UTATA umegubika kifo cha Mwalimu Anthony Sulle wa shule ya sekondari Ebenezer iliyopo Sango wilaya ya Moshi baada ya taarifa mpya kudai mwilivwa marehemu ulikutwa hauna nguo.
Taarifa hizi zonakuja siku chache baada ya kifocha mwalimu huyo kudai zilitokana na kuzongwa na msongo wa mawazo uliotokana na mikopo kausha damu kutoka kwa Mwajiri wake.
Habari kutoka Sango nje kidogo ya mji wa moshi zinadai kuwa kwenye eneo la tukio mwili wa marehemu ulikutwa ukiwa hauna nguo huku nguo zake zikiwa pembeni.
Inadaiwa ndani ya mfuko wa suluari ilikutwa simu ya marehemu na karatasi yenye ujumbe unaodaiwa kuelezeq sababu ya kujiua.
Hata hivyo uongozi wa shule hiyo umekataa kutoa ushirikiano kwa wanahabari kwani mmoja wa wakurugenzi wa shule Hiyo Doreen Makundi licha ya awali kuwa tayari kuzungumza,ghafla alibadirika na kudao hahusiki na jambo Hilo.
'Ndugu yangu Hilo tukio Lina utata sana,kabla ya kifo marehemu alikuwa anaongea na mtu kwenye gari aina ya Passo ,na kesho yake ndo mwili wake unaokotwa ukiwa bila nguo",anasema mtoa taarifa wetu.
Habari ya awali hii hapa chini.
Mwalimu wa shule ya sekondari ya Ebenezer iliyopo Sango mkoani Kilimanjaro, Anthony Sulle amefariki dunia kwa kujinyonga.
Habari kutoka Moshi zinadai kuwa kabla ya kujinyonga marehemu aliandika ujumbe unaoelezea kisa cha yeye kuchukua maamuzi hayo magumu.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, ujumbe huo unadai kisa cha marehemu kuchukua maamuzi hayo ni kitendo cha Mwajiri wao kuwapa mikopo walimu yenye riba kubwa (kaushadamu)
Ujumbe huo unadai kuwa riba hiyo kubwa imemfanya kuishi kwa shida kwani kila mwisho wa mwezi amekuwa akijikuta hana chochote.
Hata hivyo mmoja wa wakurugenzi wa shule hiyo ,Doreen Makundi hakuwa tayari kuzungumzia tukio kwa kile alichodai hahusiki Kwa namna yoyote.