Mwalimu atelekeza kazi baada ya malipo ya mshahara wa Tsh 34,000 kwa mwezi

Kumbuka huyu mwalimu alikuwa na madeni lukuki, kabla ya adhabu hiyo alikuwa na makato mengi.

Kazi ya ualimu ina laana, maana Walimu wengi wanaishi maisha magumu.
Wenye maisha mazuri hawaandiki hivi
 
Naamini kuna zaidi ya haya uliyoandika. Umewahoji waajiri wake au viongozi wake shuleni alikokuwa akifundisha? Umemhoji yeye mwenyewe akakupa uhalisia wa maswahibu yake? Umemhoji hata mtu wake wa karibu?
 
Bila kusikiliza Upande wa pili huu ni Uzushi tu!! Mikopo huwa inawagharimu sana,Mwingine amekopa pesa kala bata na huku makato yanaendelea akiangalia anaona anafanya kazi bure....Morally wa kazi utoke wapi?
 
Kima cha chini kwa mwl mwenye certificate ni sh ngapi
 
Umeifafanua vzr, nadhani mlalamikaji ana mikopo mingi, kupanga ni kuchagua
 
Nini maana ya net pay
 
Sijauliza anadaiwa na taasisi ipi, nimeuliza peza za mikopo ziko wapi?
Mkuu umeshawahi pitia maisha ya kipato cha chini kama ya walimu wa msingi na hata sekondari? Unadhani kwa huo mshahara wake anaweza hata kukopa milioni kumi au anaenda kukopa ili anunue gari au afanyie biashara kubwa? Ukiwa na kipato kama cha hawa walimu, mkopo wenyewe hata haufiki milioni 5, halafu unakuta amekopa pesa hiyo labda aweke sawa mambo ya familia kama kulipa ada, kujenga choo, n.k.

Pia tukumbuke si kila mkopo unaenda kuzalisha na si kila mkopo uliochukuliwa ukazalishe utafanikiwa kwa hizi riba zetu Tanzania. Wanaofanikiwa kirahisi ni wale wanaokopa, huku pembeni wanakula kwa urefu wa kamba zao. Sasa mwalimu wa watu hawezi kula chaki.
 
Mi nimeuliza mkopo aliokopa uko wapi? Wewe unaleta risala? What for? Kama kachinmba choo tupewe jibu, kama kaenda kulipa ada tupewe jibu, simple.
 
Kumbuka huyu mwalimu alikuwa na madeni lukuki, kabla ya adhabu hiyo alikuwa na makato mengi.

Kazi ya ualimu ina laana, maana Walimu wengi wanaishi maisha magumu.
Yeye ndio laana,hakuna mshahara wa hivyo
 
Hua kuna 1/3 hakuna bank inayozidi makato hayo,Sema mwandishi kasema alipewa adhabu ieleweke
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…