Mnondwe
JF-Expert Member
- Apr 10, 2015
- 4,013
- 3,679
Huyo nae muongo,inamaana mwenyekiti wa tume alidanganya?kama hakufanya kazi aliyotumwa uadilifu wake uko wapi?Chadema wenzangu tuombe liludishwe jamani tupate ukweli
Ajitathmini.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Huyo nae muongo,inamaana mwenyekiti wa tume alidanganya?kama hakufanya kazi aliyotumwa uadilifu wake uko wapi?Chadema wenzangu tuombe liludishwe jamani tupate ukweli
Kha! Ndo mnamuita Dr huyo, mbona hoja zake hazina mashiko na hazistahili kuongelewa na mtu mwenye hadhi-cheti cha PHD achilia mbali nafasi aliyonayo ya uwaziri.
My take: Atumwe India kwa matibabu haraka sana, mana naona ile sumu imekula kaubongo kaliko kabakia kazima kale daaah
ExactlyMwakyembe anatupa taarifa rasmi kuwa alidanganya binge wakati ule halafu kuna ndugu wanamshangilia!! Wa TZ!!?!!
Ndiyo hao-hao kwanini yeye Mwakyembe mwenye ushahidi hajafanya hima hii kesi ya Richmond ipelekwe kwenye mahakama ya mafisadi mliyoipamba hadi kwenye ilani ya CCM??Unaongelea nyusi zilizo nyonyoka baada ya kulishwa sumu na watu wa richmond?
Waziri wa habari Harrison Mwakyembe amewambia wabunge wa chadema kama wanataka ukweli wa ufisadi wa Richmond warudishe hoja hiyo bungeni.
Haya sasa karibuni kukanyagana maana hii hoja ni mwiba ambao watu wengine hawatakaki hata kuuona!
KUMBE USHAHIDI ULIOPO NI UONGO LAKINI UKWELI WANAO...! haa! watoe ukweli.
Mnyika ndo anaoSi mliunda Mahakama ya Mafisadi sasa mnashindwa nini kumshitaki ili hali mwenyewe alishasema mwenye ushahidi aende Mahakamani?
Mbona Gwajima hakubainisha siku zote mpaka alipotaka?Kwanini asibainishe siku zote?
Kama inawauma basi si ileteni ifufuliwe? Lowassa atafungwa.Saa hizi itakuwa afterthought, uongo utatungwa azima yote 2020. Kama walishindwa kuweka wazi kipindi kile baasi.
Mbona Mwakyembe anajichanganya, yeye ndiye aliye present hii ishu Bungeni na mapendekezo yake. sasa ni jukumu la bunge kuyashughulikia kama ilivyopendekezwa na wahusika wakibainika wapelekwe mahakamani. sasa leo hii the so called PhD holder anaibuka na hoja ya kipumbavu....Fumbo mfumbie mjinga mwerevu hung'amua.
Baadhi ya makamanda wa CHADEMA (hasa CHADEMA asilia) hawaitaki ndoa ya kisiasa kati ya Mbowe na Lowasa, sasa watoke vipi ni jinsi ya kuirudisha suala RICHMOND bungeni.
Mwakyembe naye kawatega waingie vichwa vichwa. Likiachwa kurudishwa bungeni, basi yatosha CHADEMA kuthibitishiwa kuwa waliyekuwa wakimtuhumu, kwenye majukwaa kuwa ni fisadi, kweli ni fisadi.
Hivyo hoja yao, ya kila siku kila akitajwa kuhusika na ufisadi, ati mwenye ushahidi atoe afikishwe mahakamani, haitakuwa na nguvu tena. Kwanza, kwa yeye kujiuzuru Uwaziri Mkuu, ilikuwa adhabu tosha kwa mtu mwenye uchu wa madaraka, kama yeye.
Lowassa alibaki Bungeni kwa miaka zaidi ya 7 Bungeni baada ya Ripoti ya Kamati Teule aliyokuwa anaiongoza Mwakyembe kuwasilishwa Bungeni na mapendekezo yake kupelekwa Serikalini. Sasa kwa muda wote huo wa miaka 7 kilimshinda nini Mwakyembe kuleta hoja hiyo Bungeni leo anataka tena iletwe na watu wengine? Yeye si ndiye mwenye huo ushahidi. Airudishe tu!!Kama inawauma basi si ileteni ifufuliwe? Lowassa atafungwa.
Hapa ishu sio Lowasa ila ripoti ya kamati ya Mwakyembe.
Choo kilihamia chumbaniMahakama ya Mafisadi haina watuhumiwa kama Lowassa ni Ufisadi kwanini asiwe mteja wa Kwanza kupelekwa??Sababu wanajua Mafisadi ni akina Mwakyembe wenyewe wanapiga Kelele tu.
Hakuna kitakachosemwa na hiki Chama Cha Mauaji kikawa kuzuri.
Aliyesema kwamba Lowassa na Kikwete ni mafisadi kwenye huu mjadala tulio nao hivi sasa si Wabunge wa CHADEMA bali ni WEWE!!Kawaulize wabunge wa chadema hilo swali
Inamaana mahakama ya mafisadi mtafugia popo mpaka lini??
Nasubiri 'reaction' yako itakuwaje, kama hao unaowatete wakiwa kwenye orodha ya washitakiwa kwenye hiyo mahakama ya kufugia pop
Mwakyembe akili yake ilinyonyoka na zile nyusi kipindi kilee.