Kama kweli Israel ilikuwa inalenga kupambana na Hamas pekee, ingeweka njia salama kwa raia wa Gaza kuondoka. Lakini badala yake, ilifunga mipaka yote, ikazuia watu kutoka, kisha ikawashambulia bila kujali. Hilo ni kosa la kisheria na kimaadili. Huwezi kuhalalisha mauaji ya maelfu ya watoto kwa hoja ya ‘adui alikuwa karibu nao,’ wakati uliwanyima nafasi ya kujiokoa. Gaza si uwanja wa vita wa wazi ni gereza la wazi. Tusitafute sababu za kutakasa unyama...
Kuua mtoto eti kwa sababu mpiganaji anajificha karibu ni sawa na kusema "kila mtu aliye karibu na adui anaweza kuuawa", jambo ambalo ni la kikatili na halikubaliki kiutu...
Kingine tofautisha familia ya kawaida mitaani na taifa lenye jeshi rasmi, silaha za kisasa, na wajibu wa kutii sheria za kimataifa.
Kumbuka
Sheria za vita hazitegemei kila raia wa kawaida kuzijua, bali zinawalenga serikali, Majeshi rasmi na viongozi wa kijeshi na wa kisiasa..
Israel ina jeshi lililobobea, wanasheria wa kijeshi, teknolojia ya hali ya juu hii haipaswi kuchukuliwa kama mtu wa kawaida anayefaanya maamuzi kwa hisia au hasira...
Hata polisi wakienda kumkamata mhalifu akiwa nyumbani kwa watoto, hawaruhusiwi kuwapiga watoto ambao hawajui chochote kinachoendelea..
Hata juzi hapa watu wanaodaiwa ni askari walikwenda kwa mpinzani wa kisiasa wakavunja mlango alikuwepo mtoto na mke nyumbani usiku, lakini walimjeruhi na kumpiga baba wa familia na kuondoka nae, wakaacha mtoto na mke bila kuwagusa... japo ni wahalifu lakini wanafahamu hilo, sasa wewe utakuwa ni mnyama kuunga mkono huo ujinga.
Hoja yako ni mfu na haina maana...
Pia elewa Israel haikua na nia ya kuwaponya raia, imeua raia wa Gaza wakiwemo watoto kwa makusudi... Israel inadhibiti mipaka ya Gaza kwa upande wa bahari, anga na ardhi isipokuwa mpaka mdogo na Misri ambao pia hufungwa mara kwa mara... watu wa Gaza hawana pasipoti huru, hawana uwanja wa ndege, hawaruhusiwi kuvuka mpaka kiholela.
Hivyo, wakati mashambulizi yalianza, raia hawakuwa na namna ya kujinusuru, hata kama wangetaka kuondoka.
Israel haikutoa safe corridors kwa raia , badala yake ilishambulia hata maeneo yaliyotangazwa kuwa salama..
Kitendo cha kuzuia raia kutoka na kisha kuwaua kwa kisingizio cha kupambana na Hamas kinaweza kutafsiriwa kama collective punishment, adhabu ya pamoja kwa watu wote kwa kosa la wachache, jambo lililokatazwa wazi na sheria za vita.
Ikiwa kuna raia waliotaka kuondoka lakini wakazuiwa, na bado wakauwawa, hiyo ni ishara ya kukosa dhamira ya kulinda maisha ya watu wasio na hatia, hapo Israel alifanya makusudi..
hivyo kiongozi hoja yako ni dhaifu na inaonyesha uwezo wako mdogo katika kufuatilia sheria za kivita...