Mwalimu ajinyonga huko Moshi kisa riba kubwa ya mkopo

Watumishi wote wenye kipato duni kukopa nikama tabia, hata kama hana haja muhimu atakopa tu hysusani waalimu,......waalimu wangesitisha kukopa kwa miaka 10 tu benki nyingi zitafungwa na matajiri wengi watafirisika kabisa
 
Mwalimu mjinga na amejaa tamaa alivyochukua mkopo hakuona kama riba ni kubwa??je alilazimishwa? Mwalimu anapigwa maisha anakimbilia kujiua napata mashaka na quality ya alichokuwa anafudhisha watoto wetu.
Una umri gani? Waswahili walisema kua uyaone. Miaka ya nyuma kuna dada mmoja alijinyonga na tulipokuwa kwenye mazishi yake kuna jamaa mmoja alitoa maneno makali kuliko ya kwako. Alikuwa anakashifu na akawa anacheka kama yuko kwenye sherehe. Haikupita miezi sita tukasikia jamaa naye kanywa sumu. Siyo kwamba nakutisha wala nasema na wewe utafikwa na jambo baya, la hasha. Nataka kukujulisha kuwa mtu anayejinyonga anakuwa hayuko kwenye mental state yake ya kawaida. Wengi wanaweza kuwa wanaugua depression hivyo akili zinabadilika kabisa na kuona hakuna faida ya kuishi. Kwa kifupi elewa tu kuwa siyo yeye anafanya maamuzi bali kuna nguvu ambayo inamuongoza.
 
Una roho ngumu sana🤣
 
Waalimu wakiambiwa waikatae CCM kwani inahusika na madhila yote wanayopitia kikokotoo, mshashara duni, inapelekea kujiingiza ktk mikopo ya riba kubwa lakini hawa waalimu wanakataa siyo CCM inayosababisha haya yote kwa uchache hapo juu.
 
Inawezekana kuchukua mikopo mingi kama hivyo?


Hadi Platinum inaonekana kwenye salary slip?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…