Mwalimu Jambau wa Singida apewe tuzo ya heshima na NCHI kwa kuvumbua vipaji vya watoto na kuhakikisha wanakuwa wanariadha wakubwa duniani

Mwalimu Jambau wa Singida apewe tuzo ya heshima na NCHI kwa kuvumbua vipaji vya watoto na kuhakikisha wanakuwa wanariadha wakubwa duniani

MamaSamia2025

JF-Expert Member
Joined
Mar 29, 2012
Posts
21,387
Reaction score
44,030
Kuna watu wachache sana duniani ambao pesa sio kipaumbele chao cha kwanza maishani. Yaani wanaweza fanya kitu bila kuzingatia maslahi yoyote ya kifedha. Mwalimu Jambau wa shule ya msingi Lighwa huko Singida ni miongoni mwao. Hauwezi kuzungumzia mafanikio ya wanariadha wakubwa toka mkoani Singida kama Alphonce Simbu ukaacha kumtaja Mwalimu Jambau pichani.

Binafsi nilimfahamu Mwalimu Jambau mwanzoni mwa miaka ya 2000 mkoani Arusha. Yeye alikuwa akiwaleta wanariadha chipukizi toka Singida kujiunga na clubs za riadha zilizokuwa mjini Arusha wakati huo. Kulikuwa na Team100, Timmax na nyingine kadhaa. Huyu mwalimu alikuwa anawaleta watoto wa kinyaturu na kinyiramba wakiwa wadogo sana waje kupata mafunzo na wengine kumalizia masomo Arusha ili baadae kuwa wanariadha pro.

Ninakumbuka alimleta Simbu mjini akiwa na umri wa miaka 14 ikabidi Simbu aachwe kwanza amalize kidato cha nne ndo aingie rasmi kwenye training ya riadha. Simbu ni miongoni mwa wanariadha wachache sana wa kiafrika ambao hawajadanganya umri ndo maana bado yuko fit kwa miaka mingi. Umri wake ni halisi.

Chama cha riadha, BMT, TOC na wizara husika fanyeni jambo kwa kuutambua mchango wa Mwalimu Jambau kwa mchezo wa riadha nchini.
 

Attachments

  • Screenshot_20260529-110403_Instagram.jpg
    Screenshot_20260529-110403_Instagram.jpg
    59.9 KB · Views: 19
Ni jambo jema ✅ .
Waziri wa michezo ni jukumu lako kusimamia na kulea vipaji vya michezo ili kukuza ustawi kwenye jamii .
 
Back
Top Bottom