwa kutoka mahotelini huko, kimekuja kiakigari (hiace van) kizima cha catering wanalipa fadhila, rohoni mwangu nasema nyie Waarabiu hiyo mihela mlionunuwa hivyo vutu si mngenipa mimi.
Mungu si Athumani, ulifikiri walikuwa wanausikia moyo wangu, mmoja akasema twede Dubai tukanzishe biashaara ya juisi na hizi sauce za jana tu. Nikawaambia tatizo nini spices zingine zipo seasonal, wakanambia usijali, twakati wa season tutanunuwa kwa wingi mpaka za season nyingine. Nikawaambia game. Nizubae tena? Hivi nangoja warudi, lwo wameenda selous kutaza wanyama wataka huko siku tatu. Vibosile vinakula bata tu.
Kuondoka bwana wameona haya kunipa mimi mshiko si wakampa kibahasha baba mwenye nyumba. Alivyokuja nachondani, akanambia siamini na sijuwi kina nini, kufunguwa ndanu. Myamwezi mtupu ananukia upya khamsa khams a mbili. Utajaza mwenyewe. Nikamwachia mwenye nyumba kifurushi kimoja cha khamsa, kibindoni kingine cha khamsa.
mzee si ikamtoka "hawa ndiyo wageni wakuwapokea..". NIkamchomekea waoze wajukuu zako, akasema hata leo nawaachsha kusoma, wangoje nini tena, watasoma hukohuko kwa waume zao!
Hao jamani ni indurect za DP World hizo ni wagnya biashara tu wwa Dubai wapo holiday season wakaona waje kutenbelea Tanzania, maana huko kwao, huwa wanfata Mlame wao anafanya nini wapi, basi na wao ndiyo hukohuko.
Nikaona pesa si mchezo jamani.
DP World Hoyee.