Mwalimu alipoteza kitabu chake cha kiongozi cha mwalimu, tuliwekwa juani na kuchapwa kumbe kakisahau kwa mtoto wake

Mwalimu alipoteza kitabu chake cha kiongozi cha mwalimu, tuliwekwa juani na kuchapwa kumbe kakisahau kwa mtoto wake

Mawele

Platinum Member
Joined
Jul 25, 2023
Posts
1,161
Reaction score
4,251
kuna siku shuleni mwalimu wa Historia aliibiwa kitabu kile cha kiongozi cha mwalimu, kile ambacho huwa wanapewa vya kufundishia vinakuwa na majibu na baadhi ya mifano.

Kilitafutwa shule nzima akawa anasema wanafunzi tumekiiba, akatuzuia shule nzima kuingia madarasani tukapigishwa magoti juani tunaita ndege juu, tulichapwa sana siku hiyo.

Tukiwa katikati ya adhabu na vilio vya kutosha akaja mtoto wake ambaye alikuwa anasoma shule ya msingi ya jirani, akaja kakishika kitabu kumbe wakati wanatoka nyumbani baba alimpa mfuko mtoto wake pamoja na kitabu na alipochukua alichukua mfuko na kusahau kitabu.

Hiyo siku tulilaani sana.
 
asante kwa kutushirikisha
 
Hiyo Shule ya Msingi Mamba iliyopo Wilaya ya Chunya. mwaka 2005 Wakat nipo Darasa la Nne. Kilipotea kitabu cha kiongozi wa Mwalim cha Lugha ya Kiingereza. Mwalim wa Somo akiwa Cesilia Mdessa. Alooo tulipigwa sana juu ya kile kitabu, Funga kazi ikaja hii ya watu kupiga kura ya Siri kumtaja aliyeiba. Ooh wale wote tuliokuwa walau tunafanya Vizuri Darasani ndio kura nyingi zikatuangia. Duu kipigo kikaendelea tena na tena. Mwisho iliadhimiwa kuwa Kila Mwanafunzi achange Tsh 300 kwa ajili ya kununua hicho kitabu na kwa Wote ambao hawakuwa tayari wamechang basi adhabu yake ilikuwa kila Mwalimu wa Somo hilo akiingia kwenye kipindi Chake mnatolewa nje na Kuwekwa katikati ya Assembly na kuanza kuita Mvua mpaka kipindi kiishe.

Kitabu kimekuja patikana tuko darasa la Tano. Na aliyekuwa ameiba ni Kiongozi wa Darasa kwa wakati ule ambae alikuwa ni wa Kike
 
Back
Top Bottom