Mwalimu ajinyonga huko Moshi kisa riba kubwa ya mkopo

Haya ndio mambo ya kujinyogea, sio sijui mpenzi kafanyaje, sijui maisha magumu, "hongera" watu wa Moshi kwa kujinyonga kwa mambo ya maana...
 
Huna akili.unatetea mtu kujiua kwa sababu ya kibwege ivo???

Hardtime niliyopitia na ninayopitia angekuwa huyo bwege wako ashakufa tangu 2019
 
Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, ujumbe huo unadai kisa cha marehemu kuchukua maamuzi hayo ni kitendo cha Mwajiri wao kuwapa mikopo walimu yenye riba kibwa (kaushadamu)
Kausha damu wenyewe hawana amani. Hata hao wanaokula riba kubwa wamekondeana sana tena kama hawali. Mungu anawanyonya damu hao kausha damu
 
Awamu ya sita hii utashangaa hadi huyo anaesifiwa kuupiga mwingi akajinyonga
 
Huna akili.unatetea mtu kujiua kwa sababu ya kibwege ivo???

Hardtime niliyopitia na ninayopitia angekuwa huyo bwege wako ashakufa tangu 2019
Tofauti yangu na wewe ni kwamba mimi nakwenda kwa hoja za kisayansi na siendi kwa matusi kama wewe. Watu hukabiliana na nyakati ngumu kwa njia tofauti kutokana na mchanganyiko wa mambo mengi. Na yapo mengi eg. uvumilivu wa kisaikolojia, mbinu za kukabiliana, mitandao ya kusaidia, uzoefu wa zamani, afya ya akili, na tabia za kibinafsi. Aidha, matatizo ya afya ya akili yanaweza ku-play part kubwa katika jinsi watu wanavyokabiliana na hali ngumu. Ni muhimu kutambua kwamba kila mtu ana njia au namna yake ya ku-handle matatizo, na sababu zinazochangia katika wazo la kujidhuru ni ngumu kuelezea kwani zina sura mbalimbali. Sikulaumu sana kwa sababu kama una elimu ya kubabaisha haya mambo huwezi kuyaelewa.
 
Kuna mwingine alikopa milioni4 akaenda kuwapa Q-net.Alichoahidiwa anakifahamu mwenyewe kwani huu nimwaka wapili bado analaani hicho kitendo.
 
Soma hii ripoti hapa Ripoti ya Haki za Binadamu 2023: Watu 57 walijiua, wengi wao ni wanaume vijana
 
Wewe mwenye elimu isiyo ya kubabaisha kitu gani kipya ulichoongea hapa zaidi ya blah blah za hapa na pale....mtu unayejitambua huwezi kujidhurumu uhai kwa sababu nyepesi ya madeni......nimekuuliza swali jepesi wakati anakopa hakuona kama riba ni kubwa???alilazimishwa kwa kushikiwa bastola???ulitaka aachiwe asilipe pesa za watu alizokopa ili asijiue????

Naamini hilo deni hata M15 halifiki....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…