Wewe ni nani kuichallenge quran 17:1 unless hujui maana ya uislamu. Kuna wakristo wengi tuu na wayahudi ambao ni waislam na kuna waislam wengi tu amani si waislam, hivyo kuwa muislam ni haina nyakati maalum Uislam ni muongozo alipewa Adam As, hivyo unaenda usiobadilika kulingana na jamii husika, Yes Kuna kipindi ambacho uyahudi ndio ulikua uislam wenyewe kipindi cha nabii Suleiman,daudi, Yusuphu na wengine
Ndugu kwanini unaendelea kudanganya ? Toka nje ya box halafu ruhusu akili yako iwe huru,
Uyahudi haujawahi kuwa Uislamu,ni maji na mafuta , historia ipo wazi
neno "Uislamu" kama dini ilivyofundishwa na Qur'an na Mtume Muhammad halikuwepo katika historia kabla ya karne ya 7 B.K. Ingawa manabii wa kale kama Ibrahim, Musa, na Daudi walimtii Mungu, hawakuwahi kufundisha sala tano, kufunga Ramadhani, kwenda Hijja Makka, au kuamini Qurโan mambo ambayo ni nguzo za Uislam wa kisasa. Hivyo basi, si sahihi kihistoria kusema kwamba wao walikuwa Waislam kwa maana ya dini ya kiislamu kama ilivyo leo.
Pili, Biblia haijawahi kufundisha kwamba Uislamu ni dini ya milele iliyokuwa tangu Adam. Kwa mfano, Yesu mwenyewe aliwafundisha wanafunzi wake kusema โBaba Yetu uliye mbinguniโ (Mathayo 6:9), tofauti kabisa na fundisho la Qurโan ambalo halikubali Mungu kuitwa Baba (Qurโan 112:3 โHakuzaa wala hakuzaliwaโ). Hii ni tofauti ya msingi ambayo haiwezi kufichwa kwa hoja ya โmuongozo mmoja.โ
Tatu, kuhusu Qurโan 17:1, haifai kudai kuwa mtu hawezi kuichallenge au kuijadili kama hana Uislamu. Kila andiko la kidini liko wazi kwa uchunguzi, hoja, na tafsiri. Mathayo 7:15 inasema tuwe waangalifu tusidanganywe na manabii wa uongo. Hii ina maana tunaruhusiwa kuuliza maswali, kuchambua maandiko, na kulinganisha kama kweli ujumbe unatoka kwa Mungu au la. Mtu hawezi kudai kuwa ujumbe wake wa imani hauwezi kuguswa au kuulizwa maswali ,huo ni uoga na ujinga ,Imani lazima ihojiwe
Mwisho, historia inatuonyesha wazi kuwa Uislamu kama mfumo wa kisiasa na kijamii ulianza karne ya 7 chini ya Mtume Muhammad (s.a.w) mjini Makka na Madina. Kabla ya hapo, Wayahudi walikuwa na sheria ya Musa (Torati), na Wakristo walikuwa na injili ya Yesu. Hakuna ushahidi wa kihistoria unaothibitisha kuwa dini yao ilijulikana kama Uislamu.