Kim Jong Jr
JF-Expert Member
- Mar 15, 2014
- 12,096
- 22,468
Endelea kujidanganya tu,Hamas imefanikiwa kuharibu uhusiano mzuri uliokuwepo kati ya Israel na mataifa mengine hasa ya kiarabu, hata nchi baadhi za Ulaya tumeona zikisikitishwa kwa kile Israel inafanya.. Maandamano makubwa yamefanyika kote duniani kuunga mkono Palestina, na baadhi ya nchi zimechukua hatua kama kusimamisha uhusiano wa kidiplomasia na Israel au kutoa wito wa kuipeleka Israel Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC).
Wamefanikiwa kuionyesha dunia Israel haitishi kijeshi kama watu walivyodhani mwanzoni..
Pia wamefanikiwa kuwapa Palestinians sauti duniani wasikilizwe tofauti na mwanzoni, hii imeibua mijadala mipya kuhusu ukoloni na haki za binadamu.
Yote hayo kutokea gharama kubwa ya damu ya wapalestina imetumika...
yote na yote walichofanya Hamas Oct 7 haikuwa sahihi, walitumia zaidi hisia kuliko akili, lakini pia siwalaumu kwa sababu nao ni wanadamu, wanahisi uchungu na hawapendi kunyanyaswa... hata katika maisha yetu ya kawaida hasa kwenye mahusiano kuna watu wanauana tena mauaji ya kikatili kutokana na usaliti, kudhalilishwa n.k
Hasira isiyodhibitiwa ni hatari na inaweza kugeuza mtu mzuri kuwa muuaji au mharibifu...
Hiyo vita walioko nyuma ni wazungu hao hao wanaohadaa Dunia kuipinga.
Nchi za kiarabu kama UAE na Saud Arabia wanafurahia kuuawa Kwa Extremist hapo sema wanaaamua kutosheherekea.
Kama kweli unataka kuamini kuwa nchi za kiarabu zinaenda kinachoendelea kwanini nchi za kiarabu zimekataa kuchukua Wakimbizi wa palestina. Hawa Kila nchi inayowachukua Huwa wanaishia kufanya mapinduzi.
Misri wao wamejenga Hadi ukuta na palestina na hawataki refugee hata mmoja.