Mwalimu atelekeza kazi baada ya malipo ya mshahara wa Tsh 34,000 kwa mwezi

Mwalimu atelekeza kazi baada ya malipo ya mshahara wa Tsh 34,000 kwa mwezi

Kumbuka huyu mwalimu alikuwa na madeni lukuki, kabla ya adhabu hiyo alikuwa na makato mengi.

Kazi ya ualimu ina laana, maana Walimu wengi wanaishi maisha magumu.
Wenye maisha mazuri hawaandiki hivi
 
Nimesikitishwa kupata habari kuhusu mwalimu anayefundisha shule ya sekondari Dunda iliyopo Bagamoyo mkoa wa Pwani kukimbia kazi ya ualimu baada ya kulipwa 34000 kwa mwezi.

Hii inatokana na adhabu ya kushushwa cheo na kulipwa nusu mshahara na Tume ya Utumishi wa Walimu kwa kosa la utoro kazini.

Mwalimu huyo wa kike aliishi maisha magumu sana hapo hapo shuleni ,alikosa mpaka hela ya kula ilimlazimu auze miwa na maembe aliyoyaokota hapo shuleni ili apate pesa ya kula.

Uzalendo ukamshinda baada ya mazingira magumu ya kazi aliamua kuondoka kazini bila ya taarifa kwa muajiri.

Habari nilizozipata mwalimu huyo yupo Mlandizi akifanya kazi ya kuhudumia wateja bar.

TSC mnapotoa adhabu ya kupunguza mishahara kwa walimu mzingatie iwapo kama mtuhumiwa ana mikopo benki, isitoshe adhabu ya kupunguza mshahara ni ya kikatili maana mshahara wenyewe hautoshi hapo hapo mnaupunguza.

Habari nilizozipata huyu mwalimu alikuwa na madeni benki na taasisi za fedha hapo Bagamoyo.

Kutokana na mazingira magumu ya kazi mwalimu huyo kaamua kutelekeza kazi yake.
Naamini kuna zaidi ya haya uliyoandika. Umewahoji waajiri wake au viongozi wake shuleni alikokuwa akifundisha? Umemhoji yeye mwenyewe akakupa uhalisia wa maswahibu yake? Umemhoji hata mtu wake wa karibu?
 
Bila kusikiliza Upande wa pili huu ni Uzushi tu!! Mikopo huwa inawagharimu sana,Mwingine amekopa pesa kala bata na huku makato yanaendelea akiangalia anaona anafanya kazi bure....Morally wa kazi utoke wapi?
 
Walimu waboreshewe maslahi kama wabunge.

Nilisikia report ya katibu mkuu wa tume ya Utumishi wa Walimu kwamba asilimia 50 ya Walimu wamefukuzwa kazi kwa utoro baada ya kuishi ktk mazingira magumu.

Mbona hatusikii idadi hiyo kuacha kazi Benki Kuu, TRA, Uhamiaji, Bandari, Jeshi?
Kima cha chini kwa mwl mwenye certificate ni sh ngapi
 
Wa zamani sio siku hizi.
Graduate anavuta sio chini ya laki 8 akiwa na masters anavuta 1.8.
Ukipata Kazi ya ualimu omba vijijini life is simple Hakuna kufatiliana baada ya Kazi piga ujasilimali.
Timiza wajibu wako wasome wasisome shauri yao na wazazi wao ukijifanya unawafatilia fatilia Ili wasome watakuroga.
Anaetaka kusoma mpe ushirikiano.
Wikiendi kuwa bize kwenye mishe zako.
Umeifafanua vzr, nadhani mlalamikaji ana mikopo mingi, kupanga ni kuchagua
 
Let’s say alikuwa na netpay ya 468,000 na jumla ya makato yalikuwa 200,000.
Ukiigawa nusu na bank wakakata chao unabaki na 34,000 ikutunze kwa siku 30 zijazo. Mmmmae naacha kazi.

Mwajiriwa na madeni ni pete na kidole, pengine ukute huo utoro kazini chanzo ni kujiongeza kutafuta kipato cha ziada baada ya maisha kuwa magumu pale unapokopa na kuwekeza kwenye ujenzi na pesa ikakata kwenye renta.
Nini maana ya net pay
 
Sijauliza anadaiwa na taasisi ipi, nimeuliza peza za mikopo ziko wapi?
Mkuu umeshawahi pitia maisha ya kipato cha chini kama ya walimu wa msingi na hata sekondari? Unadhani kwa huo mshahara wake anaweza hata kukopa milioni kumi au anaenda kukopa ili anunue gari au afanyie biashara kubwa? Ukiwa na kipato kama cha hawa walimu, mkopo wenyewe hata haufiki milioni 5, halafu unakuta amekopa pesa hiyo labda aweke sawa mambo ya familia kama kulipa ada, kujenga choo, n.k.

Pia tukumbuke si kila mkopo unaenda kuzalisha na si kila mkopo uliochukuliwa ukazalishe utafanikiwa kwa hizi riba zetu Tanzania. Wanaofanikiwa kirahisi ni wale wanaokopa, huku pembeni wanakula kwa urefu wa kamba zao. Sasa mwalimu wa watu hawezi kula chaki.
 
Mi nimeuliza mkopo aliokopa uko wapi? Wewe unaleta risala? What for? Kama kachinmba choo tupewe jibu, kama kaenda kulipa ada tupewe jibu, simple.
 
Kumbuka huyu mwalimu alikuwa na madeni lukuki, kabla ya adhabu hiyo alikuwa na makato mengi.

Kazi ya ualimu ina laana, maana Walimu wengi wanaishi maisha magumu.
Yeye ndio laana,hakuna mshahara wa hivyo
 
Hua kuna 1/3 hakuna bank inayozidi makato hayo,Sema mwandishi kasema alipewa adhabu ieleweke
 
Back
Top Bottom