[emoji23] [emoji23] [emoji23]
Acha kumung'unya maneno bwana...once a Yanga?...
Heheeeeee
Mimi nilianza kuipenda Yanga rasmi mwaka 2000 nilikuwa darasa la kwanza hapo,nilikuwa napenda sana kusoma magazeti.
Sasa siku moja nikakutana na habari ya Yanga...kichwa chake tu cha habari kilinisisimua sana.Hadi leo sisahau...kilisomeka
"Yanga yawasha Indiketa"
Halafu pichani alikuwepo Said Maulid 'SMG',eeeh bwana kuanzia pale nilikata shauri la kuwa shabiki wa Yanga rasmi.
Hapo kabla miaka ya 98/99 mama yangu mdogo alikuwa anapenda sana kuniita "Wewe shabiki wa Yanga"...alinijenga kwa kweli.
Guess what?Mamangu mdogo ni shabiki wa kutupwa wa Yanga na mimi ndiye afisa habari wake.
Kukiwa na game anataka nimpe updates zote na nini...[emoji12]
Ajabu baba yangu kipenzi ni shabiki wa Simba,ukitukuta tunavyotaniana utadhani hawa watu ni washkaji na sio baba na mwana.
Ila aliwahi kuniambia roho ilimuuma sana alipogundua mwanae kipenzi ni shabiki wa Yanga...club asiyoipenda maishani!
Yalaaaaaah itabidi siku moja tuwe ktk pitch tunyooshane...tena ndani ya uzi wa Madrid.
Can you imagine that?
[emoji5] [emoji5] [emoji5]