Mwalimu wa shule ya sekondari ya Ebenezer iliyopo Sango mkoanikilimanjaro, Anthony Sulle amefariki dunia kwa kujinyonga.
Habari kutoka Moshi zinadai kuwa kabla ya kujinyonga marehemu aliandika ujumbe unaoelezea kisa cha yeye kuchukua maamuzi hayo magumu.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, ujumbe huo unadai kisa cha marehemu kuchukua maamuzi hayo ni kitendo cha Mwajiri wao kuwapa mikopo walimu yenye riba kibwa (kaushadamu)
Ujumbe huo unadai kuwa riba hiyo kubwa imemfanya kuishi kwa shida kwani kila mwisho wa mwezi amekiwa akijikuta hana chochote.
Hata hivyo mmoja wa wakurugenzi wa shule hiyo, Doreen makundi hakuwa tayari kuzungumzia tukio hilo kwa kile alichodai hahusiki Kwa namna yoyote.
Kazi kwenu waalimu na mikopo kausha damu.