Mwaka wa kumi huu au zaidi umeajiriwa (unatumwa tumwa tu); je, ni kitu gani kinakufanya usijiajiri?

Forbes ishacover hadi kina Elizabeth Holmes, Charlie Javice, Sam Bankman etc. unajua walipo?

CEOs wa apple, Google, Microsoft ni waajiriwa nenda kawaambie ajira ni mbaya na uliza walikua Hapo miaka mingapi Kabla ya kuwa CEOs. BTW nao washakua on Forbes
Kuna ajira na ajira. Kuna watu wameajiriwa na wanakula life. Halafu kila mtu akijiajiri nani ataajiriwa sasa
 
Tunaamini elimu tunayoipata huko vyuoni na mashuleni, inatupa uhuru wa kufanya maamuzi sahihi katika uzalishaji mali pamoja na kujitegemea.

Tulitegemea ujuzi na elimu ulioipata huko duniani n.k iwe chachu ya wewe kujijenga na kuanzisha na kumiliki kampuni, taasisi, au kiwanda ili pia iweze kutoa ajira kwa wengine.

Mtaji kwako sio tatizo, kwa sababu umeshaajiriwa kwa miaka mingi na una sifa zote za kukopa; Swali, kwanini unashindwa kujiajiri?

Tatizo ni nini?​
Mkuu Equation X,
Elimu yetu haituandai kuikabili dunia halisi, embu fikiria kati ya wazazi 50 wanakuwa wakiwaambia watoto kwamba soma kwa bidii, upate alama za juu na baada ya hapo upate kazi nzuri yenye mshahara mnono.
Tunakuwa tukiaminishwa hivyo na kiuhalisia mambo yanakuwa tofauti.

Elimu misingi yake ni kwamba shuleni ukifanya makosa wewe huna akili na hicho ndicho kipimo cha mtu anavyopimwa, lakini katika dunia halisi kadri unavyofanya makosa ndio kadri unavyojifunza zaidi.

Tatizo ni blue print ambazo tulizonazo wengi wetu, ndio maana mtu yupo radhi kuhangaika na vyeti wakati anaweza akafungua sehemu ya kuuza mishkaki na ikamtengenezea pesa kuliko kazi anayohangaikia! Very strange.

Mifumo ya elimu inatengeneza watu kwa ajili ya kuajiriwai, tukiwa chuo stori nyingi ni nitafanya kazi sehemu fulani na si kufikiri kuajriwa.
 
Hivi unajua kuna watu by nature tuu, anapenda Kuajiriwa? Yaani yeye kukaa ofisini iwe za uma/binafsi/taasisi kuhudumia watu hilo jambo kwake ni tosha kabisa..
Nazungumzia mtu ambaye hata ukae nae miaka 7, hutosikia ana wazo la kufungua biashara...
Na huwezi ukamlaumu ameridhika na ni maisha yake, watu wa namna hii haono kazi anayofanya kama kwake ni shida, Lakini pia wengi wanaridhika sana.
 
Elimi Ughaibuni na elimi ya hapa nyumbani ni sawa kabisa......tofauti ni (infrastructures)tu....by the way tunasoma Mfumo wa Cambridge na Oxford....hatuna elimu yetu wenyewe
Sasa, tatizo ni nini? au vyakula tunavyokula ndio vinadumaza akili zetu?
 
Je tukienda kupata elimu ughaibuni, inaweza ikatusaidia katika kujiajiri?
Bila shaka ,Ila inategemeana na Uko ughaibuni nchi gani, kama ni Nchi kama USA exposure tu itakufanya ubadilike kimtazamo , faida kubwa pia elimu ya nchi zilizoendelea zinamjengea msomi kuelewa thamani yake , Ukija bongo mhitimu ndio anampa thamani kubwa muajiri kupita kiasi na kuishusha thamani yake na hapo ndio chanzo cha kupata mshahara mdogo na ajira kuonekana haifai.
All in all sio wote wanaweza kujiajiri hata kama usomee nje , halafu ieleweke kujiajiri sio lazima kuwa mfanya biashara moja kwa moja.
 
Jibu ni Moja tu..sisi ni WAVIVU..kijiajir kunahitaji watu wachapakazi ndio maana hata waajir wetu wanajua sisi mpk tusimamiwe hasa ndio wapate faida..
Ingekuwa sio sheria, kampuni nyingi zingekuwa na wachina / wahindi..
 
Mkuu Equation X,
Elimu yetu haituandai kuikabili dunia halisi, embu fikiria kati ya wazazi 50 wanakuwa wakiwaambia watoto kwamba soma kwa bidii, upate alama za juu na baada ya hapo upate kazi nzuri yenye mshahara mnono.
Tunakuwa tukiaminishwa hivyo na kiuhalisia mambo yanakuwa tofauti.

Elimu misingi yake ni kwamba shuleni ukifanya makosa wewe huna akili na hicho ndicho kipimo cha mtu anavyopimwa, lakini katika dunia halisi kadri unavyofanya makosa ndio kadri unavyojifunza zaidi.

Tatizo ni blue print ambazo tulizonazo wengi wetu, ndio maana mtu yupo radhi kuhangaika na vyeti wakati anaweza akafungua sehemu ya kuuza mishkaki na ikamtengenezea pesa kuliko kazi anayohangaikia! Very strange.

Mifumo ya elimu inatengeneza watu kwa ajili ya kujiajiri, tukiwa chuo stori nyingi ni nitafanya kazi sehemu fulani na si kufikiri kuajriwa.
Uko sahihi, mfano; watoto waliotoka kwenye familia zenye viwanda, huwa hawaajiriwi, wataenda nje watapata elimu, na baadaye wanakuja kusimamia viwanda vilivyoanzishwa na watangulizi wao.
 
Hivi unajua kuna watu by nature tuu, anapenda Kuajiriwa? Yaani yeye kukaa ofisini iwe za uma/binafsi/taasisi kuhudumia watu hilo jambo kwake ni tosha kabisa..
Nazungumzia mtu ambaye hata ukae nae miaka 7, hutosikia ana wazo la kufungua biashara...
Na huwezi ukamlaumu ameridhika na ni maisha yake, watu wa namna hii haono kazi anayofanya kama kwake ni shida, Lakini pia wengi wanaridhika sana.
Inawezekana ndio amezaliwa hivyo (biological factor); na hii inatokana na vyakula pamoja na vinywaji alivyokuwa akitumia mzazi kabla ya mtoto kuzaliwa
 
Nina rafiki yangu ni Lecture, ana Salary iliyoshiba, Anafundisha vyuo vi 3..

Huyu jamaaa Suala la biashara ni mtambuka,
Nimefahamiana naye miaka 14, Sijawahi msikia akizungumzia biashara, mpka siku nikamuuliza hivi wewe hata kimoyo moyo ushawaza kufanya biashara..
Akacheka akasema achana na hayo mambo, Ikaisha hio,

yaani hana hio hobby, Sio kwasababu anamshara mzuri,
Kuanzia kipindi ana hustle na Ajira anakamshahara kakubembeleza kafika mwisho wa mwezi hataki hizo mambo..
Akapata mke mpenda biashara, Mke kambembeleza wee ampe mtaji, Jamaa kagoma Kamtafutia Shavu sehmu flani hivi anapiga kazi.

Biashara sio kwa kila mtu.
 
Watu wanaona changamoto ya ajira sababu gharama za maisha zipo juu kuliko kipato cha mwezi. Na maokoto hakuna kabisa.

Kimsingi tazama watu wanaofanya taasisi za mbele utaona namna ambavyo maslahi yao yapo vema na hawahangaiki na hizi shida ndogo ndogo wametulia ila sasa hawa ambao wanalipwa mishahara below standards of living.
 
Mkuu Equation,
Sidhani kama upo uhusiano wa mtu kupendwa kuajiriwa sababu tu ni nature au vinywaji.

Kitu kikubwa mkuu wengi hatupendi kutoka katika “Comfort zone”

Kutoka katika hali ya kustarehe au sehemu tuliyoizoea huwa ni mtiti sana, ndio maana kuna kuwa hakuna mabadiliko.
Huenda inasabishwa na kuogopa sehemu nyingine,
Kupenda kuajiriwa by nature nafikkri ni mazingira ya mtoto anapokulia na nini anCholishwa akilini mwake tangu udogo mpaka ukubwa wake.

Familia nyingi watoto wazazi waliokulia katika biashara lazima wataangukia humo, kadhalika mtoto atakayekulia kumuona baba ni mjeshi, mama ni mjeshi kuna asilimia kubwa mtoto akaangukia humo japo si wote.
 
Jibu ni Moja tu..sisi ni WAVIVU..kijiajir kunahitaji watu wachapakazi ndio maana hata waajir wetu wanajua sisi mpk tusimamiwe hasa ndio wapate faida..
Ingekuwa sio sheria, kampuni nyingi zingekuwa na wachina / wahindi..
Uko sahihi; jibu sahihi ni uvivu, wengi tunataka fedha za mteremko, ndio maana fitna kwenye ajira zinakuwa ni nyingi
 
Nina rafiki yangu ni Lecture, ana Salary iliyoshiba, Anafundisha vyuo vi 3..

Huyu jamaaa Suala la biashara ni mtambuka,
Nimefahamiana naye miaka 14, Sijawahi msikia akizungumzia biashara, mpka siku nikamuuliza hivi wewe hata kimoyo moyo ushawaza kufanya biashara..
Akacheka akasema achana na hayo mambo, Ikaisha hio,

yaani hana hio hobby, Sio kwasababu anamshara mzuri,
Kuanzia kipindi ana hustle na Ajira anakamshahara kakubembeleza kafika mwisho wa mwezi hataki hizo mambo..
Akapata mke mpenda biashara, Mke kambembeleza wee ampe mtaji, Jamaa kagoma Kamtafutia Shavu sehmu flani hivi anapiga kazi.

Biashara sio kwa kila mtu.
Alafu ukute chuoni ndio anafundisha 'Entrepreneurship/ business issues'
 
Watu wanaona changamoto ya ajira sababu gharama za maisha zipo juu kuliko kipato cha mwezi. Na maokoto hakuna kabisa.

Kimsingi tazama watu wanaofanya taasisi za mbele utaona namna ambavyo maslahi yao yapo vema na hawahangaiki na hizi shida ndogo ndogo wametulia ila sasa hawa ambao wanalipwa mishahara below standards of living.
Uko sahihi,kuna huyu mtu anaitwa 'entrepreneur' huyu ata kwa mwezi umpe milioni 100, hutomuajiri?
 
Back
Top Bottom