Kurzweil
JF-Expert Member
- May 25, 2011
- 6,621
- 8,411
Habari wanaJamiiForums,
Mwalimu George Ngallu wa Mahiwa Sekondari aliyekuwa na kesi mahakamani ya kufanya ngono na mwanafunzi wake wa kidato cha tano 2019/20 katika mchepuo wa History, Geography na Kiswahili (HGK) amakutwa na hatia na amehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela kuanzia tarehe 14/08/2020.
Hata hivyo Mwanafunzi naye alifukuzwa Shule na Bodi ya Shule na hata alipokata rufaa, bado Bodi ya rufaa ya Mkoa iliona bodi ya Shule ilikuwa sahihi na adhabu ya kufukuzwa Shule iliendelea.
=======
Taarifa husika iliripotiwa kama ifuatavyo;
Mwalimu wa Shule ya Sekondari Mahiwa, wilaya na mkoa wa Lindi, John Ngalu (38) amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya mkoa wa Lindi kwa tuhuma za kumbaka mwanafunzi wake anayesoma kidato cha tano.
Hayo yalielezwa jana na wakili wa serikali, Juma Maige alipozungumza na Muungwana Blog, ofisini mwake mjini Lindi.
Maige alisema Ngalu alipandishwa kizimbani tarehe 5 mwezi huu baada ya kufunguliwa kesi ya jinai yenye namba za jalada 4/2020, na kuongeza kuwa kitendo hicho kilifanyika kwenye nyumba anayoishi mwalimu huyo. Ambayo ipo katika eneo la shule hiyo.
Alisema mshitakiwa huyo alikutwa usiku baada baadhi ya wananchi ambao ni raia wema kutoa taarifa,kwa wananchi wenzao ambao walipokwenda eneo la tukio walimkuta akifanya mapenzi na mwanafunzi wake huyo.
Maige alisema inadaiwa kuwa kitendo cha namna hiyo kwa mwalimu huyo na mwanafunzi wake ni cha muda mrefu. Hali iliyo sababisha wananchi hao wamchoke na kuamua kumkamata.
Kesi hiyo itaendelea tena tarehe 13 Februari 2020. Huku Ngalu akirudishwa mahabusu baada kushindwa kutekeleza vigezo na masharti ya dhamana.
Chanzo: muhabarishaji.com

Mwalimu kizimbani kwa tuhuma ya kumbaka mwanafunzi wake